Ahsanteni kwa salam za faraja

Bishanga

JF-Expert Member
Jun 29, 2008
15,323
10,050
Naomba nichukue fursa hii kuwashukuru kwa salam za faraja mlizonitumia kupitia MMU kufuatiwa kuondokewa na baba yangu mpendwa.Wapendwa Dena,Sweetlady,Wakumwitu,Pdiddy,Likasu,Freetown,Sweetdada,Baba Enock,Mayenga,Baba Lao,NATA,Kure(avatar yako kiboko!),Afro Denzi,PakaJimmy,Susy(na wewe again pole na msiba wa dada),Freema Agyeman,Edson,Fidel80,Simbamiwene,Ivuga,Iza,Saharavoice,Pearl(na wewe pole mama kwa kuondokewa na baba ),Miss Judith,Dark City,Mwanajamiione,Lizzy,Blakiwoman,Mpevu,Jaguarpaw,Bubu ataka kusema,Mpendwa,Mtumishi wetu,Nnunu,Born town(avatar ya kikombe,du!),Chapakazi,Pota,Ferdinandes Rodri,Eltorro,Mbimbinho(avatar yako mwisho wa matatizo!),Mzee punch(wa UDSM 80's?,msiba ulikuwa bukoba),The Finest,Husniyo,Sugar wa ukweli,Jomse,Maalim Jumar,Michelle,Mufiya Kicheko,ANY,Chetuntu,Gaga na Quinty nawashukurini sana kwa salam zetu.
Gaga amezungumzia suala la ubani,mi nakubaliana naye maana kusema kweli kupitia MMU baadhi yetu kupitia keyboard tumejenga undugu.Nashauri Ndugu Maxence asajili namba vodacom/tigo/airtel specific kwa ajili ya kutoa rambirambi na misaada kwa wana MMU wenye shida.Kupitia namba hii tunaweza kuwa tunachangia wenzetu wenye matatizo na Maxence anaweza kuwa anawa PM waliochangiwa ili awapitie michango yetu.
Kwa mara nyingine nawashukuruni sana wana MMU,tuendelee na moyo huu huu.
 
Tunashukuru na wewe! Mungu azidi kukubariki na kukupa nguvu zaidi! Karibu tena Jf!
 
Pole kwa msiba Bishanga karibu tena ndani ya jumba la Almas. Eti kaka umekuja kuendeleza ile biashara yako ya pumba?
 
Natumai umerudi salama, pole pia kwa uchovu wa safari ndefu.
HAIJALISHI TUMEPITIA AU TUNAPITIA MAGUMU KIASI GANI, LAKIN LAZIMA MAISHA YAENDELEE.
Karibu tena JF.
 
Karibu tena, tunafurahi kwa kurejea kwako

Mungu aendelee kuwafariji wafiwa wote
 
Pole kwa msiba Bishanga Mungu aendelee kukupa nguvu. karibu mtaani tena
 
Pole sana Bishanga na karibu tena (nasikia huko kwenu wanasema hivi..mwagila ibi).

Naunga mkono hoja ya kuwa namba maalum ya wanajukwaa wa MMU ili tuweze kuitumia kutuma michanggo yetu au rambi rambi zetu. Hii itasaidia kumtumia mtu mchango wako bila ulazima wa kumtafuta yeye kwa simu au kumwona endapo hupendi kufanya hivyo!

Binafsi nisingependa kulazimika kumwona DA, AD, Maty au TF eti kwa sababu nataka kumpa mchango wangu, uwe wa harusi au jinginelo!
 
Ahsante Dark City,'mwagila ibi'unaitikia 'elitagalaile'.Kwetu kuzika mtu mzima ni shughuli pevu maana watoto mliofiwa mnakuwa na shughuli pevu 'kupambana' na wajukuu,ukicheza hata maiti ya baba yako wanaweza kuichoropoa ndani na kuificha porini hadi muikomboe! kwa kweli wajukuu wanachangamsha sana msiba wa watu wazima.
 
Kweli mkuu, nilishawahi kushuhudia mahali na ndipo nilipoambia hayo maneno.

Natumai Mungu atakupa nguvu wewe na familia yote ili muyaanze vema maisha mapya bila mpendwa wenu!
 
karibu mkuu,Mungu azidi kukutia nguvu, kuhusu avatar ni mambo ya JF shemeji,sie tumeoa bukoba,kwangu huo ni msiba wa baba mkwe. karibu jamvini tena.
 
karibu mkuu,Mungu azidi kukutia nguvu, kuhusu avatar ni mambo ya JF shemeji,sie tumeoa bukoba,kwangu huo ni msiba wa baba mkwe. karibu jamvini tena.

Ahsante shemeji Kuree11,hongera kwa kuoa kwetu,bila shaka mnafaidi matoke na njugu mawe na 'nsanyuse'!
 
Back
Top Bottom