Aibu kubwa kwa wanawake na wanaume tanzania.....

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,063
115,462
ETI WANAWAKE WANAWEZA....HAYA SOMENI WENYEWE HAPA....

SIJUI HII NI AIBU YA WANAWAKE PEKEE YAO,
AU YA WANAUME PEKE YAO,

AU YA KWETU WOTE, BUT NI AIBU KWA KWELI.....


45% ya Wanawake wenye Ajira wametoa Rushwa ya Ngono!
?45% wanawake, wasichana wamepata kazi kwa ngono?


Wednesday, 16 March 2011 20:36


Nora Damian
ZAIDI ya asilimia 45 ya wanawake na wasichana walioajiriwa kwenye ofisi mbalimbali nchini, zikiwamo za serikali walipata ajira hizo baada ya kutoa rushwa ya ngono, imeelezwa.

Hayo yalisemwa jijini Dar es Salaam jana na Mwenyekiti wa Asasi ya Ushauri Nasaha na Maisha ya Familia (CAFLO), Mariam Mlugu, kwenye mafunzo kwa viongozi wa serikali za mitaa kuhusu unyanyasaji wanawake na wasichana katika familia.

Mlugu alisema hali ya unyanyasaji wa mwanamke imekuwa ikiongezeka kila siku, hasa ngazi ya familia na kaya, kazini na maofisini.“Wengi wa wanawake na wasichana, wamekuwa wakinyanyasika kingono ikiwamo kubakwa, kupigwa na kunyimwa haki ya kurithi mali na hata kuuawa,” alisema Mlugu.

Alisema zipo sababu mbalimbali zinazowafanya wanawake kunyanyasika, kama kutofahamu haki za binadamu, mfumo dume, mawazo mgando, mila, desturi na wanawake kutotambua nafasi na majukumu yao kwenye familia.

Pia, Mlugu alisema unyanyasaji wanawake na wasichana haupo Tanzania peke yake, kwani ni tatizo ambalo limeenea sehemu nyingi duniani na kutolea mfano Afrika Kusini kuwa, hadi kufikia mwishoni mwa mwaka jana, wastani wa wanawake watatu walikuwa wakibakwa kila baada ya dakika 90.

Mwenyekiti huyo alisema unyanyasaji mwanamke unaleta madhara makubwa kwenye familia na jamii, kama kushuka kwa kasi ya maendeleo, kuongezeka kwa umaskini, kupotea kwa hadhi na thamani ya utu wa mwanamke.
Kwa mujibu wa mwenyekiti huyo, madhara mengine ni kusambaratika kwa familia, kuongezeka kwa matatizo kama Ukimwi, vifo na watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.

Nao viongozi wa serikali za mitaa walioshiriki mafunzo hayo, ambao wanatoka kata za Buguruni na Vingunguti, waliaswa kuwa na mikakati mahsusi ya kutokomeza unyanyasaji huo, kwani wao ni wadau wakubwa wa mapambano hayo.

Pia, viongozi hao walitakiwa kuimarisha mabaraza ya usuluhishi kwa kuwawezesha wadau, kupata mbinu sahihi na utaalamu wa kutatua kesi mbalimbali zinazoletwa kwenye mabaraza yao.Mlugo aliwataka wanaume kutumia nafasi zao kuleta maendeleo ndani ya familia, bila kubagua wanawake kwani wakipewa fursa wanaweza kuleta mabadiliko ya familia na taifa.​
 
Saa nyingine huwezi kuangali kazi yako inakuponyoka mbele ya macho yako..
Una familia ya kulisha Una watoto shuleni ..
Na mara nyingine we single parent..
u have to do what ever it takes to keep up with ur family demand..

Kwa kweli si kitu kizuri
but that's life..

Ni makosa yetu wote kama taifa na si mtu mmoja..
Silipend I hili jambo kabisa..

Lakini haya maisha unayachukulia kama yanavyokuja..
 
Saa nyingine huwezi kuangali kazi yako inakuponyoka mbele ya macho yako..
Una familia ya kulisha Una watoto shuleni ..
Na mara nyingine we single parent..
u have to do what ever it takes to keep up with ur family demand..

Kwa kweli si kitu kizuri
but that's life..

Ni makosa yetu wote kama taifa na si mtu mmoja..
Silipend I hili jambo kabisa..

Lakini haya maisha unayachukulia kama yanavyokuja..

pole sana,
unazungumza kama yamekukuta...
 
Nashukuru naweza kukwepa haya yote mpaka kufikia nilipo ila ni kweli yapo na lilikukuta huna jinsi kama alivosema AD hapo juu
 
pole sana,
unazungumza kama yamekukuta...

Mmhhh nimeshuhudia
kumbuka hakuna apendae bad repetition
wala kukutwa na mambo kama hayo

Lakini ndo maisha
saa nyingine there is no way out ..
Mpaka hapo nchi yetu ibadilike sheria ziwe
Zinafuatwa ...
kuwe na kazi za kutosha ili ukibabaishwa huku
unaweza kuchapa mwendo. ...
 
Hapa tunaangalia hili la rushwa ya ngono tu pengine kwa sababu huyu dada mtoa takwimu amelianza mwanzo, lakini mada nzima inahusu unyanyaswaji wa wanawake na wasichana kutokana na mfumo dume.

Kama alivyosema AD, mara nyengine dada zetu wanalazimika kukubali wasiyoyapenda kwa sababu hakuna jinsi. Kukubali kwao kamwe kusichukuliwe kuwa ni udhaifu wao bali mazingira yanawalimisha. Afanye nini? Akikataa, hamna kazi. Akishitaki, hamna kazi na anajenga uadui. Pengine yeye aonekane mnafiki. Tumeshayaona mifano humu: M'mke anamshitakia mume wake kuwa anatongozwa na fulani, jawabu zimetoka eti kwa sababu hampendi mtongozaji, anaowapenda hasemi. Hii inauma sana.

Kuhusu unyanyaswaji wa wanawake ni suala la dunia nzima, mabara yote. Mifano ni mingi. Wanawake wanalipwa kasoro kuliko wanaume kwa kazi ile ile, hasa katika sekta binafsi. Pia kuna unyanyaswaji wa ndani, kupigwa, kubughudhiwa na hata kuuliwa. Spain kwa mfano, takwimu zinaonesha wastani wa wanawake 6 wanauliwa na waume/wapenzi ma-ex wao kila mwezi.

Pia suala la ubakaji wa wanawake, wasichana na hata watoto wadogo limeenea ulimwenguni kote. Cha ajabu, zimeongezeka tabia za wavulana (wadogo) chini ya umri wa miaka 18 kubaka na kuua wasichana. Vile vile kumeongezeka tatizo la "pedophile", yaani kuharibu wasichana wadogo ama moja kwa moja au kuwanyanyasa katika mitandao. Jambo linaloudhi zaidi ni kuona wakuu wa dini na imani wanashiriki katika katika unyanyasaji wa watoto wa kiume na wasichana.

Mengine ni biashara ya ngono, yaani kusafirisha wasichana kutoka nchi/bara moja kwenda jengine kwa kuwalazimisha kufanya umalaya, ubakaji wa wanawake katika nchi zenye vita... pamoja na maovu mengine mengi ambayo WANAUME (kama wana sifa ya kuitwa hivyo) ndio watekelezaji wakuu.

Bado ipo haja kwa Tanzania kupitia na kurekebisha sheria zetu ili kulinda haki za wanawake, kutoa elimu ya uraia kwa raia wote ili tufike pahali tukubali na kutekeleza kwa vitendo kauli ya kuwa binadamu wote ni sawa, isiwe kwenye makaratasi tu.
 
"Mi Tanzania ndivyo tulivyo", tunaacha hata kazi za Kanisa kwa ajili ya chini, nani abishae?
 
"Mi Tanzania ndivyo tulivyo", tunaacha hata kazi za Kanisa kwa ajili ya chini, nani abishae?

Hakuna abishae! Hata kazi za kuendesha nchi tunaacha kwa ajili ya chini, nani anabisha!!

Anyways it is a serious problem especially in TZ and Africa in general! inauma!!! Elimu ya maadili ndio suluhisho....kutoka vidudu hadi chuo kikuu ...
 
Wanawake wanamis-use k zao! Mara wauze, mara waringishie...sasa nashindwa kuelewa wapi unachora mstari na kusema huyu nampa na yule simpi, nk! out of topic but wanted to get it out!
 
its both sides but im different style. Hata wanaume hutakiwa kuwapa kichapo maboss wanawake ili mambo yao yaende sawa. Tuulizeni ss wanaume tutawapeni issues . Bosi sura mbaya ,unajifanya unamtongoza kumbe yeye ndicho anachotaka, unafanya kweli ili tenda yako ya kusupply stationaery ipate backup . Haishii hapo, ukipata tenda uendee kumridhisha na fedha juu. You may call sex anything but using it for your benefit
may not amount to unyanyasaji , othewise ni ubakaji. worse enough baada ya sex hamna anayedai ametoa au amekula rushwa ya ngono wote hufurahi tu. Bora mtoa mada angekuja na hoja kwamba wanawake wazuri wanawanyima wengine fursa maana
Uzuri wao unachochea matamanio ya ngono, hivyo kupata kazi kirahisi kuliko wenzao wasio na mvuto, may be hilo ndio lingekuwa tatizo. Ni mtizamo tu .
 
Saa nyingine huwezi kuangali kazi yako inakuponyoka mbele ya macho yako..
Una familia ya kulisha Una watoto shuleni ..
Na mara nyingine we single parent..
u have to do what ever it takes to keep up with ur family demand..

Kwa kweli si kitu kizuri
but that's life..

Ni makosa yetu wote kama taifa na si mtu mmoja..
Silipend I hili jambo kabisa..

Lakini haya maisha unayachukulia kama yanavyokuja..

Wakati huo ukimwi unaweka pembeni si eti eeeh teh teh greti thinka
 
Kweli kabisa Chapakazi maana huwa tunajifanya wenyewe.

ukienda interview umepiga vazi la kazi bila kuweka mtego wowote, nani atapata nafasi ya kukuomba? Unaingia kwenye interview umevaa mini-skirt, maziwa nje,...what image are you creating?
Another question...kwa nini mademu wanavaa vimini? kuna demu alinijibu ni ili kujifurahisha mwenyewe! nilitaka kucheka kwa nguvu sana!
 
ukienda interview umepiga vazi la kazi bila kuweka mtego wowote, nani atapata nafasi ya kukuomba? Unaingia kwenye interview umevaa mini-skirt, maziwa nje,...what image are you creating?
Another question...kwa nini mademu wanavaa vimini? kuna demu alinijibu ni ili kujifurahisha mwenyewe! nilitaka kucheka kwa nguvu sana!

Acha kutusingizia
Kuna wanaume wengine hawana
heshima hata uvae gunia...
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom