Airtel na Huduma zao Mbovu

mchillo

JF-Expert Member
Oct 13, 2010
500
224
Mimi ni mteja wa Kampuni hiyo ya simu toka iingie nchini kama Celtel, Zain na sasa Airtel lakini hakuna wakati niliokwazwa nao kama safari hii wanapojiita Airtel.
Nilianza kukwazwa na tangazo lao lililonihamasisha "kujirusha" kwa Tsh. 250/= ili nipate muda wa hewani wa Dk 15 au Tsh. 500/= kwa muda wa Dk 30. Mara kadhaa nilipojaribu kujiunga niliishia kukatwa fedha bila ya kupata huduma husika, yaani licha ya kukatwa fedha na kutumiwa msg ya kuthibitisha kujiunga na huduma ya "Piga Simu bure Airtel kwenda Airtel" waliendelea kunikata fedha zilizoko katika salio la simu yangu hadi zilipokwisha waliponijibu kwa ujumbe wa "Salio lako halitoshi kupiga simu unayotaka... tafadhali ongeza salio...". Nimejaribu kujiunga mara kadhaa na kuishia hivyo hivyo!
Kama kwamba hiyo haitoshi tatizo kubwa zaidi huja pale unapotaka kuwasiliana na wahudumu kuwaarifu yaliyokusibu simu itakuchukua kati ya nusu saa hadi saa nzima kumpata opereta wa kukujibu kama una bahati.
Hali hii ya kuchelewa kujibu simu imewakatisha tamaa maajenti na wanakataa au kutoza bei kubwa zaidi kwa wanaotaka kurejesha namba zao za zain zilizopotea au kuandikisha laini za simu.
Kuna mwana JF yeyote aliyekwazika kama mimi? Kilio chetu tukipeleke wapi?
 
Ndugu nashukuru kuliona hilo. nataka nihame. unaweka salio baadae ukitaka kupiga unakuta salio lako from nowere halipo
 
Competent figures in customer caring nchini mwetu ni poor kabisa.
 
Bora uhamie kampuni nyingine yenye huduma bora. Haukubinafsishwa kwenye Airtel kutoka Zain au Celtel!
 
Pole sana kwa tatizo hilo, ila kuna tatizo lingine nalo tunapaswa tulitolee macho, ambalo ni sugu na sina hakika kama kuna aliyeanza kulishtukia hii ni kwa mitandao mingi kutegemea na msukumo wa utashi wa utafiti wa mtu husika. Tatizo la kipimo cha muda wa maongezi inaposemwa secunde au dakika moja huwa ni sawa na kipimo kile kile cha saa tulizo zoea au wana dakika moja nyingine iendayo kasi sana kuliko? Njia za kuthibitisha hili zipo nyingi hebu kila mwenye wasaa ajaribu iliyo nyepesi kwake kisha aanike majibu yake yatusaidie kiutafiti zaidi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom