Agosti 31 ya JK: Baraza la EID huko Dodoma kutumika kurusha makombora, usikose!

DONDOO MUHIMU: E.L anadaiwa kusaini MOU akiwa PM katika mpango wa kusaidia Kanisa na pia kuwasomesha wakristo nafasi ambayo waislamu pia wanataka wapewe fursa kama hiyo kuweza kusaini Memorandum of Understanding ili kuwapa fursa sawa za kumiliki Miradi na pia kuendelezwa kielimu

Alisaini akiwa waziri mwaka 1992 na sio PM
 
Kama kwaida JK alikuwepo ulitegemea nini???Mwamvuli wa udini utatumaliza muda si mrefu..
 
BAKWATA leo kupitia risala iliyosomwa na katibu wa BAKWATA ktk baraza la idd imekumbushia hoja na madai yao kwa JK ikiwamo kujiunga na oic :kadhi na nk
 
JK: Serikali inapaswa kuwa na mahusiano na wajibu wake kuhakikisha kuwa inashirikiana na taasisi zote za dini bila ubaguzi na kwamba hayasemi hayo kwa kuwapaka mafuta kwa mgongo wa Chupa bali ni ukweli ulio wazi kuwa serikali inayathamini mashirika haya ya Dini kutokana na mchango wake kwa huduma muhimu za kijamii kwa watanzania.

Anasisitiza kuwa hakuna kitu chochote ambacho itatoa kwa Dini yoyote na Dini nyingine ikanyimwa.

Kama hujaomba usiumlaumu aliyepewa na wala usimkukumu aliyetoa

Na kama mmefanya hivyo na hamjapewa mwashitaki kwa mamlaka husika ananzungumzia Itifaki ya mwaka 2002

Anasema maobi ya BAKWATA pia yatashughulikiwa
 
Wanaelezea yafuatayo:

1. Ugawaji sawa wa kuchumi: Hapa msoma risala analalamikia serikali kuwawezesha wakristo pekee yao kupitia MOU

2. ANASEMA UCHAGUZI ULIOPITA ULITAWALIWA NA UDINI, hivyo tuepuke udini

3. Anasema serikali imewarudishia wakristo baadhi ya shule ilizotaifisha (hazitaji) hivyo waislam warudishiwe zao (hazitaji)

4. Mahakama ya kadhi,.anataka serikali waongeze kasi kuanzisha mahakama hiyo

5. Muswada wa sheria ya ndoa usikinzane na maandiko ya kiislam

Mufti anazungumzia matendo mema baada ya mwezi wa ramadhani,..anaongelea sana wizi wa wake za watujk anajibu vizuri hoja zaokuhusu MOU anawaambia nao waombe sio kusema wenzao wanyimwe
 
Anatoa pia Mkono wa EID kwa Watanzania na wakazi wa DODOMA kama mkoa mwenyeji
mkuu tafadhali naomba utoe hizo ahadi za jk kwenye post ya juu ....zinatukwaza kidogo kwenye ku scroll !! utaziweka baadaye mambo yakitulia! ni ombi tu!
 
Mkuu Edson uansikia anajibu makombora kama yalivyo sasa TUNASUBIRI PALE KWA MADAWA YA KULEVYA Sijui anatasema nini
 
GR nasikia ngoja tusubiri kwenye madawa ya kulevya.......ila watachukia sana amewaambia huwa hawaombi ila wanalia lia na kulalamika..
 
Anaelezea mambo ya kuhiji Makka. Nadhani anajaribu kupoteza muda ili asiongelee siasa na matatizo.
 
hii hotuba ni ya mwezi na kwa taifa? au anajibu hoja za bakwata?....GR nisaidie
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom