Agent Provocateur: Ni wito kwa Serikali kulinda "maadui" wake!

Steve Dii

JF-Expert Member
Jun 25, 2007
6,402
1,254
Explanation nzuri ya agent provocateur ni kama ifuatavyo:
Traditionally, an agent provocateur (plural: agents provocateurs, French for "inciting agent(s)") is an agent employed by the police or other entity to act undercover to entice or provoke another person to commit an illegal act. More generally, the term may refer to a person or group that seeks to discredit or harm another by provoking them to commit a wrong or rash action.

Nakumbuka 2010 jinsi palivyokuwa na tension kubwa kutokana na pilikapilika za uchaguzi. Wakati huo naamini kabisa kwamba iwapo viongozi wakubwa wa upinzani kama Maalim Seif na Dr. Slaa wangelidhurika, lazima pangelitokea machafuko makubwa nchini mwetu. Na hiyo kwa ukubwa isingelitegemea ni sababu zipi zimepelekea viongozi hao kudhurika.

Tulivyoweza kuwalinda wakimbizi wakawaida kutoka nchi jirani, na hata marais kama Obote; basi ni wito na muhimu pia kwa serikali yetu kuwalinda wale wote walio 'high-profile,' maadui kwa marafiki, ndani ya nchi yetu. Maana kutofanya hivyo kunaweza kusababisha madhara mengine makubwa na yenye gharama kubwa kwa amani ya Taifa letu.

The likes of Dr. Ulimboka, mwenzake katika migomo kule Bugando, n.k. hapa nchini wanapaswa kulindwa na serikali, kama jinsi vile wanavyolindwa high-profile suspects kama akina Lulu. Kwani gharama ya kufanya hivyo ni nafuu kuliko ile ya kusawazisha matukio ya jambo-limezua-jambo! Maana matukio ya machafuko yaliyojitokeza kutokana na kudhurika kwa wapinzani wa serikali au kundi la watu fulani katika nchi mbalimbali hapa duniani mifano ipo. Tukio la Dr. Ulimboka ni wito kwa serikali yetu kulinda "maadui" wake!

Steve Dii
 
Naamini serikali makini haihitaji kukumbushwa hayo kwa sababu kama unavyosema iko mifano mingi ya matukio kama ya ulimboka yaliowahi kuleta vurugu nchi mbalimbali,hilo kila mtu anafahamu isipokuwa serikali ya ccm ambayo inahitaji kukumbushwa na wewe.
bunge dhaifu serikali dhaifu waziri mkuu dhaifu rais dhaifu unategemea nini ,sana sana watakimbilia kutumias mbinu za kitoto
binafsi kama mtanzania mmoja tu,sitaamini maneno yoyote kutoka serikalini au mtu yeyote anayejaribu kuonyesha serikali haiukusika katika hili.
ushaidi wa kuhusika kwa serikali upo wazi kwa kila mtu mwenye akili
 
Maneno yoyote hayatawaridha wananchi nikiwemo, ingawa najua kuwa inaweza wanaweza wasihusike kupiga. Ulinzi kazi yao.
 
Back
Top Bottom