Mzalendo JR
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 1,193
- 515
Jokakuu.
Ninachosema ni ukweli usiopingika na nimekiona kwa macho yangu na kukifanyia kazi kubwa. Wewe jaribu tu kuangalia
1.kwanza kabisa Bunge la Katiba ya muungano ambalo wakti huo walikuwa ni kamati kuu ya chama tawaala Znz na Tanganyika. Wajumbe 20 kila upande. Tafuta majina yao upande wa Tanganyika. Jiulize ilihitajika shule kiasi gani hapo kupitisha katiba hiyo?
2.Hata Katiba yenu ya 77 wajumbe wake. Angalia wajumbe kuto ka Tanganyika? jiulize ilihitajika shule kiasi gani hapo kupitisha katiba hiyo?
Mimi nilifanya kazi wizara ya fedha mara baada kumaliza UDSM. Nakumbuka wakti wetu katika wakuu wa idara wakti ule 14 za wizara hiyo waislam tulikuwa 6 tu na 4 kati yao tulikuwa tunatoka Znz.Na sisi tuliletwa ingawa tulikuwa wote ni graduates 2 wetu wakiwa ma shahada za uzamili lakin lengo kuu ilikuwa nikuzidi kuimarisha muungano kwa Tanganyika
Suala la UDINI kwa bara ni suala la urithi toka kwa wakoloni ambao walitumia njia hii kuweza kuwatawala kama walivyotumia ukabila huko kenya na Uganda.
Suala hili lilizimwa na Muungano wenu na Znz. Lakin sasa naona kuna kila dalili za kuibuka tena haswa baada wa watunza siri akina Mtei kuanza kuliibua na kuliweka hadharani.
Mimi nimestahajabu kusikia BAKWATA ambacho ni chombo maalum cha Serikali kilichoundwa kuwadhibiti waislam kimeungana na Jumuiya nyingine za Kiraia kudai haki zao kielimu na hata katika mustakabali wa zoezi la Sensa.
Tukumbuke kuwa historia siku zote haifichiki na inajirudia kila mara. Na hakuna dhulma yenye kudumu.
Jaribu kukumbuka wakati ule wewe unabahatika kusoma kwa msukumo wa wazazi wako ni majirani wangapi wa kiislamu walikua wakiwaamsha watoto wao kwenda MADRASA kukariri kurani na sio kwenda darasani? Kubali ukweli kua wakati ule na hata sasa waislamu huona fahari mtoto kujua dini kuliko elimu dunia.
Hapo utapata jibu kua waislamu wakati ule na hata sasa muamko wa elimu no mdogo mno, sasa tukupe wizara na elimu ya Madrasa?