AIR TEL One Network au??

sekulu

JF-Expert Member
Jan 17, 2011
988
157
Hello JF,
Nilijua ni mimi tu naibiwa kwenye simu yangu ya mkononi, Kumbe tupo wengi sana,

Langu ni Hili;

Mimi ni msafiri wa hizi nchi za afrika mashariki na mara nyingi sana hupenda kutumia namba ya simu moja ili ku keep in touch na wadau wangu mbali mbali, Tangu ilipokua Celtel Mpaka Sasa Air Tel Au air Patel.

Enzi za Zain Simu yangu kutumika katika Hizi nchi Tatu (Kenya TZ na UG) oilikua rahisi sana na ONE NETWORK Ilileta maana sana kwani
  1. Simu ulikua unapokea bila kulipia hela yoyote yani kama nina line ya TZ nikend UG naweza pokea simu zangu bure na Sikatwi pesa yoyote.
  2. Kuweka pesa kwenye simu ilikua rahisi sana na ilikua inakuchukua step moja tu kuweka Airtime kwenye simu yako ukiwa ktk nchi ulotembelea 138*2345652657 then unapiga ok

Tangu Imebadilishwa jina yani Airtel kwanza naichukia Logo yake pili Hainamaana kuiita one netwok tena kwani mimi nitembeleapo nchi nyingine ambako Airtel inapatikana natakiwa nilipie Tsh 45 kwa dakik moja na Message imepanda kutoka 75 mpaka 86!, Ni gharama kubwa sana ila wameamua kufanya hivo.

Mbaya Zaidi na Uozo unapoweka pesa kwenye simu kwa mfano mimi nikiwa Kampala nikitumia vocha za pale, Vocha zinachelewa kuload na Hakuna ujumbe wowote unaokuja kama labda umekosea au kuna tatizo la system kama ilivokua kwa zain, Pili unaweza kuanza kuload pesa muda huu ikagoma mpaka saa 6 usiku.
Sas muda mwingine mtu unakua na dharura na unataka kuwasiliana na mtu unakuta wanaleta Drama Hizo

Mnafikiria nini Airtel??

Au Organization Change management mmedondokea pua??

Mnaboa

Wana JF naomba kuwasilisha yangu ya moyoni!

Airtel:A S 112:
 
Back
Top Bottom