Airtel sasa ni Tigo (Wezi)????

DASA

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,031
301
Pamoja na kupandisha gharama za Internet ambazo ni kubwa sana kuliko uwezo wa mwananchi wa kawaida kwa vigezo ambavyo haviko wazi. Jana masikini mie nimejikamua jana nikaweka kifurushi cha 1GB nilichokifanya ni kujibu emails kama 6 hivi pamoja na kuchat na mwenza wangu ambaye yupo nje ya nchi kwa takriban masaa mawili tu, leo asubuhi nacheki imebaki 271MB tu. Jamani huu kama sio wizi nini!!! Chondechonde Airtel hizi hela tunapata kwa shida sana, Wizi wa namna hii kwakweli mnastahili kuchomwa moto!!.

Hivi hilo tangazo hapo juu hakuna uwezekano wa kulitoa, maana limeshaanza kunitia kichefuchefu.
 
hii mijitu ni mijizi mkuu kama unakumbuku nzuri ya matumizi yako unaweza ukawafunga hawa wanatuibia sana yaani wameona siku hizi tunatumia internet kuwasiliana wameamua kutukamua
 
Nafikiri airtel, kwa upande wa modem zenu hizi mpya za 3.75 hampo sawa, mara inafanyakazi mara haifanyi, nini tatizo?, ukiachilia mbali hilo tatizo la gharama kutoendana na matumizi
 
Pamoja na kupandisha gharama za Internet ambazo ni kubwa sana kuliko uwezo wa mwananchi wa kawaida kwa vigezo ambavyo haviko wazi. Jana masikini mie nimejikamua jana nikaweka kifurushi cha 1GB nilichokifanya ni kujibu emails kama 6 hivi pamoja na kuchat na mwenza wangu ambaye yupo nje ya nchi kwa takriban masaa mawili tu, leo asubuhi nacheki imebaki 271MB tu. Jamani huu kama sio wizi nini!!! Chondechonde Airtel hizi hela tunapata kwa shida sana, Wizi wa namna hii kwakweli mnastahili kuchomwa moto!!.

Hivi hilo tangazo hapo juu hakuna uwezekano wa kulitoa, maana limeshaanza kunitia kichefuchefu.
Tatizo si hawa vibaka ila ni hii serikali ya mafisadi, wezi na majambazi wanaolisaliti taifa na kuwafukarisha wananchi. hapa ni hadithi ya nguruwe kukabidhiwa ulinzi wa shamba la mihogo kwani baada ya kitambo kifupi tu utakuta shamba lote limetafunwa!
Haiingii akilini kuona serikali ikishindwa kuwadhibiti wezi hawa ambao hawalipi kodi, wanatoza bei za ajabu ajabu, hawabanwi na wanawaongezea wananchi umasikini wa kutupwa. Ni serikali ya CCM pekee iliyoweka rekodi ya "kushindwa" kusimamia sheria ya kuwabana wahalifu waliokuwa waki "chakachua" Petroli na dizeli kwa kuichanganya na mafuta ya taa yaliyokuwa mkombozi wa mlala hoi kwa kuuzwa bei nafuu hadi kuipandisha bei kuwa sawa na petroli na dizeli hivi kuwazidishia maumivu raia wa kawaida!
Wakati huko Kenya Safaricom wenye wateja wachache kulinganisha na matapeli hawa (Vodacom, Airtel, Tigo n.k.) wanaongoz katika kuchangia pato la taifa kwa kodi hapa makampuni hayo hayako hata katika orodha ya walipa kodi ishirini bora! Eti wanazidiwa hata na makampuni ya ulinzi!
Hawana hofu hawa, hawamwogopi Mungu wala shetani, sembuse serikali ya vibaka wenzao? Watanzania wana chaguo moja tu; chaguo gumu lakini la uhakika; nalo ni kuiondoa kabisa serikali ya CCM hadi kwenye mizizi katika uchaguzi wa 2015 na kuweka chama mbadala kitakachokuwa na hofu ya kukutwa na yatakayokuwa yamewapata wezi, vibaka na mafisadi hawa. Hilo litakapotendeka, Tanzania itakoma kuwa shamba la mwendawazimu na wananchi watakuwa wamepata uhuru mpya.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom