Ajali iliyotokea Kilwa rd. leo

Buza

Member
Aug 7, 2011
57
14
Ajali iliyotokea ktk barabara ya Kilwa ya gari aina rav4, air bag vipi. Wanasema gari ilipinduka zaidi ya mara 3 lakini air bag haikutoka inakuwaje? Msaada p/z.
 
airbag zina expire, inatakiwa kila baada ya miaka kumi zifanyiwe service la sivyo haziwezi fanya kazi sawasawa ,pia zina sensor kwa hiyo kama ajali sio head collision haziwezi kufunguka hasa kama ziko kwenye steering na dashboard
 
Air bag mara nyingi hu-deploy kama kuna impacts. Kama gari likipinduka bila kugonga kitu chochote basi airbag haitadeploy. Hivyo hili si tatizo la gari wala mfumo wa airbag bali mechanism.
 
Gari haiwezi kupinduka bila kugonga kitu chochote, hata ingebiduka hewani hewani ingeishia kupiga ardhini, hakuna kitu kinachoweza kupinduka bila kuwa na impact! Excuse me but you are not making any sense!
 
Hujawahi kuendesha gari ndio maana unasema hivyo....
Gari inaweza kupinduka kwenye corner kali sana na rough driving pasipo kugonga kitu chochote
 
Air Bags need frequent services as car enginer does.Hapa Tanzania no one take this serious.
 
Hujawahi kuendesha gari ndio maana unasema hivyo....
Gari inaweza kupinduka kwenye corner kali sana na rough driving pasipo kugonga kitu chochote
Gari inapopinduka body linagonga ardhi, hiyo tayari ni impact! Gari haiwezi kupinduka bila impact!
 
Nadhani jibu kuhusu airbag limepatikana, tupe zaidi kuhusiana na hiyo ajali kuna vifo au majeruhi?
 
Hujawahi kuendesha gari ndio maana unasema hivyo....
Gari inaweza kupinduka kwenye corner kali sana na rough driving pasipo kugonga kitu chochote

Msamehe bure huyo layman maana comment yake inadhihirisha wazi kuwa ni maamuma wa magari, japo angejua hata gari ikipata pancha (hasa tairi la mbele) ikiwa katika mwendo mkali linaweza kupinduka! je kuna collision yoyote hapo kabla ya kupinduka?
 
Hata kama cause ya ajali ya gari kupinduka ni pancha, at certain point gari hilo lita fanya contact na ardhi ambayo itaresult katika kutoa impact flani...vilevile gari hilo linapo "come to rest" litafanya impact ya kiwango flani na ardhi. Sasa swali ni at that point kwanini air bags zisi deploy?
 
Gari haiwezi kupinduka bila kugonga kitu chochote, hata ingebiduka hewani hewani ingeishia kupiga ardhini, hakuna kitu kinachoweza kupinduka bila kuwa na impact! Excuse me but you are not making any sense!
Msome mshana jr hapo juu,ni lazima iwe iwe impact ya uso kwa uso na siyo impact ya aina yoyote inaweza kufungua airbag.Inawezekana hii gari ilikuwa inatua kwa mgongo na matairi alternatively!
 
Ok....kama zinafunguka ajali inapokuwa ya uso kwa uso tu hapo sawa...
 
Hakuwa amefunga seat belt.seatbelt tensioner huwa zinatuma taarifa kwenye mifumo ya usalama ya gari ili kudeploy airbargs hasa likipinduka.la sivyo unaweza kuzIma pia.zikawa hazifanyi kazi

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Kweli bwana, hata mimi ilinikuta hiyo. Nimepinduka kwa kulalia mgongo wa gari na kisha kusimama kwa mataili nje ya barabara na kusimama kwa kugeukia nilikotokea, lakini airbag haikudeploy. Dikugonga kutu sababu nilikuwa namkwepa mwendesha Fuso aliyebeba nyaya toka mikoani pale Ruvu Sekondari saa 11.30 alfajiri. Si unajua wanawahi sokoni kutua mzigo na wanalala huku wanaendesha, alikuwa ananijia uso kwa uso nami nikiwa na familia nzima naenda mikoani, sikutaka kuimaliza familia yangu yote hapo, kumkwepa nikajikuta naticktack. Mungu alivyo mwaminifu, gari ikawa nyang'anyang'a lakini hakuna binadamu aliyechunika mahali popote ingawa wind screen ilikuwa neti tayari. Kwa hiyo I buy the idea kwamba kugonga head on pengine ndio maudhui ya airbags. Asante kwa shule mliyoitoa.
 
Mkuu ni lazima iwe ya on head collision ndiyo airbags zinatoka siyo ma impact ya ubavuni.
 
Gari haiwezi kupinduka bila kugonga kitu chochote, hata ingebiduka hewani hewani ingeishia kupiga ardhini, hakuna kitu kinachoweza kupinduka bila kuwa na impact! Excuse me but you are not making any sense!

Mkuu hadi ubamize pale mbele, ukiviringika na usibamize mbele airbag hazitafumuka!
 
Hakuwa amefunga seat belt.seatbelt tensioner huwa zinatuma taarifa kwenye mifumo ya usalama ya gari ili kudeploy airbargs hasa likipinduka.la sivyo unaweza kuzIma pia.zikawa hazifanyi kazi

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums

Ni kweli ila kuna baadhi ya magari hata usipofunga mkanda. Ile impact inatosha kufumua airbags. Ila inabidi ubamize mbele.
 
Mkuu ni lazima iwe ya on head collision ndiyo airbags zinatoka siyo ma impact ya ubavuni.
..You have said it all KImbweka. Airbag hu-deploy pale tu kunapokuwa na head on collision na si vinginevyo. Nimekuwa nafatila sana vipindi vya Megafactory (NatGeographic Channel) hujitahidi kuonyesha jinsi airbag inaweza kusaidia kupunguza madhara kwa waliomo kwenye gari husika. Na huonyesha jinsi gari inapogonga kitu kigumu kwa mbele ambavyo airbag inatoka na kumkinga abiria. Ajali ya Kilwa road niliona kwenye Tv ile gari ni RAV 4 new model nina imani itakuwa na air bag lakini kwa mazingira ya ajali airbag isige-deploy..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom