lee Vladimir cleef
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 9,133
- 33,173
Mkuu Bukyanagandi huwa nafuatilia sana comment zako,wewe ni msema kweli kabisa,na wala sio mbabaishaji,huwa unaongea vitu vilivyoenda shule,mara nyingi nikisoma ulichoandika huwa naona kama Lecturer yuko mbele ya darasa anafundisha,hujawahi kusema uongo,amini nakwambia huku kuna wasomaji huwa tunafuatilia kila comment,hivyo huwa tunaweza kupembua pumba na mchele,wewe pamoja na wadau kadhaa hutupa mchele ulio safi kabisa.Kitu ambacho mimi huwa nakataa siku zote ni propaganda zia West.Sawa kabisa Congo hununua ndege used kwa ajili ya unafuu wa bei,halafu sidhani kama huwa zinafanyiwa maintanance za uhakika.We fikiria ndege watu wanapakia hadi mifugo kama mbuzi n.k,hizo zitakua ndege za maana kweli.Mkuu vijana wengi kwa kulishwa propaganda za West huwa wanasema Urusi ni nchi maskini na haina viwanda,sasa hiyo midege mikubwa duniani huwa inatengenezwa wapi? Hata juzi tu hapa kwenye Russia victory day 2016 wameonesha zana za kivita pamoja na dege kubwa zaidi duniani amabalo lipo Russia peke yake.Utakuta watu wanasema ooh Russ inategemea mali ghafi pekee gesi na mafuta,sasa hiyo midege imetoka ardhini kama gesi?Comment zako zinanikumbusha kauli za Balozi wa Uchina nchini Tanzania, aliwahi kusema amechoshwa na watu kulalamika ovyo eti Wachina wanawauzia bidhaa feiki, akasema matatizo ni wafanya biashara wa Tanzania wanao kwenda Uchina kununua substandard goods kimaksudi, hawataki kununua bidhaa zenye viwango vya Kimataifa wako interested na bidhaa feiki ili wa maximised faida - waswahili wanajali faida alafu wanawasingizia Wachina.
Sasa tuje kwenye comment za Wacongoman, wenyewe wanakwenda kununua ndege ambazo airworthness ni highly questionable i.e za zamani sana hazikufanyiwa maintainance ya kutosha, kwa kuwa zinauzwa kwa bei ndogo wafanya biashara wa Congo wanazibec hivyo hivyo bila ya kujali hatari ya kutumia vyombo vya anga vilivyo pitwa na wakati. Sasa kwenye mizingara kama hayo unawezaje kuiluhumu Urusi, ukichunguza kiundani ndege hizo zinanunuliwa kutoka kwenye nchi ambazo zilikuwa chini utawala wa USSR specifically Ukraine, Uzhubek nk hazinunuliwi kutoka Russia Federation.
Mkuu naikubali sana micango yako na ya wadau ambao tumekataa kulishwa sumu za west.Tuendelee kuwaelimisha.