Aina mpya ya wizi/wezi

KAKA A TAIFA

JF-Expert Member
Apr 27, 2011
566
80
Jamani kuweni macho na wezi hawa,akina dada/mama=wanawake kadhaa hapa jijini wamekwapuliwa handbags/pochi wanazoninginiza mabegani na wezi hawa.yaani wao wanatembea na bajaji ,pikipiki, tax,magari madogo ya abiria ,wanaendesha mwendo wa taratibu usawa wa mama /dada mtembea kwa miguu akiwa na pochi/handbag lake begani au mkononi.wakishamfikia tu wanalikwapua /wanakupua kwa nguvu na kisha kuondoka kwa mwendo wa kasi.kwa kuwa mlengwa anakuwa kama ameshitukizwa na pia kushtuka kwa tukio, bado anakuwa haamini kilichotokea na hivyo huduwaa.huku mkupuaji akimwacha kwa mbali na waliokaribu kuanza kuelewa kilichotokea.akina mama /dada chukueni tahadhari na jaribuni kuripoti matukio haya polisi.pia ukiweza chukua/andika namba za chombo husika katika tukio.je wanajamii hili mnalionaje?
 
Kwa kweli ni hatari sana. Fikiria kina dada humo huweka vitu vyao muhimu kama lipstick, vitambulisho nk. Kwa kufanyahivyo ni kuathiri maisha ya watu. Kwa kweli njaa ni darasa katika dunia
 
Sio kwa kina dada/mama tu. Pia wababa/wakaka. Wakaka wamekwapuliwa sana laptops kwa style hii.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom