Ahsante Mungu, wife amejifungua salama

Kubeba mimba na kujifungua salama ni jambo jema na la kumshukuru Mungu!..Hongereni sana wazazi wapya! Malezi mema na welcome to the parenthood!!
 
Siku hizi ukiwa mjamzito na ukajifungua salama ni bahati ndugu yangu, Joji amefurahia hiyo bahati so akaona si vibaya kushea furaha yake na memba wenzie... Wanawake wanakufa sana wakat wa kujifungua...
Sweetlady umenena ukweli mtupu! Jojipoji ana kila sababu ya kuonyesha furaha yake hapa.Maana siku hizi ukiwa mjamzito ni kama unatembea na kifo.Hongera sana Joji!!!!!!!!!
 
hehehe hongera mwaya maana kuna wengine hawajaaliwa. Ushauri wangu mengine nimeyatoa kwa imani ya dini yangu hivyo badilisha kwa imani yako kama wewe ni mkristo lkn natumai utazingatia
1. utakapoenda hospitali kumuona mtoto wako hakikisha umechukua udhu na uko tohara kitu cha kwanza mpe salaamu uyo mtoto (asalaam
aleikum au kwa kiswahili amani iwe juu yako na msamaha uwe juu yako)
2. Mpigie adhana kwenye sikio la kulia na kimu sala kwenye sikio lake la kushoto
3. Mshike kichwa na kumuombea dua kwa Mungu amuepushe na mabalaa na awe mtoto mwema
4. Mtolee sadaka siku ya arobaini kwa kupima nywele zake halafu linganisha uzito wa nywele zake na dhahabu na tuo sadaka ya kiasi cha
fedha kulingana na uzito huo kwa masikini
5. Kumbuka kumfanyia hakika mwanao kwani huu ni wajibu wa kila mzazi kwa mwanae
6. Mkumbushe mama kumnyonyesha mtoto wenu kama hana matatizo ya kunyonyesha. Amnyonyeshe mtoto kama ilivyoelezwa kwenye Korani
kuwa mtoto anatakiwa kunyonyeshwa kwa muda usiopungua miaka miwili atamuachisha mapema tu pale ambapo kutakuwa na matatizo
yanayomfanya afanye hivyo.
7. Hakikisha unampa zawadi au pesa mkeo mbali na matumizi kama ahsante ya adha anayopata mkeo kumnyonyesha mwanao kama
ilivyoandikwa kwenye koran.
8. Kama mkeo kajifungua kwa operation jitahidi usijempa ujauzito mwingine angalau baada ya miaka minne.
9. Ni vizuri kutomuingilia mkeo kwa muda walau wa miezi mitatu tangu ajifungue kama kweli unamjali
10. Jiepushe vishawishi kwa kusali na kuomba Mungu huku ukiamini kuwa mkeo ndio mke bora na mzuuri sana kuliko wote duniani kwani ni
kipindi kigumu sana kwako na ndio wakati wanaume wengi wanaiba nje
11. Tumia kondomu kupanga uzazi kuliko vidonge vya vingine kwani vinaweza mfanya mkeo asindwe kucontrol mzunguko wake wa mwezi
12. Kumbuka ukimaliza kazi ofisini ujitahidi kurudi nyumbani mapema kwani hiki ni kipindi ambacho mkeo atakuwa hana amani sana moyoni na ni kipindi ambacho anahitaji kuwa karibu sana na wewe kama kipindi alichokowa mjamzito. Utani wa hapa na pale na kujiepusha lugha za maudhi ni muhimu sana kipindi hiki ili kumfanya apone haraka
13. Kumbuka kusali kabla hamjalala na kushika kichwa mtoto kumuombea dua kabla hamjalala itasaidia mtoto kutolia sana usiku. Waweza chukua udhu kisha somea maji ayatul kursiyu x 7, surat nas, falaq, ikhlas x 3 kila moja alhamdu mara saba mpake haya maji mwilini mwake na mlambishe kidogo vile vile waweza mpaka juice ya vitunguu swaumu kwenye nyayo za miguu kama anasumbua kulia sana usiku
14. Sisitiza usafi kwa mama na mtoto na hasa vyombo anavyotumia mtoto ni vizuri vichemshwe
15. Pempa ni nzuri kutumia lkn mama inabidi awe makini kwani ni chanzo kikubwa cha UTI hivyo bora kutumia nepi kwani pempas kina mama wengi wanajisahau mtoto akikojolea au kujisaidia ni bora nepi au pempa kubadilishwa haraka iwezekanavyo
16. Muanzishie mwanao mafuta ya samaki kwani ni muhimu sana kwake kutengeneza kinga mwilini na kujenga mifupa na kumpatia vit A
17. Mpe dawa za majimaji za maleria walau kila baada ya miezi mitatu dawa hizi waweza zipata pale Natural therapy opposite hindumandal
18.Clinic ni muhimu na ingekuwa bora sana kwenda na mkeo kwani inapendeza zaidi na mkeo atajisikia jinsi unavyojali
19.ukitoka kwenye mizunguko yako kabla ya kumshika mtoto bora uoge kwanza au unawe mikono kwa sabuni kwanza kwani kumbuka ngozi yake bado chango
20. Sali na umshukuru Mungu kwa kukujaliia mtoto muombee mkeo na mtoto pamoja na wewe binafsi afya njema na Muombe mungu awajallie riziki na kuwaepusha na vishawishi, A wajaliie amani na upendo.


Nakuombea kwa Mungu akuzidishie upendo na amfanye mkeo na wewe mwenyewe kuwa wavumilivu. Awajaalie upendo wa dhati amjaliie mwanao awe na tabia njema, amjalie afya njema na awaepushe wewe, mkeo na mtoto na mabalaa yote. Ewe Mwenyeezi mungu ijaliie familia hii riziki na amani mioyoni mwao, Mjalie mama wa mtoto huyu kupona haraka kutokana na maumivu ya kujifungua
A men
 
Kwani kupata mtoto ni big deal, mi kila siku navikataa hivyo vi-kid. Sasa naona kuna umuhimu wa kuanzisha Jukwaa la UJAUZITO NA KUJIFUNGUA. Siyo kila kitu lazima kije hapa, mwisho mtaanza kupost mpaka chakula mnachokula sasa.
Kaonane na daktari wa magonjwa ya akili asap!
 
hongereni na Mwenyezi Mungu awaajalie kwa hali na mali mkalee vizuri....kabinti kangu keko eti!
 
Back
Top Bottom