Ajabu: Balozi Seif Iddi apigiwa Saluti na Heshima zote na majeshi, Seif Shariff wampa Mkono

thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
1,566
Nilikuwa nikiangalia TV sherehe za Mapinduzi.
Wakati wa Kutoka uwanjani, kabla ya kupanda gari kuna makamanda wa jeshi na Polisi, Shein,JK,Bilali walipigiwa Saluti ya heshima.
mara baada ya kuondoka hao, ilkuwa zamu ya Maalim seif, kwa bahati majeshi na polisi waliokuwepo hapo walimpa tu mkono tena baada ya maalim kutoa mkono na hakuna alienyanyua mkono kama Saluti, Makamo wa Pili wa Rais wa ZANZIBAR naye alipigiwa saluti ya nguvu.
jee imekaaje ktk Siasa zetu. jee maalim seif hatakiwi na Vyombo vyetu vya usalama?
 
Ahhaha Makamo wa Kwanza wa Rais wa Serikali Mapinduzi ya Zbar amabe sio mtendaji...ni Ceremonial tu!!!kazi ipo!!!ina maana kama Shein na Makamo 2 hawapo nchi haiwezi bakia kwake??twaomba ufafanuzi hapo!!
 
Ha ha ha ha ha ha ha ahaaaaaaaaaaaa! Sorry! kiingledha sio lugha ya mama yangu lakini mkuu hapo kwenye
red nilitegemea leo ndio ingekuwa hasa siku ya Maalim; ha ha ha haaaaa ceremonial VP!
 
Muunguja hawezi akamuheshimu Mpemba hata siku moja. Vile vile Wapemba hawawapendi Waunguja. Ndiyo maana wengine tunasema kuwa hii nchi ya Zanzibar haiwezi ikatawalika ikiwa ni nchi Zanzibar. Ni lazima liwepo taifa lingine kubwa la kuwachunga hawa wasiuane.

Zamani taifa hilo kubwa lilikuwa Wakoloni UK, leo hii ni Muungao URT. Seif, Jussa na wote waliosahau ukweli wa siasa na Hizbu wachunge sana wanachojaribu kufanya. Litawageukia na itakuwa ni too late, labda Tanzania bara itawaokoa tena.
 
oyaaa kamanda acha majungu hayoo sasa saluti unaona big deal kama huna mada usiweke pumba tunataka mada za faida katika jamii sio uzushi
 
kwali hata mimi nimeona, wale jamaa baada ya kutoka maalim Seif majeshi waliokuwa wanatoa saluti kwa viongozi, kufika maalim waliuchuna na wakajifanya kama seif sio kiongozi. lkn balozi Alipigiwa masaluti mpaka basi tu.

Salamu tosha kwa CUF waliosaliti upinzani wakajihisi nao ni sehemu ya utawala. Chekeni na magamba mtaipata habari yake.
 
Muunguja hawezi akamuheshimu Mpemba hata siku moja. Vile vile Wapemba hawawapendi Waunguja. Ndiyo maana wengine tunasema kuwa hii nchi ya Zanzibar haiwezi ikatawalika ikiwa ni nchi Zanzibar. Ni lazima liwepo taifa lingine kubwa la kuwachunga hawa wasiuane.

Zamani taifa hilo kubwa lilikuwa Wakoloni UK, leo hii ni Muungao URT. Seif, Jussa na wote waliosahau ukweli wa siasa na Hizbu wachunge sana wanachojaribu kufanya. Litawageukia na itakuwa ni too late, labda Tanzania bara itawaokoa tena.

Lakini mkuu hapo kwenye red umesahau kwamba Shein ni Mpemba. Sijui inakuwaje hapo?
 
kwali hata mimi nimeona, wale jamaa baada ya kutoka maalim Seif majeshi waliokuwa wanatoa saluti kwa viongozi, kufika maalim waliuchuna na wakajifanya kama seif sio kiongozi. lkn balozi Alipigiwa masaluti mpaka basi tu.

Eti kweli ulipata ajali mpaka watu wakakuombea upumzike kwa amani?
 
oyaaa kamanda acha majungu hayoo sasa saluti unaona big deal kama huna mada usiweke pumba tunataka mada za faida katika jamii sio uzushi

Mkuu katika medani ya utawala hiyo kitu achana nayo kabisa. Kama vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi havina nidhamu na heshima kwako tena hadharani utawala wako ni feki. Heshima namba moja ya mtawala ni kuheshimiwa na vyombo vya kimabavu mengine yanafuatia.
 
Nilidhani umeweka na picha kwa faida zaidi ya ambao hatujafuatilia kwa runinga,so far so good its a message kwamba hauna kitu pale, kiitifaki alitakiwa kupigi wasalute. wapi Mtatiro?
 
Basi kama kuna kitu kimemshusha hadhi Maalim S.S.Hamadi basi ni sherehe za mwaka huu za kumbukumbu ya uhuru wa Tanzania Zanzibar, maana, hii imedhihirisha kuwa Mh. Hamadi Rashid Mbunge wa Wawi alikuwa na pointi kusema S.S.Hamadi anaidhoofisha CUF. Mheshimiwa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Tanzania Zanzibar Dkt. Shein amesema serikali iliyoko madarakani inatekeleza ilani ya CCM ya 2010, kwa hiyo Maalim S.S.Hamadi naye pia anatekeleza ilani ya CCM huku akidhoofisha CUF ama bila kujua au kwa kujua. Ingekuwa ahueni kwa S.S.Hamadi kama neno Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Tanzania Zanzibar lingetajwa mara nyingi kwenye hotuba ya Mheshimiwa Rais wa Serikali ya mapinduzi ya Tanzania Zanzibar Dkt. Shein, hiyo ingedhihirisha kuwa CUF inatoa mchango katika kufanikisha maendeleo ya Watanzania waishio Zanzibar, lakini leo haikuwa hivyo.

Kwa hili Maalim S.S. Hamad inabidi amuombe msamaha Mh. H. Rashid na wana CUF wote kwa kuwasaliti.
 
bora dk slaaa anavyokimbia jamii. seif angalikuwa vijana wake wa CUF, angalibebwa kama anavyobebwa dk slaa kwenye mikutano ya CDM
Suala sio kubebwa hapa tunachojadili ni saluti kwa mzee Seif kama huna cha kuchangia sogea msikitini ukanywe gahawa
 
Muunguja hawezi akamuheshimu Mpemba hata siku moja. Vile vile Wapemba hawawapendi Waunguja. Ndiyo maana wengine tunasema kuwa hii nchi ya Zanzibar haiwezi ikatawalika ikiwa ni nchi Zanzibar. Ni lazima liwepo taifa lingine kubwa la kuwachunga hawa wasiuane.

Zamani taifa hilo kubwa lilikuwa Wakoloni UK, leo hii ni Muungao URT. Seif, Jussa na wote waliosahau ukweli wa siasa na Hizbu wachunge sana wanachojaribu kufanya. Litawageukia na itakuwa ni too late, labda Tanzania bara itawaokoa tena.

Watu wanapoambiwa Tanzania ni nchi ya mwisho kwa mambo mengi sana tukubali matokeo, ikiwa hadi ndani ya Karne hii ya 21 bado ndani ya nchi hii muna wanadamu wana mawazo pumbu kama haya!!!! Halafu watu kama hawa ndio eti baada ya miaka fulani wanakuwa Watunga sheria, Mawaziri, Majaji na Wadudu wengine! Daima nitakataa kuitwa Mtanzania. Am proud to be Zanzibari.
 
Muunguja hawezi akamuheshimu Mpemba hata siku moja. Vile vile Wapemba hawawapendi Waunguja. Ndiyo maana wengine tunasema kuwa hii nchi ya Zanzibar haiwezi ikatawalika ikiwa ni nchi Zanzibar. Ni lazima liwepo taifa lingine kubwa la kuwachunga hawa wasiuane.

Zamani taifa hilo kubwa lilikuwa Wakoloni UK, leo hii ni Muungao URT. Seif, Jussa na wote waliosahau ukweli wa siasa na Hizbu wachunge sana wanachojaribu kufanya. Litawageukia na itakuwa ni too late, labda Tanzania bara itawaokoa tena.

Watu wanapoambiwa Tanzania ni nchi ya mwisho kwa mambo mengi sana tukubali matokeo, ikiwa hadi ndani ya Karne hii ya 21 bado ndani ya nchi hii muna wanadamu wana mawazo PUMBA kama haya!!!! Halafu watu kama hawa ndio eti baada ya miaka fulani wanakuwa Watunga sheria, Mawaziri, Majaji na Wadudu wengine! Daima nitakataa kuitwa Mtanzania. Am proud to be Zanzibari.
 
Back
Top Bottom