Balozi wa tz Sweden ni swahiba mkubwa wa Mkapa... na alimpa huo ulaji wakati anafungasha virago ikulu... Anyway Ubalozi huu nadhani ndio unaoongoza kwa uzembe kati ya balozi zote. Hata wakati wa kubadilisha passport waliwaliza wabongo hela nyingi tu i.e. walitoza gharama za juu kulinganisha na gharama halisi
Dr. Ben Moses amekuwa balozi kwa muda mrefu sasa, ninakumbuka amewahi kuwa balozi wa Tanzania nchini Japan pia, na kabla ya kuwa balozi Japan amewahi kuwa Principal Secretary kwenye moja ya wizara. Kwa hiyo, uteuzi wake kwenda sweden ilikuwa ni kubadilisha kituo na si kweli kwamba aliteuliwa wakati mkapa anafungasha vilago. Nadhani amekuwa balozi nchi mbalimbali kwa kipindi chote mkapa akiwa madarakani