Agizo la SUMATRA kwa wenye mashule

M-bongotz

JF-Expert Member
Jan 7, 2010
1,734
405
Ni leo ndio kwa mara ya kwanza nimeona hili agizo la SUMATRA kwa wamiliki wote wa mashule wanaotoa huduma ya usafiri kwa wanafunzi wao, eti wanataka mabasi yote ya wanafunzi yapakwe rangi za njano, nimetafakari sana baada ya kuona/kusikia agizo hili.,nahisi huu ni mradi mwingine wa wakubwa, sitoshangaa kusikia kuna garage maalum zimeandaliwa kwa ajili ya kufanya zoezi hili, sioni tofauti na ule mradi wa suti za makonda na madereva wa daladala na miradi mingine iliyojaa mizengwe kama ile ya kupiga mstari kwenye daladala nk.,yawezekana kuna kigogo ana makopo yake ya rangi ambayo karibu yanaexpire na ameshindwa kuyauza sasa wanatafuta soko kwa nguvu.
Nawaza itakuwa vipi kwa yale mashule ambayo hayamiliki mabasi yao yenyewe bali yanakodi mabasi kama daladala nk kwa ajili ya kubebea wanafunzi wao, nini itakuwa hatima yao hawa?.,ina maana watataka na hizo daladala ziwe za njano?.,najua watu wa Majembe Auction Mart na Trafick wanachekelea tu kwani ulaji mwingine unakuja.,nahisi kuna sakata linakuja kati ya SUMATRA na baadhi ya mashule.,yangu macho!!!
 
Na hiyo rangi ya njano imechaguliwa kwa kuwa?

Au ndio yale ya kutaka kufanana na Marekani?
 
Back
Top Bottom