Ah! I hate suprises!

PetCash

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
1,997
1,997
Habari zenu wanajamvi,

Leo mchumba wangu wangu amenifanyia suprise ambayo nimejuta kumfahamu!
Mchumba wangu (yuleyule tuliyekuwa na problem naye back then-sasa hivi mambo supa)
ni graduate wa herpetology from JcU Australia.Na mojawapo ya matatizo ya relationship yetu yalikuwa ni research zake!
Huwa anawapenda sana vyura na reptiles(na ndicho alichosoma), sasa ana collection ya hao wanyama at her parent's house
ya kutosha! Alhamisi alisafiri na rafiki zake(wametoka Australia) kwenda Arusha park moja inaitwa tarangire.

Akiwa safarini kila mara tukiwasiliana ananiambia ataleta something.Mimi namjua so nikawa namwambia usilete.
Leo asubuhi kanitembelea kunifanyia surprise(sikujua kwamba kesharudi dar), akakaribishwa, akasneak
mpaka chumbani(mimi nimelala sijielewi).Then akaniamsha akajificha. Naamka tu! kuna nyoka on my bed!
Nimepiga ukelele mpaka nyumba ya 3 wamesikia na isingekuwa mvua mtaa mzima ungesikia!

Yani hapa nina hasira! hata kazi nimeshindwa kufanya niko zangu Jf. I hate frogs, lakini nyoka!
Kweli I hate surprises ever!

Nnavyoenda naona kabisa kabisa huu uhusiano utanishinda, leo ningevunjika miguu kwa kupiga acrobatic jumps-kisha naambiwa kanyoka kenyewe kadogo!
 
Hahahahahaha haaaaaaaaaa, dah nimecheka mpaka ofisini wamebaki wananishangaa nacheka na kompyuta..ebana mwana pole sana hiyo suprise kweli kiboko....
 
Wewe una visa, yaani hicho kitu tu unaanza kuwaza kama mtaweza ishi pamoja!
 
hahaahaaaaa nimecheka haswaaa........

Mpende jinsi alivyo, unajua mpenzi wako ana udhaifu na nyoka, mkubali the way she is.........
 
Hiyo nayo ni suprise...!
Hiyo ni sawa na zamani mtoto akikataa kula au kunywa dawa unamtafutia kitu cha ajabu kumtisha..........hususan vitu anavyoogopa........... sasa wewe rafiki yangu PetCash huyo anakutisha baada ya kutomtimizia shida yake fulani..........hiyo ni mbinu kama ile ya kumtisha mtoto................LOL

Kaka siku nyingine suprise itakuwa konokono................................
 
suprise ya aina hiyo,na mimi yangenishinda.hakuna kitu ninachokiogopa kama nyoka.
 
Hizi sapraizi zenu mtaja kuta mamba mivunguni, khaa!

Anywayz, wanasema ukipenda boga, penda na ua lake, jianzie na wewe shosti biashara ya kukusanya ma-nyoka kama pets. Ndiyoo, ufanyeje sasa?
 
M2 wng, plz plz plz mna mipango mizuri, mnapendana sioni haja ya kuachana kwa 7bu hyo tu!Cha msing jtahid ukae nae umweleze kinagaubaga abt suala la surprise!2mia busara atakwelewa,2mia hata rafik zko + rafki zke especialy during Dinner smhwea!
 
hahaha..huyo mchumba ni dume au jike?kama ni jike akikushnda nifanye mpango mimi napenda sana suprise..
 
Kaunga na Husninyo ombeni yasiwakute! Kidume nimekomaje? yani nimeulizwa kelele za nini sina jibu. Nnaona aibu hata kurudi nyumbani sina hamu! ah!
Hivi tukioana na makabrasha yake akahamishia kwetu si nitakimbia nyumba mimi? wewe utaweza kunitembelea ukijua hivyo?
Wewe una visa, yaani hicho kitu tu unaanza kuwaza kama mtaweza ishi pamoja!

umeona eeh!
 
Last edited by a moderator:
Kaunga na Husninyo ombeni yasiwakute! Kidume nimekomaje? yani nimeulizwa kelele za nini sina jibu. Nnaona aibu hata kurudi nyumbani sina hamu! ah!
Hivi tukioana na makabrasha yake akahamishia kwetu si nitakimbia nyumba mimi? wewe utaweza kunitembelea ukijua hivyo?

Uoga tu, dume zima. Ila if it will make you happy; kaka yangu mimi akiona mende anapanda juu ya vitu. So you are not alone. Mkioana kutakuwa na chumba maalumu ambapo ataweka hizo sample zake ambacho wewe hautaingia; simple!
 
Pole yamekukuta, kwani haujui kuwa ni muhimu kuonyesha interest kwenye vitu ambavyo anavipenda mpenzi wako maana hao reptiles wanaweza kuwa pets katika nyumba yako. Anza kujenga mapenzi toka sasa!
 
M2 wng, plz plz plz mna mipango mizuri, mnapendana sioni haja ya kuachana kwa 7bu hyo tu!Cha msing jtahid ukae nae umweleze kinagaubaga abt suala la surprise!2mia busara atakwelewa,2mia hata rafik zko + rafki zke especialy during Dinner smhwea!

Mkuu, namuelezaje aache na hiyo ndo carrier yake? kweli mi nimejitahidi lakini it just doesn't work out well between me and snakes. Ananipa habari za; ukipambana na mamba ukimbana mdomo hana ujanja-habari za kupambana na mamba mi naanza anzaje? Siku akitaka mimi niwe hero wake si ndio atanipeleka ziwani nimkamatie mamba?
 
Sitaki hata kusikia akiwataja jina!
Pole yamekukuta, kwani haujui kuwa ni muhimu kuonyesha interest kwenye vitu ambavyo anavipenda mpenzi wako maana hao reptiles wanaweza kuwa pets katika nyumba yako. Anza kujenga mapenzi toka sasa!
 
Kwenye kula Tunda si ataishia kunawa tu?????? kama sio hata Maji ya kunawa hatapewa
 
Back
Top Bottom