Ahadi ni deni...CCM imetekeleza ilani yake ya uchaguzi

security guard

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
799
603
Chama cha mapinduzi kwa kiasi kikubwa kabisa kimetekeleza ilani zake na sasa kinapita kwa kila mwananchi kumueleza yale yaliotekelezeka na kukamilika na yalio karibu kukamilika.

Usikose kusikiliza mkutano wa CCM Kigoma leo ITV saa moja jioni.

Ukweli ndio huu...AHADI NI DENI (A.N.D)
 
bila shaka itakuwa ile ahadi ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA,
KUNUNUA MELI MPYA ZIWA VICTORIA NA ZIWA NYASA,
NA KUPUNGUZA MFUMUKO WA BEI
 
dah kweli kabisa naona wa tz sasa ni mwendo wa bata kwa mrija kwa sababu ahadi ya maisha boro imetimia teh teh teh teh teh
 
Kweli kabisa na mfumuko wa bei kwa sasa ni 0.0000000000001
Na wananchi wote wanaishi maisha bora na usafiri wa uhakika na chakula cha kutosha. Miundo mbinu iko juu asilimia 99.9
Mishahara ya wafanyakazi wote iko juu hakuna mwenye shida
Hakuna migomo tanzania ya sijui wanafunzi mara madoctor mara walimu mara waendesha mikokoteni
Wanafunzi wanapata mikopo asilimia 99.9 ya kuwawezesha kusoma kwa furaha na madarasa na mabweni yao yana kila kitu kuwawezesha kusoma
Wahadhiri wa vyuo wanalipwa vizuri sana
Ahhhh kweli ahadi ni deni
 
bila shaka itakuwa ile ahadi ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA,
KUNUNUA MELI MPYA ZIWA VICTORIA NA ZIWA NYASA,
NA KUPUNGUZA MFUMUKO WA BEI
Kununua meli ziwa Nyasa wakati wamalawi wanadai ziwa ni lao!
 
bila shaka itakuwa ile ahadi ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA,
KUNUNUA MELI MPYA ZIWA VICTORIA NA ZIWA NYASA,
NA KUPUNGUZA MFUMUKO WA BEI

Nakumbuka JK wakati anazindua bunge mwaka 2005 alisema "...nitapambana na rushwa, hasa zile rushwa nene-nene..."
 
Chama cha mapinduzi kwa kiasi kikubwa kabisa kimetekeleza ilani zake na sasa kinapita kwa kila mwananchi kumueleza yale yaliotekelezeka na kukamilika na yalio karibu kukamilika.

Usikose kusikiliza mkutano wa CCM Kigoma leo ITV saa moja jioni.

Ukweli ndio huu...AHADI NI DENI (A.N.D)
Ni kweli Mkuu ahadi zote imezitimiza mpaka nyingine ambazo haikuahidi majukwaani kama ya kupeleka watetea haki mabwepande ambayo utekelezwaji wake kwa sasa ni asilimia 100
 
Hata ile ahadi ya kupeleka vyombo vya uchunguzi anga za juu imefikia asilimia 99.9:flypig:
 
hawashindwi kitu ccm wametimiza ahadi na ilani yao,ulimboka kimya,madaktari kimya walimu nao wataufyata,basi ikiwepo mahakama na msitu wa mabwepande ccm inatekeleza ahadi zake mia kwa mia.
 
Njia iliyo bora kwa serikali sikivu ni kujadili na kuamua kwa pamoja kati yake na wananchi wake. Mipango inayotekelezeka ni ile inayopangwa na wananchi wenyewe wakishirikiana na watendaji wao wa serikalini. Naamini katika Kijani na hivyo ndivyo ilivyo...!
 
Kweli kabisa na mfumuko wa bei kwa sasa ni 0.0000000000001
Na wananchi wote wanaishi maisha bora na usafiri wa uhakika na chakula cha kutosha. Miundo mbinu iko juu asilimia 99.9
Mishahara ya wafanyakazi wote iko juu hakuna mwenye shida
Hakuna migomo tanzania ya sijui wanafunzi mara madoctor mara walimu mara waendesha mikokoteni
Wanafunzi wanapata mikopo asilimia 99.9 ya kuwawezesha kusoma kwa furaha na madarasa na mabweni yao yana kila kitu kuwawezesha kusoma
Wahadhiri wa vyuo wanalipwa vizuri sana
Ahhhh kweli ahadi ni deni
Hahahahah kusema kweli nimeipenda hiyo M. uko juu
 
Baada ya kukosa wahudhuriaji ktk mikutano ya ccm,wameamua kununua vipindi itv kudanganya umma kwa miradi ya ufadhili uliosimamiwa na wazungu
 
Ni kweli mkuu, naona ahadi zimetimia kwa 98%, safi sana!!!!! Ila ile kauli yenu ya ARI ZAIDI, KASI ZAIDI NA NGUVU ZAIDI siku hizi hamuisemi kabisa, hata Baba Ritz naye yuko kimya kabisa!!!!
 
bila shaka itakuwa ile ahadi ya MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA,
KUNUNUA MELI MPYA ZIWA VICTORIA NA ZIWA NYASA,
NA KUPUNGUZA MFUMUKO WA BEI

Zile machinga complex sita zipo tayari zinangojea kukabidhiwa tu na tayari kigoma tushaigeuza kama dubai.wajinga ndiyo waliwao ha ha ha ha ha ha
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom