Ahsante Kikwete - Chuo Kikuu Kingine

zomba

JF-Expert Member
Nov 27, 2007
17,240
3,910
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ameendelea kuweka rikodi iliyotukuka katika nyanja ya Elimu na katika kuendeleza kauli mbiu ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania, amefunguwa Rasmi Chuo Kikuu Cha Kwanza Kijeshi Cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Hongera sana Kikwete, mpaka sasa tunaona juhudi zako na hii ni rekodi nyingine adhimu kwako na kwa Taifa.

Kwa hakika Elimu pekee ndio itayompa Maisha Bora kila Mtanzania. Na unafanya kweli!

moja.jpg

Photo source: http://2.bp.blogspot.com/-mgh60RLHe8s/UE4oZ3b2WkI/AAAAAAAABOU/mBTX2Erq-Mc/s1600/moja.jpg
 
big up presidaa, umejitahidi.
Binafsi naamini jk anaweza kufanya mengi zaidi, hajaamua tu kufanya.
Naamini hakuna linalo mshinda ila ni uamuzi wake tu unahitajika.
 
Umefurahiii?!!!! Akili yako haiko sawa wewe

sidhani kama umetafakari vya kutosha ulicho andika, hoja hujibiwa kwa hoja na sio matusi wala kejeli.
Mtu Yeyote anapo patia asifiwe na anapo kosea akosolewe.
Siasa sio uadui, hii nchi ni yetu sote, jk akifanya zuri litatunufaisha sote na anapo kosea litatugharimu sote.
 
sidhani kama kuna cha kumpongeza
ametimiza wajibu wake tuache unafiki.
hakugombea urais ili aje kusifiwa
yapo mengi aliahidi 70% hajatimiza na miaka inayoyoma
atakaegombea atakuja na sera hizi hizo na kwa ujuha wetu tunamchagua tena tukiota maendeleo
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, ameendelea kuweka rikodi iliyotukuka katika nyanja ya Elimu na katika kuendeleza kauli mbiu ya Maisha Bora kwa Kila Mtanzania, amefunguwa Rasmi Chuo Kikuu Cha Kwanza Kijeshi Cha Jeshi la Wananchi wa Tanzania.

Hongera sana Kikwete, mpaka sasa tunaona juhudi zako na hii ni rekodi nyingine adhimu kwako na kwa Taifa.

Kwa hakika Elimu pekee ndio itayompa Maisha Bora kila Mtanzania. Na unafanya kweli!

zomba, unaweza kutupa details zaidi kuhusu hicho chuo kikuu kipya cha kijeshi? i.e kiko affiliated, na chuo gani? funding zinatoka ndani au kwa nje, na kama ni nje ni nchi gani? kinajengwa/kimejengwa wapi? na kitachukuwa wananfunzi wangapi? shukrani.
 
Huu ni mzaha. Mfumo wa elimu wa Tanzania unahitaji marekebisho makubwa. Tukikimbilia kujisifia kwa kuongeza idadi bila kuangalia suala zima la ubora pamoja na ukidhi wa mahitaji tunajidanganya sana. Ona tunavyopoteza muda wa vijana wtu kwnye sekondari za kata!
 
Kimejengwa kwa Sh.ngapi na chanzo cha fedha hizo ni nini?
Kitaendeshwa kwa budget ipi?
Kitasomesha watu gani na wangapi kwa mara moja?

Nadhani ingekuwa vizuri kama ungemuuliza Waziri wa Elimu Dr Shukuru Kawambwa ungepata majibu murua, tunachojua JK kajenga chuo kikuu.
 
huku unaongeza idadi ya vyuo, huku unapunguza mikopo ya elimu. Hivi unajua mwaka huu kuna maelfu ya wanafunzi hawataweza kujiungana vyuo vikuu kwa kushindwa kujilipia ada?
NB: angalia vigezo vya kupata mkopo 2012/13
 
big up presidaa, umejitahidi.
Binafsi naamini jk anaweza kufanya mengi zaidi, hajaamua tu kufanya.
Naamini hakuna linalo mshinda ila ni uamuzi wake tu unahitajika.
Anasubiri aage dunia ndio aamue, muda wake unaisha, tunamkumbusha, zile meli nyasa, victoria na tanganyika, na kigoma bado haijawa dubai na.....du ukianza kutaja zile ahadi unapata degedege kwa jinsi zilivyo changa la macho. Hongera presidaa kwa kutupiga kipapai
 
zomba, unaweza kutupa details zaidi kuhusu hicho chuo kikuu kipya cha kijeshi? i.e kiko affiliated, na chuo gani? funding zinatoka ndani au kwa nje, na kama ni nje ni nchi gani? kinajengwa/kimejengwa wapi? na kitachukuwa wananfunzi wangapi? shukrani.
Zomba hana uwezo au uelewa wa kuweza kujibu haya maswali. Yeye anaposikia chuo kikuu cha kijeshi, mawazo yanamtuma kwamba ni Military University. Kumbe hajui kwamba tuna hata chuo kikuu cha polisi kurasini na chuo kikuu cha magereza ukonga. Hapa haina maana kwamba ni universities, bali katika mafunzo yao ya kijeshi vyuo hivyo ndiyo vinatoa mafunzo advanced. Haina maana ukitoka hapo unakuwa na digrii au diploma ya kijeshi, ya polisi au ya magereza.
 
Back
Top Bottom