Ajali jamani tena?

Magulumangu

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
3,047
452
Wakuu nimepata habari leo kuna ajali ya basi la Najimunisa limeua lkn sijui ni wangapi na lilikuwa linaenda wa\pi ila barabara ni ya Dar Mza ila yawezakuwa lilikuwa linaenda Bukoba au kahama...mwenye deteili zaidi jamani nijuzeni......Mungu aweke roho za marehemu pema peponi...amina...
 
Wanasema limeua zaidi ya watu 19 na majeruhi kibao lilikuwa likitokea dar kwendaa Bukoba..ajali imetokea maeneo ya Bukombe inasemekana ilikuwa ni ushindani wa kuovatake ndo ikasababisha yote hayo.Naona mpaka kuelekea mwisho wa mwaka tutegemee mengi sana ya namna hii.Mungu azilaze roho za marehemu wasio na hati mahali pema peponi
 
dah asante mkuu maana jamaa yangu pia amefariki katika ajali hiyo...nimeumia sana maana ni mtu wa karibu sana na mimi anyway alietoa ndiye aliyetwaa na jina lake lihimidiwe...na hiyo lami we acha tu watatumaliza kwa kweli...
 
Kwanza pole sana kwa msiba wa jamaa yako wa karibu..afu nimepita pale sunday tu ile barabara inafanyiwa ukarabati mkubwa toka kahama mpaka rwanda so ile lami ya zaman inabanduliwa na weka nyingine kiwango zaidi.wanasema Kagema katoa fungu kujazia lile la msaada wa benki ya africa.
 
Hivi ni lini serikali itakuwa serious na hii issue, watu wanakufa kila kukicha na hakuna kinachofanyika. Nionavyo mimi hawa madereva wanastahili kupewa adhabu sawa na wauaji wengine, na matajiri inabidi washikishwe adabu maana baadhi yao wanachochea hizi ajali kwa ushindani kati yao. Wanaajiri madereva wahuni na wengi wao leseni wamezipata kupitia mlango wa nyuma. Tufike mahali matajiri wafidie wafiwa na wale repeat offenders wapewe adhabu za vifungo, faini na kama vipi wafutiwe leseni.
 
Hizi ajali zitaendelea kutumaliza kwa vile serikali yetu haioni umuhimu wa kufanyia kazi sheria za barabarani na kuwachukulia hatua kali wanaotoa leseni feki,madereva wanao vunja sheria,polisi wa barabarani wanao pokea rushwa na kurekebisha barabara zetu mbovu.

Ajali zinatumaliza kama kuku lakini husikii kitu chochote kutoka kwa viongozi wa nchi yetu wanachukulia jambo la kawaida kwao.

Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi na atuepushe na ajali zaidi.
 
Kwanza pole sana kwa msiba wa jamaa yako wa karibu..afu nimepita pale sunday tu ile barabara inafanyiwa ukarabati mkubwa toka kahama mpaka rwanda so ile lami ya zaman inabanduliwa na weka nyingine kiwango zaidi.wanasema Kagema katoa fungu kujazia lile la msaada wa benki ya africa.
mkuu mie ndo home huko kila nikikamata njia either mza au kahama...si mmoja tu nadhani jamaa zangu waloumia pia watakuwepo wengi tu maana kila siku wanasafiri...tunashukru kwa lami na pia je madereva na matajiri itakuwaje ajali maana zinazidi ongezeka...nilipita huko mwaka jana mwezi wa saba...mza imekuwa waja leo warudi kesho...
 
BASI LA NAJMUNISA LAPATA AJALI NA KUSABABISHA VIFO KADHAA!!

Ajali ya Kanegele - Fuso na Super Najimunisa Kahama Mkoani Shinyanga jana kama unavyoona picha mbalimbali zilizochukuliwa eneo la tukio mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo inayodaiwa kusababisha vifo vya watu 18 . Cha ajabu ajali imetokea mita 10 kutoka katika kizuizi cha askari wa maliasili wanaokagua mazao ya maliasili.
Katika ajali hiyo inasemekana askari aliyekuwa akisindikiza basi hilo alikatwa kicha baada ya fuso kuharibiwa vibaya na basi. hebu Jionee mwenyewe picha zilizopigwa katikaajali eneo la tukio huko Kanegele kama inavyoonekana Sura ya Basi la Super Najimunisa baada ya Ajali.(Picha na Bernard Kinte wa mtandao wa Wanabidii)​
Waokoaji wakitafuta maiti ndani ya Fuso. Eneo la ajali-Kwenye kizuizi cha Kanegele. Baadhi ya wananchi walioshuhudia ajali hiyo wakichungulia Maiti zilizopakjiwa ndani ya magari aina ya Toyota Landcruiser hardtop. Askari wa usalama Barabarani katika eneo la ajali

ANGALIZO:Ajali hii imetokea karibu kabisa na ROAD BLOCK.....how can this happen??Kwenye vizuizi hivi si magari huwa yanapita taratibu sana kwani kuna ukaguzi hapo au mimi sielewi hizo road block ni za nini.
 
Hakuna wa kuwajibika na hizi ajali?????? Innocent people are dying just like that.....

Poleni sana wafiwa
 
Back
Top Bottom