Aisha Babu:- Mwanamke m'babe, aliyewashinda POLISI wa Tanzania.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,870
155,831
Mwanamke Aisha Babu amekuwa akiwa akiwaumiza vichwa viongozi waandamizi wa jeshi la polisi nchini.

Polisi wetu wameshindwa kumdhibiti mwanamke huyo, hivyo basi wameamua kupiga marufuku mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani.

Taarifa za kiintelijensia zinadai mwanamke huyo anawaogopa wanachama wa CCM, ndio maana hashambulii mikutano inayoandaliwa na viongozi wa juu wa CCM na mikusanyiko inayofanyika Uwanja wa Taifa.

Wito wangu kwa jeshi letu la polisi ni kwamba, Kariakoo kuna watu wengi sana, na kwa usalama wa raia na mali zao, wakatazwe kwenda huko kwani Aisha Babu anaweza kuwadhuru na kusababisha janga la KITAIFA.
 
ha ha ha, wala hashambulii uwanja wa taifa kukiwa na mpira wala makanisani
 
ni nani huyu Aisha Babu? ndo mara ya kwanza kumskia leo

Wale jamaa waliomfanya Kova na Mwema kupelekwa kusomea Intelejensia ya Maandamano yanayoingiliwa na Al Shabab, Intelejensia yao inatabiri maandamano. Ni wanafunzi wa Shekhe Yahya
 
Narudia kusema kuwa Tanzania hamna polisi, ila kuna yunifomu za polisi

Acha tu bana, jana nimepita maeneo ya barabara ya nyerere Gongo la mboto kuelekea Pugu , yaani nimekutana na askari polisi mmoja trafic nia aibu, yaani jamaa ana kitambi kama nyumba , kavaa reflector yaani kama mama mja mzito mwenye mimba nne za triplets!!
 
sijui polisi kama huyo anafukuzaje mwizi.?
 
Huyu asha babu hajaona lile kusanyiko kubwa la epic nation pale arusha anatarget mikusanyiko ya cdm tu! Hatari kweli.
 
Mwanamke Aisha Babu amekuwa akiwa akiwaumiza vichwa viongozi waandamizi wa jeshi la polisi nchini.

Polisi wetu wameshindwa kumdhibiti mwanamke huyo, hivyo basi wameamua kupiga marufuku mikutano na maandamano ya vyama vya upinzani.

Taarifa za kiintelijensia zinadai mwanamke huyo anawaogopa wanachama wa CCM, ndio maana hashambulii mikutano inayoandaliwa na viongozi wa juu wa CCM na mikusanyiko inayofanyika Uwanja wa Taifa.

Wito wangu kwa jeshi letu la polisi ni kwamba, Kariakoo kuna watu wengi sana, na kwa usalama wa raia na mali zao, wakatazwe kwenda huko kwani Aisha Babu anaweza kuwadhuru na kusababisha janga la KITAIFA.

bujbuj we ni soo
 
Nina wasiwasi kuna mahusiano ya siri kati ya sisiemu na huyo dada
 
Tanzania kuendelea kwa kila kitu mpaka ipite miaka elfu kumi. Ova.
 
Back
Top Bottom