MDAU JR
JF-Expert Member
- Mar 9, 2011
- 451
- 82
Jamani Kuna dhuluma inafanyika airtel internate : ukijiunga na bundle au ukiwa na bonus na huku ukiwa na hela ya ziada kwe modem, ile hela inaliwa yote na kubakia sh 4 ambapo huwezi kupata connection ya net, unalazimika uweke hela nyingine nayo italiwa hadi ibakie sh 4 na net inakata tena ilhali una bundle ama bonus ya mb 200.Hili limenitokea zaidi ya mara tatu na hii yangu ni kali zaidi kwa kuwa ukiachilia mbali hiyo ya bonus ya mb 400 hela yangu iliyokuwamo kwe simu ikaliwa, huwa najiunga na bundle ya wiki ya shs 15000 na hela ya ziada inayokuwemo huw inaliwa pia, wizi ulioje airtel? nimejaribu kuongea na customer care kuhusu hili naishia kupewa namba ya kumbukumbu ya tatizo langu na kuambiwa tatizo linatafutiwa ufumbuzi nitapigiwa simu ("mpendwa mteja, tunashughulikia ombi lako, kumbukumbu no. yako ni 516477 tutawasiliana nawe hivi punde") haya ndo majibu yao hii ilikuwa ni tar 20/04/2011 nyingine ni kumb na 530247 ya tar 25/04/2011, hizi ni baadhi tu ninazo ahadi nyingi nilizoahidiwa kutatuliwa tatizo langu lakini bado nikijiunga na bundle hela yangu ya ziada iliyokuwamo inaliwa. Watanzania wenzetu mlioko kwenye airtel mtusaidie ndg zenu tunadhulumiwa, eneo nililopo napata airtel pekee unless ningekwisha hama zamani. Wewe unayejiita ccrairtel humu JF una msaada gani ktk hili au ni kuweka matangazo tu humu jf ya ku-support dhulumati kwa watanzania wenzio? naomba unisaidie niweze kurudishiwa hela zangu zilizokatwa ilihali zimeshakatwa elfu 15 za bundle ya wiki.