AIBU: Rais Kikwete azuiwa kusoma ripoti...

dah wadau kwakweli inasikitisha kama sio kuhuzunisha hivi hao maafisa wanafanya kazi gani hasa na wanalipwa mishahara ya nini kama hawawezi kutekeleza majukumu yao kama inavyowapasa kufanya huko tuendako ni kiza kinene kama hali ndio hii
 
Daaahh, aibu gani hii kwa taifa letu jamaniiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hii ndiyo ari mpya, nguvu mpya na kasi mpya ya msanii Kikwete

MKuu hii nchi ni kama inaendeshwa na genge la mission town. Yaani kwenye kulipa madeni ya Dowans na mikataba mingine ya Ki-Carl Peters watendaji wako faster kupigia chapuo-kwa kuwa kuna %, ila ada ya laki moja kwa mwaka wanaona ni hasara. Halafu bado unataka tuendelee kuheshimika kimataifa. Nimesikiliza Mwakyembe akiwapasha wafanyakazi wa ATCL nao, walipopata Insurance compasition ya $7m baada ya ajali ya ndege ya Kigoma mabosi wakawa busy kuwapigia Creditors (Wadai) simu kuwa hela imeingia waongeze bidii kudai madeni yao, na mpaka mahakama ikashikilia kiasi, wakati mpango ulikuwa ni kuzi-invest hizo pesa ili ATCL iwe na ndege zake acha hizi za kukodi. Yaani sisi ni watu wa ajabu sana.

Mimi ndiyo ningekuwa JK nimezuiwa kusoma report kwa sababu hii basi hii ingeondoka na watu wizarani. Ina maana jamaa tokea alipoondoka wizara ya mambo ya nje na kuingia Ikulu subscription ika-stop. Kweli Tanzania ni nchi ila ni nchi ya ajbu kabisa duniani. Watu hawana uzalendo kabisa, kila kitu kama hakina faida na wewe japo ni kwa ajili ya pro bono you don't give a damn!
 
  • Thanks
Reactions: BAK

images

Ha, ha, haaa...mbavu zangu, Kikwete anaangushwa tu na wasaidizi wake!

Kwani yeye mwenyewe huwa hajiangushi?? Ukiachia mbali kiutendaji, hata kimwili huwa anajiangusha kama alivyofanya jangwani 2005
 
....kaaazi kwelikweli...
...wezi tuwasamee na ikibidi tuwalipe...
...halali tusilipe, hazina faida kwa mifuko yetu...
 
MKuu hii nchi ni kama inaendeshwa na genge la mission town. Yaani kwenye kulipa madeni ya Dowans na mikataba mingine ya Ki-Carl Peters watendaji wako faster kupigia chapuo-kwa kuwa kuna %, ila ada ya laki moja kwa mwaka wanaona ni hasara. Halafu bado unataka tuendelee kuheshimika kimataifa. Nimesikiliza Mwakyembe akiwapasha wafanyakazi wa ATCL nao, walipopata Insurance compasition ya $7m baada ya ajali ya ndege ya Kigoma mabosi wakawa busy kuwapigia Creditors (Wadai) simu kuwa hela imeingia waongeze bidii kudai madeni yao, na mpaka mahakama ikashikilia kiasi, wakati mpango ulikuwa ni kuzi-invest hizo pesa ili ATCL iwe na ndege zake acha hizi za kukodi. Yaani sisi ni watu wa ajabu sana.

Mimi ndiyo ningekuwa JK nimezuiwa kusoma report kwa sababu hii basi hii ingeondoka na watu wizarani.
Ina maana jamaa tokea alipoondoka wizara ya mambo ya nje na kuingia Ikulu subscription ika-stop. Kweli Tanzania ni nchi ila ni nchi ya ajbu kabisa duniani. Watu hawana uzalendo kabisa, kila kitu kama hakina faida na wewe japo ni kwa ajili ya pro bono you don't give a damn!

Mkuu Hoftstede bahati mbaya msanii Kikwete hajiamini na uchafu aliokuwa nao ambao wengi ndani ya magamba wanaufahamu unamuogopesha kuchukua hatua muhimu dhidi ya subordinates wake. Kumbuka jinsi Watanzania tulivyokuwa tunapigia kelele uzembe katika Serikali yake lakini hakuwahi kumfukuza hata mtendaji mmoja. Kama siyo Bunge kuchachamaa hivi karibuni basi Mkullo, Maige, Ngeleja wangekuwa bado wanapeta katika baraza la Mawaziri.
 
Back
Top Bottom