AJALI: Basi la UDA laigonga treni eneo la Gerezani - Kariakoo, Dar

Ekyoma

JF-Expert Member
Dec 30, 2015
2,177
2,802
Ajali mbaya sana imetokea muda huu Kariakoo Gerezani, watu sita wamepoteza maisha papo hapo akiwemo konda wa kampuni ya Uda dereva kakimbia. Mungu awalaze mahali pema wote waliopoteza maisha

1469562866654.jpg
1469562890012.jpg
1469562902233.jpg

image.jpeg
 
Kuna shida kubwa sana hasa maeneo ambapo treni linakatisha. Juzi kidogo niiache dunia kwa sababu ya uzembe wa dereva wa daladala.

Tulikuwa Karume pale reli inapokatisha. Dereva kakimbiza gari ile anawahi foleni na taa za makutano ya Pugu na Kawawa road.

Kabla hatujafika relini kibendera kanyoosha kibendera sijui dereva hakumuona au alimpuuza. Ile tunafika kwenye reli gari ikawa inacheza tu kucheki kushoto kwangu kichwa cha treni kinakuja kasi balaa na kelele za honi.

Nilipokiona nguvu ziliisha maana abiria wote tukawa tushachanganyikiwa hatujui la kufanya. Kama muujiza ila kichwa kimebakiza mita chache kama tano basi likafanikiwa kutoka pale. Sikuamini maana kichwa cha treni kilipita nyuma yangu hata siamini kimepita vipi. Naamini kama tungegongwa siku ile wengi wangefariki.

Nashauri trafic watafute utaratibu mzuri pale maana kuna maeneo yana shida sana hasa pale Karume na Buguruni. Kuna siku itatokea ajali kubwa sana na kulihuzunisha taifa.

Mungu aweke roho za marehemu mahala pema peponi. Na awajalie majeruhi wepesi na kuwaponya majeraha.
 
Madereva kwa wanacheza na roho za watu, tena wakirekebishwa wanakua wakali sana..

Alafu wakisababisha ajari, wanakimbia
 
MWENYEZI MUNGU awarehemu & kuwapa mioyo imara wafiwa wote.

Tupo pamoja nao katika kipindi hiki kigumu.
 
Kuna shida kubwa sana hasa maeneo ambapo treni linakatisha. Juzi kidogo niiache dunia kwa sababu ya uzembe wa dereva wa daladala.

Tulikuwa Karume pale reli inapokatisha. Dereva kakimbiza gari ile anawahi foleni na taa za makutano ya Pugu na Kawawa road.

Kabla hatujafika relini kibendera kanyoosha kibendera sijui dereva hakumuona au alimpuuza. Ile tunafika kwenye reli gari ikawa inacheza tu kucheki kushoto kwangu kichwa cha treni kinakuja kasi balaa na kelele za honi.

Nilipokiona nguvu ziliisha maana abiria wote tukawa tushachanganyikiwa hatujui la kufanya. Kama muujiza ila kichwa kimebakiza mita chache kama tano basi likafanikiwa kutoka pale. Sikuamini maana kichwa cha treni kilipita nyuma yangu hata siamini kimepita vipi. Naamini kama tungegongwa siku ile wengi wangefariki.

Nashauri trafic watafute utaratibu mzuri pale maana kuna maeneo yana shida sana hasa pale Karume na Buguruni. Kuna siku itatokea ajali kubwa sana na kulihuzunisha taifa.

Mungu aweke roho za marehemu mahala pema peponi. Na awajalie majeruhi wepesi na kuwaponya majeraha.
Madereva wamekua wazembe sana..pole sana.mkuuu sehemu nyingine italiza watu ni pale relini gari za gongo la mboto na mbagala zikiwa zinafukuzana zinapitaga pale utadhan hamna kitu
 
Back
Top Bottom