VeroEretico
JF-Expert Member
- Jun 23, 2013
- 505
- 388
Well saidWanyantuzu walio wengi wana vipato vikubwa, ardhi yao ina samani kubwa. Wamezaliana sana hivyo kuifanya ardhi kuwa kitu cha muhimu sana,nyingi za kaya zao zina mifugo na chakula cha kutosha. Hakuna mnyantuzu utakaemfunga jela kwa faini ya milioni moja mahakamani,lazima atailipa tu, ndo viwango vidogo za faini ktk mifumo yao ya kijadi ktk utoaji wa maamuzi. Wana uchumi mkubwa lakini wanaishi kimasikini sana, tajiri anaemiliki ng'ombe elfu 10 wa kinyantuzu anavaa, kula, kulala, hovyo kuliko utegemeavyo. Vivyohivyo na kwa mwenye semi trailer hata 5. Nilimanisha hivyo, kikubwa ni imani za kishirikina na ukale zaidi. Huku bado wana sheria zote za kijadi, mahakama zao (degashida) polisi wao (wasumbantale) na magereza yao (faini au kutengwa) hakuna anayestafu viboko huku hata uwe wa miaka mia, mahakama ikisema fimbo ni fimbo na hata hawagomi. Kuna mengi ya kushangaza kama wewe hujawahi ishi kwenye mifumo ya kiafrika asilia.
Mkuu umejitahidi sana kufafanua mila na desturi za Ntunzu perhaps ni mtu wa huko au ni mtu wa kujifunza sana cultural sphere/anthropology za maeneo flani