Agosti 31 ya JK: Baraza la EID huko Dodoma kutumika kurusha makombora, usikose!

SHULE ZILIZOTAIFISHWA BAADA YA UHURU

Waislamu wanaomba shule zao zote zilizotaifishwa baada ya Uhuru zilijeshwe kwao waweze kuziendesha wenyewe kwa kuwa wana nia na uwezo wa kufanya hivyo kwa sasa

MSWAADA WA MAREKEBISHO YA SHERIA YA NDOA NA MIRATHI
Waislam hawategemei kama mswaada huo utapingana na maelekezo ya dini yao katika taratibu za mirathi na wanaomba washirikishwe katika hilo kwa kuwa nao wana taratibu za dini zinazotoa muongozo kuhusu suala zima la Mirathi na NDOA

BEI ZA VYAKULA
Anaipongeza serikali katika kushughulikia na kusimamia vema bei za vyakula wakati wa mwezi mtukufu wa ramadhani

anatoa mkono wa EID

KATIBU MKUU BAKWATA

Suleima LUWINGA
jamaa akili yao ni ya kujitengatenga tu...sasa hizo shule zilizotaifishwa wenye kuzijua watutajie. Na wakristu nao wakidai shule zao zilizotaifishwa hali itakuwaje?mmmh ndugu zetu hawa.! Ngoja tumsikilize JK naye atakuja na upupu gani!
 
Mkuu Ghost Ryder, yule mwenyekiti wa h/mashauri ya bakwata kagusia MoU iliyosainiwa baina ya serikali na madhehebu ya kikristu mwaka 1992, katika hilo kaomba serikali ifanye hima pia kwa waislamu. Sijaona umepost wapi ili jamvi liende sawia.
 
DONDOO MUHIMU: E.L anadaiwa kusaini MOU akiwa PM katika mpango wa kusaidia Kanisa na pia kuwasomesha wakristo nafasi ambayo waislamu pia wanataka wapewe fursa kama hiyo kuweza kusaini Memorandum of Understanding ili kuwapa fursa sawa za kumiliki Miradi na pia kuendelezwa kielimu
 
Udini udini udini asipoangalia kwa makini kutakuwa na mgogoro mkubwa wa madhehebu hapa nchini!
 
Mkuu Ghost Ryder, yule mwenyekiti wa h/mashauri ya bakwata kagusia MoU iliyosainiwa baina ya serikali na madhehebu ya kikristu mwaka 1992, katika hilo kaomba serikali ifanye hima pia kwa waislamu. Sijaona umepost wapi ili jamvi liende sawia.

NOTED: Nakimbizana na wazungumzaji lakini pia nikiapata fursa kama hii ya Mufti anapotoa mawaidha tutaziweka Data sawa...Machine zinarekodi pia
 
Mufti ni kama anachekesha huku nyundo ndogo ndogo zikiendelea kutembea kwa chini...anakemea udini, uchu wa mali, uroho wa madaraka na tamaa ya Ngono...Maneno haya yanareflection kubwa kwa tabia za viongozi wetu kwa reflection yangu.

Mufti anahitimisha na tusikie sasa JK alivyotegwa
 
Mufti katoa hii kauli leo katika sherehe za Eid Dodoma "msiwe wapuuzi wa kutenda mema alafu baadae mnayakanyaga kanyaga na kuyatia masizi" mbele ya JK. Naamini JK kamsikia.
 
kikwete atapndisha hawezi kusema juu ya madongo yale........hotuba yake haina hayo madai labda atoe kichwani mwake
 
Anatoa pia Mkono wa EID kwa Watanzania na wakazi wa DODOMA kama mkoa mwenyeji
 
ngoja tupo kwenye msikiti wa Ghadafi ndio hivyo tunamkumbuka na kumuaga kutoka kwake madarakani
 
kikwete atapndisha hawezi kusema juu ya madongo yale........hotuba yake haina hayo madai labda atoe kichwani mwake

Anapaswa kuwa Makini Mkuu maana alivyotegwa ndo hekima inatakiwa kufanya kazi yake
 
Anaaanza na mawaidha kidogo akirejea na kunukuu dodosa muhimu kuhusu maadili kwa waumini wa dini ya Kiislam
 
<font size="4"><b>...........................Nachosubiria ni kauli kama hizi; Kumeanza kuonekana chokochoko za udini kwa Taifa letu....Naomba tuheshimu utawala wa katiba,wananchi wamekikubali CCM wamekipa dhamana ya kuongoza....na si vinginevyo...(Hapa atakuwa anaogopa jinamizi lililowakuta akina Gaddafi na wenzake) Lazima Gaddafi atajwe kwasababu ni rafiki yake mkubwa...

Kama ameswalia msikiti wa gaddafi dodoma kuna nini tena..
 
nimeyasikia na kuyaelewa.........hilo ndilo jibu la madai yote
 
Mkuu Ghost Ryder, yule mwenyekiti wa h/mashauri ya bakwata kagusia MoU iliyosainiwa baina ya serikali na madhehebu ya kikristu mwaka 1992, katika hilo kaomba serikali ifanye hima pia kwa waislamu. Sijaona umepost wapi ili jamvi liende sawia.
yaani yale mambo yote yaliyo kwenye cd/mihadhara ya kichochezi leo yanatolewa kwenye baraza la eid! This is cantankerous!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom