Ajabu: Balozi Seif Iddi apigiwa Saluti na Heshima zote na majeshi, Seif Shariff wampa Mkono

Watu wanapoambiwa Tanzania ni nchi ya mwisho kwa mambo mengi sana tukubali matokeo, ikiwa hadi ndani ya Karne hii ya 21 bado ndani ya nchi hii muna wanadamu wana mawazo pumbu kama haya!!!! Halafu watu kama hawa ndio eti baada ya miaka fulani wanakuwa Watunga sheria, Mawaziri, Majaji na Wadudu wengine! Daima nitakataa kuitwa Mtanzania. Am proud to be Zanzibari.
Imenishangaza sana Maalim kutopigiwa salute while hata makamu wa pili amepigiwa! Tunaweza kuchukulia ni jambo dogo lakini lina mantiki kubwa sana na ukweli halisi anaujua Maalim mwenyewe!!
 
Ahhaha Makamo wa Kwanza wa Rais wa Serikali Mapinduzi ya Zbar amabe sio mtendaji...ni Ceremonial tu!!!kazi ipo!!!ina maana kama Shein na Makamo 2 hawapo nchi haiwezi bakia kwake??twaomba ufafanuzi hapo!!
Maalim alipewa nafasi kuzibwa baada ya yeye mwenyewe kuonyesha kulainika, lakini anajulikana ni adui wa Taifa, na akipata japo sekunde moja basi history yote ya bara la afrika itabadilika.
 
Nilikuwa nikiangalia TV sherehe za Mapinduzi.
Wakati wa Kutoka uwanjani, kabla ya kupanda gari kuna makamanda wa jeshi na Polisi, Shein,JK,Bilali walipigiwa Saluti ya heshima.
mara baada ya kuondoka hao, ilkuwa zamu ya Maalim seif, kwa bahati majeshi na polisi waliokuwepo hapo walimpa tu mkono tena baada ya maalim kutoa mkono na hakuna alienyanyua mkono kama Saluti, Makamo wa Pili wa Rais wa ZANZIBAR naye alipigiwa saluti ya nguvu.
jee imekaaje ktk Siasa zetu. jee maalim seif hatakiwi na Vyombo vyetu vya usalama?

Mkubwa! Hata mie nimeinukuu hiyo maneno! Basi tuwaombe wataalamu wa itifaki watujuze.
 
Imenishangaza sana Maalim kutopigiwa salute while hata makamu wa pili amepigiwa! Tunaweza kuchukulia ni jambo dogo lakini lina mantiki kubwa sana na ukweli halisi anaujua Maalim mwenyewe!!

Mkuu wala usishangae! Ni salamu tosha za magamba kwenda kwa CUF na wale wajinga wajinga wao pale mjengoni Dodoma ambao nao wanajihisi kuwa sehemu ya utawala. Magamba hayana rafiki kaka hasa "kitumbua" chao kinapoguswa ndio kabisaa. Nashangaa Maalim na CUF yake hawajui hili. Ni heri kufanya urafiki na shetani kuliko magamba.
 
Maalim aliingia unyonge, alikuwa hana jinsi. lkn ndio ukubwa mzee

Kuna wakati unakuwa mtu wa kuchangia ukweli..Kumbe uliona ee?? Wakati wa kuondoka Maalim viongozi wala hawakusimama...ila walipoondoka wengine duuuuu...Maalim angejua angeacha akajenge Chama kijulikane .....Subuhanah wata-alah
 
Imenishangaza sana Maalim kutopigiwa salute while hata makamu wa pili amepigiwa! Tunaweza kuchukulia ni jambo dogo lakini lina mantiki kubwa sana na ukweli halisi anaujua Maalim mwenyewe!!

Naona munapiga makelele bora niwasaidie jibu. Jibu halisi ni kwamba; Hayatambui Mapinduzi ya 1964 kwa msimamo sawa na wanavyoyatambua viongozi wa CCM. Kwa maelezo zaidi kitafte kitabu cha Dr. Harith Ghassany "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru"! Leo nakusaidia ila siku ya nyengine usilete mada kama hizi.
 
mwalim anajua fika urais atausikia redioni tu, tumemuweka pale kupunguza kelele tu za wafadhili, angalikuwa kam dk slaa hata rwanda hajulikani, tungalimuacha asage rumba

Hii kadhia haipo tu kwa maalim, hata huku bara majukumu ya Dr. Bilal ni kama vile hayaeleweki, mpaka leo nimepitia comments ya mwana Jf mmoja akisema likifumka dill la soko la mikasi nje ya nchi itabidi serikali imuhifadhie Dr. Bilal container mbili za mikasi kwa ajili ya kukatia utepe katika funguzii nyingi azifanyazo kwa maana ndiyo kazi yake kubwa.
 
Maalim alipewa nafasi kuzibwa baada ya yeye mwenyewe kuonyesha kulainika, lakini anajulikana ni adui wa Taifa, na akipata japo sekunde moja basi history yote ya bara la afrika itabadilika.

Good point! Ndio maana magamba wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kumpa vyeo ambavyo havina heshima yoyote wakisubiri muda wake "uishe" watawale vizuri. Magamba wanachofanya ni pamoja na vita ya kisaikolojia kum-harass Seifu na wafuasi wao kadiri inavyowezekana hatimaye CUF ife kabisa, then eventually the only option ya vyama vya siasa Zanzibar itabaki CCM ambayo itatawala MILELE.
 
Maalim aliingia unyonge, alikuwa hana jinsi. lkn ndio ukubwa mzee

Mzanzıbarı mmoja leo alınıambıa kwamba kwa Katıba ya Zanzıbar ya sasa hıvı ıkıtokea Sheın akafa Nchı anakabıdhıwa Makamu wa Pılı wa Raıs na sıyo Maalım Seıf. Kwahıyo utaona hapo nguvu ya Maalım Seıf ılıvyo ndogo. Nı cheo cha kuzıbwa mdomo tu.
 
Yakhe, ndugu zangu wa hapa JF na CHADEMA kwa ujumla nyinyi sio wa mwanzo kujenga chuki dhidi ya Maalim Seif na pia Wazanzibari, wamepita wengi tu zaidi yenu ila wameshindwa!! Mfupa uliomshinda fisi kuula nyinyi munajaribu kutaka kuumeza mzima mzima! Hatari hiyo musije kujaribu. Am proud to be Zanzibari, Zanzibar Daimaaaaaa Mbele.
 
mwalim anajua fika urais atausikia redioni tu, tumemuweka pale kupunguza kelele tu za wafadhili, angalikuwa kam dk slaa hata rwanda hajulikani, tungalimuacha asage rumba
Haya ndio matatizo ya kukimbia shule na kuishia Madrasa! Suruali fupi fupi akili fupi fupi! endelea kumtajataja Dr Slaa roho yako isuuzike binti!
 
CUF wamejiua wenyewe hilo halina ubishi. Kilichobaki ni kwamba wanachama wote wa CUF wapewe kadi za CCM na ofisi zote za CUF zipandishwe bendera za CCM. R.I.P CUF
 
Naona munapiga makelele bora niwasaidie jibu. Jibu halisi ni kwamba; Hayatambui Mapinduzi ya 1964 kwa msimamo sawa na wanavyoyatambua viongozi wa CCM. Kwa maelezo zaidi kitafte kitabu cha Dr. Harith Ghassany "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru"! Leo nakusaidia ila siku ya nyengine usilete mada kama hizi.
Lakini mkuu Majeshi yanatoa heshima kwa kiongozi na si mtizamo wake! Ni makamu wa Rais yule kiongozi wa pili ki mamlaka Zanzibar!
 
Yakhe, ndugu zangu wa hapa JF na CHADEMA kwa ujumla nyinyi sio wa mwanzo kujenga chuki dhidi ya Maalim Seif na pia Wazanzibari, wamepita wengi tu zaidi yenu ila wameshindwa!! Mfupa uliomshinda fisi kuula nyinyi munajaribu kutaka kuumeza mzima mzima! Hatari hiyo musije kujaribu. Am proud to be Zanzibari, Zanzibar Daimaaaaaa Mbele.

Proud to be brain washed? Did you see how your idolised VP Seif was humiliated? Hahahahaha
 
Maalim alishajiuza na kutengeneza serikali ya umoja wa taifa feki na bado kuna yatakayokuja kumtokea puani kwa ufeki huu wa serikali yao
 
Naona munapiga makelele bora niwasaidie jibu. Jibu halisi ni kwamba; Hayatambui Mapinduzi ya 1964 kwa msimamo sawa na wanavyoyatambua viongozi wa CCM. Kwa maelezo zaidi kitafte kitabu cha Dr. Harith Ghassany "Kwaheri Ukoloni, Kwaheri Uhuru"! Leo nakusaidia ila siku ya nyengine usilete mada kama hizi.

Asingeenda uwanjani kama anapinga hayo mapinduzi. ni kenge pekee hukimbia mvua kutumbukia mtoni. ila tuache matani sef amependeza ki-kameroon kameroon baada ya kunyoa ile midevu!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom