Airtel wamepandisha bei ya Vifurushi

nunua modem ya zantel iko fast na cheap 1gb sh 15000

Mkuu nyumbani kwangu tunatumia Zantel wanakula hela kama hawana akili nzuri huku hamna cha maana ulichofanya. Hasa pale unapo-upload files ni balaa tupu, unajikuta pesa inaisha na file halijawa-uploaded mpaka nilishaanza kufikiria kuchukua hiyo ya Airtel kumbe nako mambo si shwari, lol!
 
Acha kulala nunua 400 mb kwa 2500/= tu nenda uwanja wa sms andika intaneti tuma kwenda 15444 mambo yankuwa byeee unasurf the world bila shida
Mwanzo. Ilikuwa nazitumia sana, last two weeks imekuwa balaa, nikinunua leo matumizi yaleyale siku tatu kwisha habari yake
 
Njinji bado mnanunua bandos hapa sauth afrika nchi nzima kuna wareless
Yani ni net siku nzima labda umeme ukatike
poleni sana
 
hivi nahilo tangazo la airtel hapo juu nilakwelig'
yaani ukinunua moderm 30000 unapata free intnt kwa muda wa miezi 6?
Nilitaka nijue ili niwahi nikanunue kabla promotion haijaisha nijuzeni wajameni
Wizi mtupu. Sijui TCRA wako wapi.
 
Hii kitu nilikuwa naitumia kwa wiki nzima lakini jana nimeweka imeisha leo na hapa niweka nyingine muda mchache uliopita isipomaliza siku tatu nahamia Zantel nimeskia wameshusha. Ujanja ni kuwa na Modem za kila mtandao ili hawa jamaa wasikubabaishe.
Sahihi kabisa, nilikuwa natumia kwa zaidi ya wiki mbili zamani, juzi kati ikawa siku tatu nyingi, kwisha, nimehamia zantel
 
kifurushi cha 400mb ni kwaajili ya simu. wamekifanyia marekebisho na kimekuwa sloooow sana kama utatumia computer.
vodacom wao do useless kabisa kwao ukinunua kifurushi halafu ukakimaliza kabla ya mda kuisha huwezi nunua tena. utakumbana na sms ya aina hii
Tayari umeshajiunga na vodacom Internet.
Tafadhali unaweza kununua baada ya muda wa kujiunga kuisha.

sasa sms za namna hii ndizo zinazotufanya turudi tena airtel (400mb slow connection)

Nafkri inakuwa slow huko mjini maana watumiaji ni wengi. Huku mashambani ijo faster balaaa
 
Back
Top Bottom