airtel internet 200mb bonus

mohamedn

Member
Feb 19, 2009
54
35
Kuna kitu kinatendeka kuhusu hii airtel internet.
Wao wamekuja na offer wanakupa 200mb free ukiongeza credit kabla ya saa 6 usiku, sasa cha kushangaza nimekuja kugundua kwamba ukiweka credit na ikifika saa 6 usiku na ukaanza kusurf basi kama ulikuwa na mb zako zilizokuwa kwenye (malipo ya bundles hasa ya 400mb) zinakatwa na badala yake wana weka hii offer ya 200mb ambayo pia ikifika saa 12 asubuhi balance ya mb inakatwa.
Hii mimi imenitokea mara mbili baada ya kutumia aidha kwa modem yao au hata kwa kutumia mobile phone kama modem, sijui kama kuna mwenzangu yeyote aliepata tatizo hili.
Labda cha kufanya hakikisha una balance ya mb zako za bundle kiasi gani kabla hujaanza kusurf kuanzia 6 usiku na ukimaliza pia ucheki kama zimebaki vilevile?
 
jamani wana-jf naomba nikanushe hapo awali nilisema hakuna bonus leo nimedamkia saa 6.00 na kukuta kweli bonus zangu zipo na nimesurf bila tatizo ila mtandao ni mzito sana kwani watumiaji wa usiku wamefikia hadi 4554 naamini baadhi ni wale wa bonus
sasa sihami tena airtel
 
mi huwa naeka mia 5 napewa,ucku naweka alarm,nadownload torrent zngu kwenye cm asubuh nkiamka nakuta kla ki2 tayari!! Haijawah tokea nkaweka vocha nikakosa bonus.
 
ingekuwa poa kuwa kiasi cha vocha unachoweka kinakuwa proportional na MB unazowekewa, ukiongeza vocha ya 500 unapata 200MB, ukiweka vocha ya buku unapata 400MB.....
 
Mimi naona wangetoa hiyo ofa mchana na wala siyo ucku.
 
hivi hiyo kujua sijui nini *6# hakuna jipya hapo... AIRTEL WEZI TUU...Ngoja nijivinjari na toka zamani yangu
 
ingekuwa poa kuwa kiasi cha vocha unachoweka kinakuwa proportional na MB unazowekewa, ukiongeza vocha ya 500 unapata 200MB, ukiweka vocha ya buku unapata 400MB.....

weka vocha za jelojelo kuzidabo hizo mb...pia muda wa bure huwezi kutumia kama una salio la sh 4,
 
jamani wana-jf naomba nikanushe hapo awali nilisema hakuna bonus leo nimedamkia saa 6.00 na kukuta kweli bonus zangu zipo na nimesurf bila tatizo ila mtandao ni mzito sana kwani watumiaji wa usiku wamefikia hadi 4554 naamini baadhi ni wale wa bonus
sasa sihami tena airtel

tungekucheka kama ungerudi kwenye vibajaji...
 
Kuna kitu kinatendeka kuhusu hii airtel internet.
Wao wamekuja na offer wanakupa 200mb free ukiongeza credit kabla ya saa 6 usiku, sasa cha kushangaza nimekuja kugundua kwamba ukiweka credit na ikifika saa 6 usiku na ukaanza kusurf basi kama ulikuwa na mb zako zilizokuwa kwenye (malipo ya bundles hasa ya 400mb) zinakatwa na badala yake wana weka hii offer ya 200mb ambayo pia ikifika saa 12 asubuhi balance ya mb inakatwa.
Hii mimi imenitokea mara mbili baada ya kutumia aidha kwa modem yao au hata kwa kutumia mobile phone kama modem, sijui kama kuna mwenzangu yeyote aliepata tatizo hili.
Labda cha kufanya hakikisha una balance ya mb zako za bundle kiasi gani kabla hujaanza kusurf kuanzia 6 usiku na ukimaliza pia ucheki kama zimebaki vilevile?[/QUOTE

Ndg yangu hilo limenitokea mimi pia zaidi ya mara tatu na hii yangu ni kali zaidi kwa kuwa ukiachilia mbali hiyo ya bonus ya mb 400 hela yangu iliyokuwamo kwe simu ikaliwa, huwa najiunga na bundle ya wiki ya shs 15000 na hela ya ziada inayokuwemo huw inaliwa pia, wizi ulioje airtel? nimejaribu kuongea na customer care kuhusu hili naishia kupewa namba ya kumbukumbu ya tatizo langu na kuambiwa tatizo linatafutiwa ufumbuzi nitapigiwa simu ("mpendwa mteja, tunashughulikia ombi lako, kumbukumbu no. yako ni 516477 tutawasiliana nawe hivi punde") haya ndo majibu yao hii ilikuwa ni tar 20/04/2011 nyingine ni kumb na 530247 ya tar 25/04/2011, hizi ni baadhi tu ninazo ahadi nyingi nilizoahidiwa kutatuliwa tatizo langu lakini bado nikijiunga na bundle hela yangu ya ziada iliyokuwamo inaliwa. Watanzania wenzetu mlioko kwenye airtel mtusaidie ndg zenu tunadhulumiwa, eneo nililopo napata airtel pekee unless ningekwisha hama zamani. Wewe unayejiita CCRAIRTEL humu JF una msaada gani ktk hili au ni kuweka matangazo tu humu jf ya ku-support dhulumati kwa watanzania wenzio? naomba unisaidie niweze kurudishiwa hela zangu zilizokatwa ilihali zimeshakatwa elfu 15 za bundle ya wiki.
 
Ndg yangu hilo limenitokea mimi pia zaidi ya mara tatu na hii yangu ni kali zaidi kwa kuwa ukiachilia mbali hiyo ya bonus ya mb 400 hela yangu iliyokuwamo kwe simu ikaliwa, huwa najiunga na bundle ya wiki ya shs 15000 na hela ya ziada inayokuwemo huw inaliwa pia, wizi ulioje airtel? Au ni utapeli? nimejaribu kuongea na customer care kuhusu hili naishia kupewa namba ya kumbukumbu ya tatizo langu na kuambiwa tatizo linatafutiwa ufumbuzi nitapigiwa simu ("mpendwa mteja, tunashughulikia ombi lako, kumbukumbu no. yako ni 516477 tutawasiliana nawe hivi punde") haya ndo majibu yao hii ilikuwa ni tar 20/04/2011 nyingine ni kumb na 530247 ya tar 25/04/2011, hizi ni baadhi tu ninazo ahadi nyingi nilizoahidiwa kutatuliwa tatizo langu lakini bado nikijiunga na bundle hela yangu ya ziada iliyokuwamo inaliwa.Siku moja nimepigiwa simu na mama mmoja kutoka airtel anadai anataka kushughuikia tatizo langu alipopata ukweli kutoka kwangu akaniahidi utatuzi atanipigia cm amepotea jumla! Kudhihirisha kuwa ilikuwa ni kiini macho tu hakutaka kutaja jina lake. Watanzania wenzetu mlioko kwenye airtel mtusaidie ndg zenu tunadhulumiwa, eneo nililopo napata airtel pekee unless ningekwisha hama zamani. Wewe unayejiita CCRAIRTEL humu JF una msaada gani ktk hili au ni kuweka matangazo tu humu jf ya ku-support dhulumati kwa watanzania wenzio? naomba unisaidie niweze kurudishiwa hela zangu zilizokatwa ilihali zimeshakatwa elfu 15 za bundle ya wiki.
 
Back
Top Bottom