Aibu rais kulala hadharani!

Ochu

JF-Expert Member
May 13, 2008
975
47
anagalieni rais wenu anavyolala hadharani
2722d1224755716-aibu-rais-kulala-hadharani-jknauchovuwatrip.jpg

 

Attachments

  • jknauchovuwatrip.jpg
    jknauchovuwatrip.jpg
    59 KB · Views: 1,006
It is not a joke to be Vasco da Gama. safari kibao what do you expect. anachoka and therefore hata productivity yake is dimishing. ndiyo maana anauchapa usingizi live. je muambata wake alikuwa wapi? should be sacked immeadetely kumuacha bosi wake auchape hadharani.
 
Alikuwa anataka kujikuna shavu la kulia kwa kutumia bega, ila kwa stail ya kuinamisha kichwa upande wa kulia bila kunyenyua mikono. Tatizo ni hizi picha zinaonyesha micro-second ya jambo. Ingelikuwa Video tungeliamini. Ila kama ni kweli, huwezi jua jana usiku alikuwa wapi........
 
Rais kweli ni wetu kwa vile sio wako, hii ilikuwa kwenye msiba wa Mbatia, hakuwa amelala alikuwa anajaribu kujiweka sawa,

saaa nyingine tunazidisha mno na kuishia kujishusha hadhi.

thanxs!
 
Haiwezekani akawa ameuchapa usingizi,alikuwa anajaribu kusikiliza proceedings kwa makini.
 
Rais wetu ana matatizo mengi mengine lakini ulalaji usingizi sio lake, infact huwa sielewi analala saa nagapi, maana the man is alyaways up and active, ingawa tatizo lipo kwenye results!
 
...kuna dawa nyingine zinakuja na maelekezo kama, "this syrup may cause drowsiness, or sleepness. Do not drive or operate machinery when taking it". Walaumiwe hao ma-chemists kutokusema "and do not attend rallies!"

...tumuonee huruma mheshimiwa jamani, huenda alikuwa on medication ya flu, etc..
 
Kumbe kwenye Msiba? Hivi kwa nini sisi Tanzania, na weusi wetu wote huu, inapokuja kwenye mazishi tunavaa SUTI nyeusi? Niliona mazishi ya yule mchezaji wa Cameroon Vivian Foe, wachezaji wenzake wa Lion walikuwa ndani ya Suti nyeupe. Nikajua kuwa kwa Waafrica, ni nguo nyeupe wakati wa msiba. Ila naona hapa tumePAST & Copy kutoka kwa wazungu. Au mie nimeelewa Kivyangu? Mwenye kujua zaidi anifafanulie.
 
alikuwa anataka kujikuna shavu la kulia kwa kutumia bega, ila kwa stail ya kuinamisha kichwa upande wa kulia bila kunyenyua mikono. Tatizo ni hizi picha zinaonyesha micro-second ya jambo. Ingelikuwa video tungeliamini. Ila kama ni kweli, huwezi jua jana usiku alikuwa wapi........

swali lako lingweza kujibiwa kama angekuwa new york tungeweza kusema kitu kwa kumuuliza jogwe
 
FMes,
Nasikia kwa kulala, Rais wa Guinea Conacry aendaye kwa jila la Lansana Conté ndiyo mwenyewe. Na watu hata huwa hawajali kama amelala. Sanasana watashanga kama hakulala. Siku moja alienda kwenye concert ya yule Albino kutoka Mali aitwaye Salif Keita. Mziki umeanza mzee huyoo kalala. Ikafika wimbo mmoja muhimu sana kwake huyu mwanamuziki, ikabidi aombe msamaha na kumwamsha Rais. Nasikia ilikuwa tukio la mwaka. Ila kweli Conté aliamka na kujitahidi kuusikiliza hadi mwisho. Huyu Conté ukilinganisha na Ubovu wa Kikwete unaona kuwa kumbe Tanzania kuna rais mzuri sana.
 
Kwenye la kulala nitamtetea mpaka mwisho maana nimemuona kwenye kampeni za urais, infact hata leo pamoja na urais wake bado anayo nafasi ya ku-reach out washikaji zake wote wa kawaida saa za usiku, na ndio muda huingia hata hapa,

Mengine sawa lakini hili la kulala hapana sio kweli!
 
Hata kama ali lala kweli kwani tatizo liko wapi? Yule ni binadamu kama wewe hana tofauti yoyote Angekuwa anahutubua harafu mara ana uchapa usingizi hapo sawa.Lakini kuketi ktk kiti na kuuchapa usingizi ni jambo la kawaida mno
 
Hata kama ali lala kweli kwani tatizo liko wapi? Yule ni binadamu kama wewe hana tofauti yoyote Angekuwa anahutubua harafu mara ana uchapa usingizi hapo sawa.Lakini kuketi ktk kiti na kuuchapa usingizi ni jambo la kawaida mno


tena ukizingatia maswala ya umri......kulala-lala kunakuwa inevitable kwa baadhi ya watu....so rais anaweza kuwa katika hao baadhi.
 
aaaahh.....jama acheni hizo.......

pale ilikuwa msibani (Msiba wa Mar Mh.Salome Mbatia)..........ilikuwa ni wakati wa huzuni....Rais anaonekana ameinamisha kichwa kuashiria huzuni (na sio amelala).....na ukiangalia mkanda wa video......utakubaliana nami......

....someone managed to get that pose....either from the video or from the camera itself (which is possible)........
 
tunaogopa visije vikawa vituko vya Boris Yelstin wa Russia enzi zake!!!!
 
..kikwete anajulikana kama mtaalamu wa kukesha ..hata alipokuwa waziri ...alikuwa anakwenda disco hadi saa kumi alfajiri ..na saa 12 ..yupo barabarani ....sana sana tatizo lake kuu ni kuchelewa miadi na kwenda kwenye appointments un prepared......just because previous night hana kawaida ya kupitia memoirs zake kujua ratiba ya siku inayofuatia..kupitia speeches za siku inayofuatia,kupitia agenda za miadi ya siku inayofuatia ..ets etc......so anahitaji awe na msaidizi mwenye akili ya kutosha kufanya hayo kwa niaba yake na at least apate one hour kila siku kabla ya kuanza kwa ratiba kumpa briefing ya ratiba na kumwambia cha kusema....na yeye aongezee yake.......

Muda anaokesha usiku hautumii kwa mambo ya msingi...na kuchelewa miadi hutokana na tabia yake ya kuzidisha muda kwa mambo ambayo hayapo kwenye ratiba...ie amepangiwa kuongea na mtu dk 15 akatumia dk 30 ..tayari ameshaharibu ratiba.......
 
..nilisoma kitabu cha "the making of african statesman:moi"

alielezea ratiba yake kama mtu anayeamka mapema zaidi na kulala late zaidi .....na hakuna mzaha kati kati.....

Saa 10.00 alfajiri kila siku huamka na kusali kwa dk 30.....
Saa 10.30 kamili hufanya mazoezi ya viungo [dk 30]
saa 11 kamili huoga na kuvaa [dk 30]
saa 11.30 hupata kifungua kinywa [uji na maziwa]..ets na kuelekea ofisini
saa 12 kamili bendera ya jamuhuri inapopandishwa yeye tayari huwa ofisini
na kazi ya kwanza aliyokuwa akifanya ni kuwasiliana na wakuu wa ulinzi na usalama kupata taarifa,,...

Baada ya hapo ratiba yake ya kazi za ofisini hukamilika saa 12....hurudi nyumbani na kupumzika kidogo ...saa mbili kamili hupata mlo..na kuendelea na vikao na wasaidizi wake hadi saa 4 usiku au 5..baada ya hapo hupata muda wa kusoma taarifa ya kazi zake za kesho aliyoandaliwa na msaidizi wake....

Mara nyingi inaelezwa kuwa alikuwa akilala saa 7 hadi 8 kila siku..........na wala haikuwa ajabu kuwa na miadi ya kikazi hadi saa 6 usiku.....

Nadhani ratiba kama niliyoieleza hapo juu ni kielelezo tu cha ratiba za viongozi waliodhamiria ....haitatofautiana na ya mwalimu...,na wengine kama hao.....

Tatizo na viongozi ambao ikifika usiku kama saa hizi badala ya kufanya tafakari ......huyoo anajiiba kwenda kariakoo kucheza dhumna na maswahiba ....ambao hawana la kumshauri..au kona kona!!
 
Back
Top Bottom