Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,883
- 6,884
Wengi waanguka mtihani wa NBAA
MATOKEO ya mtihani wa Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi Hesabu (NBAA) uliofanyika Novemba mwaka huu, yameidhinishwa na kuonesha kuwa idadi kubwa ya watahiniwa hawakufanya vizuri katika mtihani huo. Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji NBAA Pius Maneno, mtihani huo ulihusisha watahiniwa wa ngazi za ATEC I, ATEC II, Foundation Stage Modules A na B, Intermediate Stage Modules C na D na Final Stage Module E na F.
Alisema kati ya watahiniwa 3,414 waliofanya mtihani wa NBAA, watahiniwa 854 sawa na asilimia 25.0 walifaulu na wengine 1,048 sawa na asilimia 30.7 watatakiwa kurudia masomo waliyoshindwa huku watahiniwa 1,512 sawa na asilimia 44.3 hawakufaulu mtihani huo.
Aidha alisema katika ngazi ya mwisho ya F watahiniwa 260 sawa na asilimia 29 kati ya 874 ya watahiniwa waliofanya mtihani wamefaulu, na wengine 284 sawa na asilimia 32.5 watarudia somo moja na watahiniwa 330 sawa na asilimia 37.8 hawakufaulu.
Vilevile watahiniwa 362 sawa na asilimia 19.2 kati ya watahiniwa 1,883 wamefaulu mtihani wa taaluma ngazi ya Module E na wengine 471 sawa na asilimia 25.0 watarudia somo moja ambapo watahiniwa 1,050 sawa na asilimia 55.8 hawakufaulu, alisema Maneno.
Alisema kwa upande wa mtihani wa Shahada ya juu ya Uhasibu nchini (CPA) watahiniwa 268 walifaulu na hivyo kufikisha idadi ya watahiniwa waliofaulu mtihani huo wa CPA 3,876 tangu mtihani huo uanze mwaka 1975.
Kwa ngazi ya Module D, watahiniwa 37 sawa na asilimia 33 kati ya 109 wamefaulu na wengine 62 sawa na asilimia 56.9 watarudia somo moja huku watahiniwa 10 sawa na asilimia 9.2 hawakufaulu.
Katika mtihani wa Module C watahiniwa 37 sawa na asilimia 29.8 kati ya 124 wamefaulu na 40 sawa, asilimia 32.3 watarudia somo na 47 sawa na asilimia 37.9 walifeli.
Katika ngazi ya uandishi na utunzaji wa vitabu vya hesabu (ATEC II) watahiniwa 31 sawa na asilimia 25.6 kati ya 121 wamefaulu, 43 sawa na asilimia 35.6 watarudia somo na watahiniwa 47 sawa na asilimia 38.8 hawakufaulu.