AIBU: Uwanja wa ndege wa Dar es Salaam wakosa umeme, ndege zashindwa kutua!

JK ameahirisha safari zake za nje shauri ya janga la wenzetu Zanzibar, sidhani kama ameamua kupaa kwenda Egypt kusuluhisha maandamano kwenye ubalozi wa Israel nchini humo...lakini huenda katumwa na wakubwa.


Mkuu hao "wakubwa" ni wale waliomnunulia suti?
 
Hiyo ndo Tanzania bwana. Ngoja uone shamra shamra za miaka 50 ya uhuru, utadhani hatuna matatizo kabisa.

Ni kwa jinsi gani tunaweza kushindana na Kenya kama hata ndege zinashindwa kufanya safari zake au kutua kwa sababu ya umeme. Wanaweza kusema ni sababu ya msiba Zanzibar!!!!
 
Leo, Jpili 11/09/11 majira ya saa nane usiku umeme ulikatika ghafla katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere. Mimi nilikuwa mmoja wa wasafiri walioathirika na kukatika umeme huo kulikonifanya nishindwe kufanya connection yangu on-time kwenye moja ya uwanja wa ndenge nje ya nchi nilipopaswa kufanya connection. Matokeo ya kukatika umeme kulisababisha ndege zote zilizopaswa kutua hapo kwa wakati huo kutua kwenye uwanja wa Zanzibar kwakuwa taa za kuongozea ndege kwenye runway zilikuwa hazifanyi kazi. Hivi ni kweli jamani the only gate-way to our country inashindwa kuwa na umeme wa uhakika. Ni nani atakayezilipa airlines gharama za ziada za kutua kwenye viwanja vingine vya ndege, gharama za mafuta ya ziada, ggharama za kuchelewa, gharama za kushindwa kuwaunganisha abiria waliotakiwa kuunganisha ndege kwenye viwanja mbalimbali Duniani. Hivi inakuwaje kama ndege ina approach run-way kisha ghafla taa zinazimika? hivi tunafahamu kweli impact ya haya mambo kwa sisi tunaoongoza taasisi hizi? Uwanjani kulikuwa na kelele nyingi sana za abiria wa ndani na wa nje wakitukana na kushutumu, inasikitisha sana kuona kuwa tunashindwa hata kuwa na automatic generator kwenye uwanja wa ndege so called wa Kimataifa. Ndugu zangu naomba wale wanaohusikia au wanaowafahamu wanohusika walifanyie kazi hili ili kuondoa aibu hii na kuepusha ajali pia. Saa hizi mimi binafsi nipo stranded kwenye moja ya airport kwakushindwa kuunganisha ndege kwa wakati muafaka.
 
Hata wangetua wangeishia kuingia gizani tu. Manake unafika airport kuna umeme kwa kuungaunga, unatoka nje hakuna umeme hadi chumba unachofikia pia hakina umeme!

Umeme utangazwe ni janga la taifa ili tupate misaada kama wanayopata Wasomali kwa sababu ya njaa.
 
hii ni aibu sana...imagine kwa jana, jumamosi, SWISS na KLM pamoja na ndege za bongo kibao huwa zinatua....ni aibu ya aina yake!
 
Wana JF: Hii aibu ni kubwa kuliko, niko somewhere in Europe attending a workshop and this morning tulipaswa kupokea wageni from different parts of the world, the discussion this morning has been that delegates from Tanzania wameshindwa fika kutokana na power problems in the airport. Hii inaaibisha kuliko tunavyodhania, na ni wiki mmoja tu Ngeleja akizungumzia swala la kupata suluhisho la hii tatizo. what a shame
 
Kila uchaguzi una matokeo kama vile kupanda mbegu kuiivyo na matokeo. Iweje waliopanda washangazwe na mavuno yao au wale waliochagua na chaguo lao?
mwanakijiji una uthibitisho gani kuwa watanzania walipanda mbegu hii?usijekuta mbegu tulizopanda zilifukuliwa usiku usiku halafu zikapandwa hizi tunazokula matunda yake kwa sasa.ninaamini watanzania ni wakulima wazuri sana !!!!
 
wana JF, hii aibu ni kubwa sana, this morning we were to have a meeting somewhere in Europe with delegates from tanzania. But we are told kwamba they failed to leave yesterday with swiss air and it has been a morning topic in the meeting. Hii ni aubu kubwa ati ndege zinashindwa kutua na kuondoka cos of umeme at the same time boti inaua watu.What a crisis and where are we going.
 
Umeme uko Igunga. Waulizeni watu wa Tabora, Nzega, Igunga, Nyandekwa, Ziba, Bulyang'ombe, Usongo, Nkinga, nk kama wamekatiwa umeme tangia kampeni zimeanza. Megawat zote za airport zimesafirishwa kwenda Igunga na vitongoji vyake!!
 
Umeme uko Igunga. Waulizeni watu wa Tabora, Nzega, Igunga, Nyandekwa, Ziba, Bulyang'ombe, Usongo, Nkinga, nk kama wamekatiwa umeme tangia kampeni zimeanza. Megawat zote za airport zimesafirishwa kwenda Igunga na vitongoji vyake!!
<br />
<br />
Mmekusoma Mkuu!
 
poa tu si kikwete na ngeleja wanaona sawa tu?natamani km nchi nzima ikose umeme kwa wiki nzima ili tupate akili kidogo ya kuwawajibisha awa wahuni wasioona hasara tunayoingia
yani nchi ingine ushawajibika kitambo,tujifunze ya japan
 
Kweli hii ni fedheha kubwa ,Inamaana hawa wanaosimamia uwanja hawana Standby Generator ! Hii nchi inakoelekea ni kubaya sana .Watu hatuna umakini hata kidogo..
 
Kutakuwa na technical problem, aibu ni mgmt ya uwanja huo, but if u put safety first, u better not land least u get fatalities
 
Back
Top Bottom