Agizo la Kikwete kwa Tanesco laiva

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,792
287,994
Agizo la Kikwete kwa Tanesco laiva
Faraja Mgwabati
HabariLeo; Thursday,December 27, 2007 @00:02

MUSWADA ambao utaondoa ukiritimba wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) katika kutoa huduma ya umeme nchini na kutoa ruhusa kwa kampuni binafsi kutoa huduma hiyo, umekamilika na unatarajiwa kuwasilishwa kwenye kikao cha Bunge lijalo.

Endapo muswada huo utapitishwa na Bunge na kufanywa sheria, kampuni binafsi zitaweza kuzalisha na kusambaza umeme zenyewe bila kuiuzia Tanesco kama ilivyo sasa; kitu ambacho wataalamu wamesema kitapunguza bei ya nishati hiyo muhimu. Akijibu maswali ya waandishi wa habari baada ya kutimiza miaka miwili madarakani, Ijumaa iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alielezea nia ya serikali kubadili sheria inayoipa nguvu Tanesco ya kuhodhi mamlaka ya kutoa huduma hiyo.

Akizungumza na HabariLeo jana, Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi, alisema maandalizi ya muswada huo yamekamilika na kilichobaki ni kuupeleka bungeni kwenye kikao kinachotarajiwa kuanza Januari 29, mwakani. Karamagi alisema endapo muswada huo utapitishwa na kisha sheria kuundwa, kampuni binafsi zitaisaidia Tanesco katika kutoa huduma ya umeme ambayo yanakua kila siku.

Alisema pamoja na Tanesco kufanyia ukarabati mitambo ya kusambaza umeme waliyonayo, haitaweza kukidhi mahitaji, hivyo kuibuka kwa kampuni nyingine kutasaidia kutoa huduma nzuri. “Unajua ni asilimia 10 tu ya Watanzania ndiyo wanapata umeme, kwa hiyo mahitaji ya umeme bado ni makubwa,” alisema Karamagi alipoulizwa kama kuingia kwa kampuni binafsi hakutawanyang’anya wateja Tanesco.

Kuhusu kama hatua hiyo itasaidia kupunguza bei ya umeme, Karamagi alisema bei itapungua kwa sababu Mamlaka ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), itadhibiti huduma hiyo kwa muda hadi hapo ushindani utakapokuwa wa halali kati ya kampuni zitakazokuwapo.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Artumas, ambayo hujihusisha na utafutaji wa mafuta na gesi nchini, Salvator Ntomola, alisema hatua hiyo ni nzuri kwa sababu itawapa unafuu wa bei wananchi kutokana na kuwapo kwa ushindani katika huduma hiyo muhimu. Ntomola alisema kwa sababu wazalishaji na wasambazaji watakuwa wengi, kutakuwa na ushindani kama ilivyotokea kwenye kampuni za simu za mikononi, ambapo kuingia kwa kampuni binafsi kumeboresha huduma na bei ukilinganisha kabla ya hapo.

“Tukiwa wengi ndiyo vizuri, Ewura itafanya kazi vizuri ya kudhibiti bei na utoaji wa huduma,” alisema Ntomola. Aliungana na Waziri Karamagi kwamba Tanesco haitaathirika endapo kampuni nyingine zitaingia kwenye biashara hiyo, akisema Tanesco imeshajijenga na ina miundombinu mingi kuliko kampuni binafsi.

“Tanesco bado itakuwa na nafasi ya kufanya vizuri kama ilivyo kwenye kampuni za simu, TTCL ina advantage (unafuu) kuliko kampuni nyingine za simu za mkononi,” alisema. Hatua ya kuruhusu soko huria kwenye umeme inakuja wakati ambao Tanesco imeiomba Ewura kupandisha gharama za umeme kwa asilimia 40 ili kukidhi mahitaji ya kifedha kwa ajili ya kumudu gharama za uendeshaji.

Copyright @TSN 2006 All Rights Reserved
 
hapa sijapaelewa vizuri,je watafanya kama wanavyofanya ulaya au ndio kibongobongo kila kampuni na mitambo yake ?
 
Hapa Bongo itakuwa full kujiachia!!! Generate, transmit and distribute to end user customers
 
Katibu Tarafa kwani Ulaya wanafanyaje?Sisi tusiofika huko angalau tupate fununu ya mambo huko.Lakini ninavyosikia ni kwamba Kampuni binafsi zinatoa huduma lakini njia/line zinakuwa za kampuni mama.Hii sio kwa umeme bali ata simu.Kwa mfano nchini Australia kampuni mama ya simu ni Testra,lakini kampuni nyingine kama Optus na vodafone zimenunua njia za mawasiliano.
Raha ya hii moja wapo ni kuwa italeta ushindani wa kibiashara kama ilivyo ktk kampuni ya simu.Lakini kama wafanyabiashara wakicollude nakuamua bei kuwa pamoja na tofauti ni ndogo haita kuwa na maana kubwa kwa wananchi.Kwa mfano ununuzi wa mazao hapa kwetu Tanzania tunategemea kuwa ktk ushindani lakini badala yake wafanyabiashara wanakaa pamoja na tofauti ya bei za kununua huwa ni ndogo.
Kwa watu wa mjini kama kawaida ndio wataanza kufaidika,ni baada ya muda kidogo ndipo watu waishio mbali ya miji wategemee neema hiyo kwa wale wa vijijini sijui hii biashara holela itawafika vipi ya umeme ikiwa makampuni ya biashara yanaangalia uwezo wa kupata faida.Au mtu mmoja mwenye pesa yake aweze kufanya hivyo itakuwa Bomba.Nasikia ilipata kutokea pale Ndanda Masasi na Peramiho Songea ambako kuna umeme muda wote wa nguvu za maji ambao unatumika mission tu na wazungu wa misheni walitaka kuwapa wananchi wa maeneo yanayowazunguka huduma ya umeme kwa sharti la kuchangia gharama kidogo lakini TANESCO ikaja juu nakudai asilimia nyingi za pesa jambo ambalo wazungu hawakukubaliana nalo na hivyo kusitisha huduma kwa wananchi.
Ukiritimba wa namna hii utaondoka.
 
Tatizo liko kwenye uchafuzi wa mazingira. Kama ilivyo kwa minara ya Tigo,Celtel, Voda sijui na madudu gani mengi, tujiandae kuona transifoma za Songas,Richmond,Tanesco, Artumas. Sijui kama kutakalika. By the way, madeni ya IPTL,Richmond na Songas yaliyosainiwa na serikali kwa niaba ya Tanesco yatabebwa na nani? kwa sababu nahisi hii spidi ya kuingia mikataba ya kishenzi huenda ilifanywa kwa makusudi ili kuandaa kitanzi kwa Tanesco ili kesho ishindwe kushindana na kuishia kupigwa mnada kwa bei ya karanga.
 
Sasa mimi kwa muda mrefu kidogo ambao nimeishi ughaibuni nimegundua kwamba wazungu wanakuwa na regulator mmoja aitwae ofgem ambae ndie anasimamia biashara na bei ya bidhaa hizo ya ugavi wa iwe umeme au gesi na kuhakikisha kuna fair competition baina ya s"uppliers". Na energywatch ambao wanasaidia kutoa taarifa kwa wateja kuhusu usalama wa bidhaa hizo na kama mteja anataka kubadilisha "suppliers"

Kuna vituo karibu 2000 vya kuzalisha nishati UK!. Vituo hivi vinaendeshwa kwa gesi, makaa ya mawe na nyuklia.

Kuna makampuni mengi tu ya kuzalisha na kuuza nishati lakini kuna kampuni kubwa sita -British gas,E.ON Npower, EDF Energy na mengine ya Scotland. Kampuni hizi kwa pamoja zinahodhi asilimia 99 ya soko la nishati katika UK.

Ila hakuna kampuni kama Tanesco ambayo ndio mwenye "monopoly" na uzalishaji na uuzaji wa umeme.

Kuna kampuni zinazalisha na kugawa umeme tu na zingine ni gesi tu (gesi ndio inatumika kupikia na kutoa joto majumbani na sehemu zingine).

Kuna kampuni ambazo zinazalisha na kuuza vyote umeme na gesi.

Nikitoa mfano, mdogo wa kampuni ya E.ON ambayo inazalisha umeme wa kama megawati 400 hivi, wao wanafeed kwenye "national grid" ya UK na hupeleka ankara zake kwa kampuni mama ya Powergen ambayo ndio hukuletea "bill" yake kila baada ya miezi mitatu au kila mwezi.

Kwa hiyo bila kusema sana ni kwamba serikali ya UK imeweka au iliweka tokea enzi hizo soko la bidhaa hizi na kuunda "regulators" pamoja na watu waliosomea mambo hayo kwa hiyo ndio tunaona ulaya umeme haukatiki!

Halafu pia kuna wazalishaji wadogo kama wakulima ambao huuza umeme kwa mfano eneo la kimara tu kwa bei nafuu ule umeme utokanao na kinyesi au hata nyasi tu na takataka!

Kwa hiyo serikali ya Tanzania kama kweli inataka kuondokana na mizengwe ya kila siku na mambo yake ya 10% basi nashauri iunde "regulator" na iwape watu (wenye utaalam) leseni za kuzalisha umeme.

Nilipata kutembelea pale E-ON na pana watu wasiozidi mia! Wote ni wahandisi wa mambo ya uzalishaji umeme. Kumefungwa "information" na "real time systems" ambazo zinaonesha ni umeme kiasi gani upo na kiasi gani kipelekwe katika gridi ya Taifa na hapohapo jamaa wamezungukwa na baadhi ya mitambo ambayo wametega ardhini basi ni kitu na boksi tu.

Hapa sikuona wachawi wala misukule ni bongo yako tu.

Lakini nilichukia baada ya kijana mmoja kuniuliza kama kwetu kuna umeme! nikamwambia "I find your question very offensive".

Tchao.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom