AJALI: Basi la UDA laigonga treni eneo la Gerezani - Kariakoo, Dar

mfumo mbovu sana wa mtu Kusimama road na bendera eti anazuia gari ,siku atagongwa mshika kibendera,sijuw ni mapesa wangapi yanahitajika kuweka uzio automatic gari moshi ikiwa mita kadhaa kabla ya kuvuka na kujifungua ikipita nimeona nchi za wenzetu ni bora na salama100%
 
Innalillah ila haikuwa na hajaa dereva kukimbiaa coz mwisho wasiku utakamatwa au utaishi maisha yakuhamahama miji
 
Kuuliza si ujinga. Hivi dereva wa treni huwa haruhusiwi kusimama kwa dharura anapoona kuna gari mbele yake? Manake huwa naona wanaishia kupiga honi tu lakini mwendo ule ule
 
Poleni sana wahanga wa ajali hiyo, anaefahamu ilikiwaje ikatokea ajali naomba anifahamishe.
 
Manahodha wa tren walishaambiwa tren haigongi bali hugongwa na ndo maana tren haina mataa yenyewe inapita tu
 
Pole kwa wote waliopoteza ndugu zao ktk ajali hii.. Nilikuwa aneo la tukio lkn pia nielekeze lawama kwa wafanyakazi wa TRL coz sehemu iliyotokea ajali kuna geti na zime wekwa kwa ajili ya kufunga barabara pindi treni inapopita sasa wahusika wanao tabu gani kuzishusha wakati treni inapita

Sina uhakika na ufungaji wa geti kwa TRL lakini kwa upande wa dereva wa gari ni lazima kusimama kabla ya kuvuka reli yoyote ile na kuangalia kulia na kushoto kama vile mtu anapovuka barabara.
 
Hivi treni hainaga breki au breki zake sio Kali????
Au madereva wake wameelekezwa wasiwe wanafunga breki wanapoona magari yameingia kwenye reli????
Naomba maelekezo wataalam
 
Hivi treni hainaga breki au breki zake sio Kali????
Au madereva wake wameelekezwa wasiwe wanafunga breki wanapoona magari yameingia kwenye reli????
Naomba maelekezo wataalam

Kiwango cha elimu yako?...........taaluma?............... ili nijaribu kukujibu kulingana na kiwango chako kama nitaweza.
 
Kwanza ieleweke kwamba ajali iliyotokea ilikuwa ni kichwa cha treni na haikuwa na mabehewa.. Pili ni rahisi sana ku control na kupunguza mwendo ikiwa huna mabehewa lkn lile neno kuwa treni haingongwi ndio linalowapa nguvu hao TRL
 
  • Thanks
Reactions: MTS
Hivi treni hainaga breki au breki zake sio Kali????
Au madereva wake wameelekezwa wasiwe wanafunga breki wanapoona magari yameingia kwenye reli????
Naomba maelekezo wataalam

Poleni sana inasikitisha, ila mimi naona mfumo wetu haujarekebishwa, kwenye nchi za wenzetu treni zikiingia mijini huo zinaongozwa na mataa na wakati mwingine askari wa usalama barabarani pia wanaongoza treni pamoja na magari kama kuna jam. hapa kwetu bado tunafuata mfumo wa zamani sana kipindi cha miaka ya nyuma haujafanyiwa mabadiliko mpaka sasa. wakati ule magari yalikuwa machache sana... hivyo inawezekana mkuu treni ikiingia mjini ifuate taratibu...
 
mfumo mbovu sana wa mtu Kusimama road na bendera eti anazuia gari ,siku atagongwa mshika kibendera,sijuw ni mapesa wangapi yanahitajika kuweka uzio automatic gari moshi ikiwa mita kadhaa kabla ya kuvuka na kujifungua ikipita nimeona nchi za wenzetu ni bora na salama100%
Nchi hii si kila jambo ni majaribio na kibendera usiku hakionekani
 
Tanzania haina mfumo wa tahadhari madhubuti wa kiusalama. Pamoja na dereva wa gari kutakiwa kuchukua tahadhari anapokatisha reli, kulistahili kuwepo na automatic barriers maeneo yote kwenye crossing ili treni ikiwa imefika umbali fulani barrier inafunga. Na kama kuna kuwa na dereva kichaa gari yake imefungiwa kwenye reli, anashughulikiwa mara moja, na abiria wote wanatolewa kwenye hiyo gari.

Mifumo yetu ya usalama inategemea mno maneno, wakati tunajua kuwa si wakati wote watu huwa wanatii maneno. Siyo sahihi mfumo wa usalama kutegemea njia moja tu yaani kuwakumbusha madereva. Wale OSHA wanatakiwa kufukuzwa, sioni umakini wao.
 
Kwa ajalivyotokea kuna kila dalili DREVA alikuwa anawahi mataa ya kamata bila kujali taratibu za uingiaji njia ya treni,
 
Poleni sana inasikitisha, ila mimi naona mfumo wetu haujarekebishwa, kwenye nchi za wenzetu treni zikiingia mijini huo zinaongozwa na mataa na wakati mwingine askari wa usalama barabarani pia wanaongoza treni pamoja na magari kama kuna jam. hapa kwetu bado tunafuata mfumo wa zamani sana kipindi cha miaka ya nyuma haujafanyiwa mabadiliko mpaka sasa. wakati ule magari yalikuwa machache sana... hivyo inawezekana mkuu treni ikiingia mjini ifuate taratibu...

Umeelekea kwenye pointi nzuri, ingekuwa vema kama kungekuwa na taa badala ya mshika bendera. kwakuwa mshika bendera yawezekana usimuone kwa haraka. dereva chukua tahadhari
 
Back
Top Bottom