Yona F. Maro
R I P
- Nov 2, 2006
- 4,202
- 218
Leo Kwa mara ya kwanza nimebahatika kukutwa na ajali ya basi lakini dereva alifanikiwa kukwepa gari ya mbele na kuingiza gari porini baadaye wakalitoa na tukaendelea na safari kama kawaida
Nashukuru kwamba nimefika salama mkoani arusha , Dereva aliyekuwa anaendesha basi letu alikuwa anakunywa maji ndio ghafla akakutana na gari lingine la mizigo lilitokuwa limebeba nguzo za tanesco , Eneo lile ni eneo lenye upepo sana pamoja na kona kona , watu wengi wanaopita pale huwa wanashauriwa kupunguza mwendo kwa sababu hizo dereva wetu hakupunguza mwendo aliendelea ndio ghafla kwenye kona kukawa na gari hilo akaamua kuingiza gari porini .
Ingawa abiria wengi sana walitaka kushuka kwenye gari kwenda kumpiga dereva mwenye hiyo gari ya mizigo lakini baadaye gari liliondoka ndio baadaye sasa tukawa tunaangalia jinsi dereva anavyoendesha karibu ye hedaru kukawa na gari lingine la mizigo kama lile lile akaendelea kunywa maji yake pamoja na kupiga story na baadhi ya watu waliokuwa pale mbele napo akataka kufanya vituko ndio lawama sasa zikaanza kushushiwa upande wake .
Baada ya hapo kuna Sehemu nyingine ukitoka kwenye daraja kabla ya kufika kwa saddala kuna mlima pale na kona , alijaribu kupita gari zingine 3 coaster zenye abiria waliokuwa wanakuja arusha watu wakampigia kelele lakini hakusikia
Angalau tumefika salama namba za gari hilo ni 3644 Happy Nation la saa 12 nimejaribu kumpigia mwenye namba ambayo imeandikwa kwenye tiketi ambayo ni 0754 668389 Lakini haipatikani pamoja na yote hata hawakuandika majina ya abiria ambao walikuwemo ndani ya gari lao .
Natakiwa kwenda kufanya shuguli zingine sasa , Jioni Njema