AJALI: Basi la Simba Mtoto lagongana na Lori na kusababisha vifo 11, majeruhi 26 Korogwe, Tanga

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Watu kadhaa wamejuruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la Simba Mtoto na Lori la mizigo, Korogwe Mkoani Tanga, watu kadhaa (idadi bado haijajulikana) wabahofiwa kupoteza maisha.

Kamanda wa Polisi Mkoani humo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

1455173103994.jpg


1455173116272.jpg


1455173126391.jpg


1455173136502.jpg


===============

WATU 11 wamefariki dunia huku wengine 26 wakijeruhiwa, wanne kati yao wakiwa chumba cha wagonjwa mahututi katika hospitali teule ya wilaya ya Muheza mkoani Tanga, kutokana na ajali ya gari.

Ajali hiyo imetokea leo majira ya saa 1 asubuhi katika eneo la Tanga Mlima mkoani Tanga, iliyohusisha basi la kampuni ya Simba Mtoto lenye namba za usajili T 393 DBZ na lori aina ya Scania lenye namba T 738 CFE ambalo lilikuwa limebeba mchanga.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Mihayo Msikhela, amesema chanzo cha ajali hiyo ni dereva wa lori kusinzia na kuhama njia, kulikopelekea kwenda kugongana na basi hilo lililokuwa likitoka mkoani Tanga.

Kamanda Msikhela amesema majeruhi hao kwa sasa wako hospitali ya Muheza na 24 kati yao wanaendelea vizuri, huku watu 11 waliofariki, wanaume nane na wanawake watatu, akiwemo mtoto wa miaka miwili na nusu wote wakiwa wa familia moja.
 
Mungu Awape TAHFF Ya Haraka Ya Waliojeruhiwa Na Kama Kuna Waliofariki, Mungu Awasamehe Madhambi Yao Na Awapumzishe Pahala Pema!!! PIA Awape Moyo Wa Subira, Wanafamilia Ambao Nd Zao Wamefikwa Na Madhira Hayo!!!
 
Huyo jamaa anaonekana kabanwa hapo mbele, hajafariki kweli....!!!
 
innalillah wainnah illah rajjiun, na allah (s.w) awafanyie tahfifu majeruhi in shaa allah.
 
Hao madereva nao wawe wanapimwa, huwa wanatumia viroba; ajali zimekuwa nyingi mno.

Pole wafiwa wote.
 
Yaani mpaka cabin ya roli imeishia hapo Mbele ya bus mpaka imegandia
 
aisee roho imiuma sana poleni majeruhi na wafiwa MUNGU awape nguvu,hayo maeneo yana konakona mbaya sana
 
Back
Top Bottom