Ahsante Kikwete - Chuo Kikuu Kingine

Si jambo la kufurahia sana hii misaada tunayo pewa na hawa weupe. tutakuja juta. kila kitu kinacho fanyika utasikia wafadhiri wamechangia. "take care" malipo yake yatakuwa makubwa sana> mimi naona Tanzania ni kama tumeisha laaniwa, unshobokea misaada we uana akili timamu? na kuhusu rais kutoa uhuru wa vyomb avya habari, hii ni seheu ya unafki "akumulikae mchana usiku hukuchima 'mind you. mtakwisha kwa ubwege wenu

Mitumba yao mizuri na unatambia!
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ameendelea kuweka rikodi iliyotukuka katika nyanja ya Elimu na katika kuendeleza kauli mbiu ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania, amefunguwa Rasmi Chuo Kikuu Cha Kwanza Kijeshi Cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Hongera sana Kikwete, mpaka sasa tunaona juhudi zako na hii ni rekodi nyingine adhimu kwako na kwa Taifa.

Kwa hakika Elimu pekee ndio itayompa Maisha Bora kila Mtanzania. Na unafanya kweli!

moja.jpg


Photo source: http://2.bp.blogspot.com/-mgh60RLHe8s/UE4oZ3b2WkI/AAAAAAAABOU/mBTX2Erq-Mc/s1600/moja.jpg


HAPANA, UMERUKA maneno muhimu COLLEGE... SIO UNIVERSITY... ni CHUO sio CHUO KIKUU... kwahiyo KOZI ZAKE sio za

DEGREE...


ndc8916852697.jpg
 
sidhani kama kuna cha kumpongeza
ametimiza wajibu wake tuache unafiki.
hakugombea urais ili aje kusifiwa
yapo mengi aliahidi 70% hajatimiza na miaka inayoyoma
atakaegombea atakuja na sera hizi hizo na kwa ujuha wetu tunamchagua tena tukiota maendeleo

You're damn right mkuu. Yanini asifiwe wakati ni jukumu lake
 
Keep it up mr president unaitendea haki nchi yako..mungu mmbariki kikwete mungu ibariki tanzania
 
Tuanze kuzipa rangi ahadi zilizotekelezwa.


  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa - Nzega, Tabora
  2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda - Tanga mjini
  3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria - Igunga
  4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU) - Shinyanga
  5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini - Dodoma
  6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono - Dodoma mjini
  7. Kuwapatia trekta wakulima - Kata ya Mrijo, Dodoma
  8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi - Kagera
  9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi - Kagera
  10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba - Bukoba Mjini
  11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda - Kagera
  13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme - Kagera
  14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu - Kagera
  15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino - Mbeya
  16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba - Kagera
  17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika - Mwanza
  19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu - Mwanza
  20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani - Geita
  21. Kulinda muungano kwa nguvu zote - Pemba
  22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa - Morogoro
  23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa - Mbeya mjini
  24. Kujenga bandari Kasanga – Rukwa
  25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira - Mbeya
  27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama - Tanga
  28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini - Iringa
  29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani – Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam - Same mkoani Kilimanjaro
  30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same - Same Mjini
  31. Kuboresha barabara Igunga - Tabora
  32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu - Kisesa Magu
  33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya - Mbeya Mjini
  34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN) - Hydom Manyara
  35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa - Musoma
  36. Kulinda haki za walemavu - Makete
  37. Kujenga baabara ya Njombe - Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109 - Iringa mjini
  38. Kujenga barabara Musoma – Mto wa Mbu Arusha - Arusha
  39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  40. Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma – Kaliua,Tabora
  41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi - Arusha Mjini
  42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa, mpaka Singida - Dodoma
  43. Kuwafidia wanakijiji ng'ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009 - Longido
  44. Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria - Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
  46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo - Busekera, Wilaya ya Musoma
  47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido - Longido
  48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri - Mbulu mkoani Manyara
  50. Kusambaza maji nchi nzima - Babati vijijini
  51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015 - Babati vijijini
  52. Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha - Iringa
  53. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika - Iringa
  54. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania - Iringa
  55. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi -Ifunda
  56. Kutokomeza malaria 2015 - Bunda, mkoa wa Mara
  57. Kuwapa wanawake nafasi zaidi - Kilolo, Iringa
  58. Kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii - Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  59. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa - Kibandamaiti mjini Zanzibar
  60. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada - Kibandamaiti
  61. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay - Ruvuma
  62. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400 - Mbambabay Ruvuma
  63. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga (MBICU) – Ruvuma
  64. Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania – Ruvuma
  65. Hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam??????????????!!!!!!!!!!!!!!
  66. Mtwara kuwa mji wa Viwanda – Mtwara
  67. Ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu - Kibaha
  68. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa - Kibaha
  69. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda - Kibaha
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ameendelea kuweka rikodi iliyotukuka katika nyanja ya Elimu na katika kuendeleza kauli mbiu ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania, amefunguwa Rasmi Chuo Kikuu Cha Kwanza Kijeshi Cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Hongera sana Kikwete, mpaka sasa tunaona juhudi zako na hii ni rekodi nyingine adhimu kwako na kwa Taifa.

Kwa hakika Elimu pekee ndio itayompa Maisha Bora kila Mtanzania. Na unafanya kweli!

moja.jpg


Photo source: http://2.bp.blogspot.com/-mgh60RLHe8s/UE4oZ3b2WkI/AAAAAAAABOU/mBTX2Erq-Mc/s1600/moja.jpg

Ni Chuo Cha nini kwanza, Kinatoa Degree Programs zipi na ziko Relevance ki aje na Mahitaj yetu.
kisije kuwa ni Chuo cha Nyuki
 
yale yale ya UDOM,ama kuna kaushauri HALAFU kutoka kwa MCHINA?

Scratch my back I'll scratch yours.

Have you ever thought about many countries offering a lot of scholarships worth billions of dollars year in year out? Think!
 
ni hatua nyingine kubwa na nzuri sana hii kuelekea kuikomboa tanzania kielimu.viva kikwete
 
Huu ni mzaha. Mfumo wa elimu wa Tanzania unahitaji marekebisho makubwa. Tukikimbilia kujisifia kwa kuongeza idadi bila kuangalia suala zima la ubora pamoja na ukidhi wa mahitaji tunajidanganya sana. Ona tunavyopoteza muda wa vijana wtu kwnye sekondari za kata!
Asiye jua maana haambiwi maana.
Hiki si chuo cha kawaida,watu wasio na uelewa si rahisi kuona maana ya chuo hiki.
Nchi zote duniani zinakuwa na strategic thinkers katika masuala ya defence.
Naamini kwa chuo hiki huu ni mwanzo mzuri wa kuhimili maslahi ya nchi kwa kuwa na wahitimu ambao watafuzu strategies za kulinda maslahi ya nchi bila kuweka chumvi ya kiitikadi.
 
Nadhani ingekuwa vizuri kama ungemuuliza Waziri wa Elimu Dr Shukuru Kawambwa ungepata majibu murua, tunachojua JK kajenga chuo kikuu.

Ritz na wewe umekuwa wa aina hii? Unashindwa kujibu hoja unabaki kusema "tunachojua?" Mnachojua wewe na nani ambaye wewe ni msemaji wake? Chuo kimejengwa kwa msaada wa wachina sisi tunakaa kumsifia JK kwa kutimiza wajibu wake? Mtu hasifiwi kwa kufanya kile alichopaswa kufanya, unless amefanya extraordinary thing, hilo ni moja kati ya mengi ya majukumu ya serikali yoyote ile, halihitaji sifa hata kidogo. Kwani kwako ukileta chakula kama baba, watoto wanakusifia? Hilo si jukumu lako? Ptuuuu!!!!
 
we all know, hata JK angefanya zuri gani sio tu kwamba msingelisifia lakini msingelipenda kabasi hata kutokea kwake.
 
Pongezi kwa serikari ya China Bhaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaasi.
 
nadhani ingekuwa vizuri kama ungemuuliza waziri wa elimu dr shukuru kawambwa ungepata majibu murua, tunachojua jk kajenga chuo kikuu.
kwa nini asingekuja kukifungua huyo kawambwa ili atujibie hayo maswali...jk bhana,kupanda ndege yeye,kukata utepe yeye,..sasa bilal atafanya kazi gani?
 
Maisha bora hayawezi kutokana na bora elimu; Elimu bora ndio nguzo ya maisha bora. je elimu yetu ni bora?! tafakari.

Shule hazina madawati, maabara na walimu bora,
walimi hawana nyumba za makazi
walimu waliopo wanalipwa duni wamebaki ombaomba.
mitihani watoto wanapita kwa kununua mitihani.

Je wewe umekuwa praise singer tu au unaangalia vipi hali ya elimu yetu.
 
Back
Top Bottom