Ajabu! Polisi wa misri nao waandamana

MAMMAMIA

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
3,811
1,603
Wakati Mubarak alipokuwa Madarakani, Polisi (walamba buti) wa Misri walikuwa wako mbele katika kuwanyanyasa raia, kuwasweka lupango, kuwababambikizia kesi na hata kuwafunga bila ya kujua sababu. Hata siku za mwanzo za maandamano walianza kuua hadi pale jeshi lilipoingilia kati. Cha ajabu, kwa kuwa sasa Mubarak ameondoka, nao wameanza maandamano na migomo kudai maslahi bora.

Polisi wetu Tanzania, amkeni na mujifunze kwa wenzenu. Serikali haiwatakii maslahi bora, bali chombo cha kuwakandamiza wananchi wenzenu.
 
Ni kweli juzi na jana walikuwa wanaandamana tena kwa wingi sio mchezo.
Walisema wazi kuwa walichokuwa wakikifanya kilikuwa ni kwa sababu ya amri ya Rais wao.
Wamekiri kuwa hata wao maslahi yao ni madogo sana.
Lakini zaidi ya hapo ni kwamba, Jeshi lilisema kuwa litawafungulia mashitaka na kuwa-excute wote waliohusika na vurugu za mauaji
hivyo basi wanajua kuwa Jeshi linakwenda kuwakaanga, kwa nini wasianze kujihami? Ooh sisi ni watoto wa nyoka tu wala sio nyoka..aghhhhhhhh
 
Kwa sheria za Tanzania polisi au mwanajeshi yeyote akigoma anafunguliwa mashtaka ya uhaini na sidhani kama wana ubavu hawa wa kwetu kwa jinsi walivyovibaraka kwa ccm.na pia wao hawana maisha duni maana wameshajilimbikizia mali kwa njia ya rushwa wana majumba kibao na na daladala kila kona ya mji waliochoka ni wazembe wenyewe
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom