Agosti 31 ya JK: Baraza la EID huko Dodoma kutumika kurusha makombora, usikose!

hii hotuba ni ya mwezi na kwa taifa? au anajibu hoja za bakwata?....GR nisaidie

Mkuu Eddy hapa lengo lilikuwa kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja, lakini Hotuba ilikuwa ya Baraza la Maulidi kitaifa kutoka Masjid Gadaffi DODOMA. Kimsingi kajibu hoja nyingi kifundi na kwa ujasiri, sasa sijui huwa anakuwa wapi Mkuu kushughulikia matatizo mengine kama alivyovaa uso wa mbuzi leo kwa kutegua mitego ile ambayo kama angekosea alikuwa anazua balaa jipya.

Ila kama alivyotahadharisha MEDIA kesho zitamnukuu vibaya tu hili sina shaka, sitoshangaa kukutana na headline kama:

KIKWETE AWAKOROMEA BAKWATA....
JK AWARUKA VIONGOZI WA DINI...Sakata la Udini Nchni
JK AGEUKA MBOGO Sakata la Udini
JK ALIA NA VIONGOZI WA DINI KUHUSU MADAWA YA KULEVYA

na vingine vingi vya kuchefua roho.
 
Ameongea mambo rahisi rahisi sana.
Sijaona jambo la msingi lnalohusu taifa la tanzania na umma wake alilozungumzia.
Ni ukweli kwamba amejibu bila utata sana hoja za risala ya katibu wa BAKWATA, of which alitegemewa kujibu. Sina tatizo nalo hilo. Amejitahidi.
Sitaki kuamini kwamba hii ndo hotuba ya raisi ya mwisho wa miezi mitano kwa taifa. Hotuba hii ni hotuba nyepesi katika kipindi kigumu kwa taifa, kipindi ambacho serikali imeshindwa kudhibiti hata bei ya sukari.

Si Hotuba zake za Mwezi Hii ilikuwa maalum kwa Baraza la Maulid Mkuu Briggy usichanganye mambo. Alitarajiwa kuuwa ndege wawili kwa jiwe moja. Kimsingi kafanya jambo jema kujibu zile hoja angeziacha hivi hivi ilikuwa kadhia kubwa, lakini pia sina hakika sana kama alikusudia kushughulika na Hoja hizo katika muda wake wote wa Hotuba hiyo au circumstances pushes him to get hocked
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom