AG Werema; Serikali Ingekuwa Makini Usingekuwa Madarakani.

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,794
71,214
Werema, madaraka uliyo nayo yanapaswa kushikwa na mtu mwenye weledi wa hali ya juu katika sheria na mtu anayetumia busara katika kila afanyalo au alisemalo. Mwanasheria Mkuu wa Serikali ndiye mshauri mkuu wa serikali katika mashauri yote ya kisheria na hii si kazi ndogo na ni ya heshima kubwa.

Umejitokeza katika kuipotosha serikali na Bunge mara kwa mara kwa kauli zako zinazoonyesha kuwa hata uwezo wako ni wa kutilia shaka kama kweli ulitimiza vigezo vya kupewa hata huo U jaji wa mahakama kuu.
Mbaya zaidi sasa umeanza na kutoa kauli za kihuni kama wakina Lusinde na Mwigulu. Leo katika kupinga hoja ya Lissu umetamka kuwa "Mtu kuwa na nywele sio kuweza kufikiri" ukimaanisha kauli ya Lissu haikutoka kwa mtu mwenye kuikiri.

Haya ni matusi kwa Mbunge aliyetoa hoja muhimu kama ile inayogusa maisha na mashaka makubwa yaliyowapata watanzania katika ajali ile.

Kama serikali(Rais) haiko makini na kuona wewe kiti hicho kimekuzidi (maana waliopita wote hakuwepo mwenye utendaji mbovu kama wako), SASA NI VEMA WEWE MWENYEWE KUJIPIMA NA KUAMUA KABLA HUJAJIWEKEA HISTORIA CHAFU KUWA AG MBOVU KATIKA NCHI HII.
 
Mimi nilidhani hayo majibu huwa ni ndugu zake tu kumbe hadi mbele ya taifa...huyo jamaa hata ndugu zake hawaelewani naye kabisa kutokana na majibu yake ya kijinga na dharau,sio tu kwa wabunge lakini pia hata wadogo zake na ndugu zake wanamchukia sana.. hata kwenye kijiji chake anakotoka mwaka jana alifanya sherehe ya mwaka mpya 2012 hakuna aliekwenda nyumbani kwake.

Mzee mmoja alidokeza kwamba wazee wote na wamama pamoja na ndugu zake pia wamesusia kwenda kwake ikabidi apite kwenye senta ya kijiji kuhoji kulikoni watu hawajaenda kwake lakini hakuna alieongea nae wala kumjibu hadi akaona aibu akajiondokea...mie mwenyewe nilishuhudia akisalimia wanakijiji wakanyamaza nikauliza kulikoni wakasema ni kutokana natabia yake chafu.
 
Jee ushauri wa kujipima na kutoa maamuzi anaweza kuupokea kama hizo ndio tabia zake? Au ni wakati muafaka kwa mamlaka iliyomteua kuchukua hatua?
 
Meli ya CCM inaendelea kuzama. Bado wamejisahau hawa wanadhani bado wanaendelea kuongoza lile bunge la miaka ile ile. same level of thinking expecting different results
 
AG anajua vyema kuwa kigezo cha yeye pale ni udhaifu period. Ndio maana AG AR hakuongezewa/aliondoka unceremoniously...swala kwamba yeye kama AG ni dhaifu analifahamu fika.
 
Mimi nilidhani hayo majibu huwa ni ndugu zake tu kumbe hadi mbele ya taifa...huyo jamaa hata ndugu zake hawaelewani naye kabisa kutokana na majibu yake ya kijinga na dharau,sio tu kwa wabunge lakini pia hata wadogo zake na ndugu zake wanamchukia sana.. hata kwenye kijiji chake anakotoka mwaka jana alifanya sherehe ya mwaka mpya 2012 hakuna aliekwenda nyumbani kwake.
Mzee mmoja alidokeza kwamba wazee wote na wamama pamoja na ndugu zake pia wamesusia kwenda kwake ikabidi apite kwenye senta ya kijiji kuhoji kulikoni watu hawajaenda kwake lakini hakuna alieongea nae wala kumjibu hadi akaona aibu akajiondokea...mie mwenyewe nilishuhudia akisalimia wanakijiji wakanyamaza nikauliza kulikoni wakasema ni kutokana natabia yake chafu....
Tatoo mkuu,
Hili jamaa linatutia aibu sana watu wa Mara. Kule kwetu hamna watu pamb.afu Kama Werema.
 
Ni jumatatu asubuhi,tusubiri vituko vipya vya Werema ndani ya Bunge
 
Mimi nilidhani hayo majibu huwa ni ndugu zake tu kumbe hadi mbele ya taifa...huyo jamaa hata ndugu zake hawaelewani naye kabisa kutokana na majibu yake ya kijinga na dharau,sio tu kwa wabunge lakini pia hata wadogo zake na ndugu zake wanamchukia sana.. hata kwenye kijiji chake anakotoka mwaka jana alifanya sherehe ya mwaka mpya 2012 hakuna aliekwenda nyumbani kwake.
Mzee mmoja alidokeza kwamba wazee wote na wamama pamoja na ndugu zake pia wamesusia kwenda kwake ikabidi apite kwenye senta ya kijiji kuhoji kulikoni watu hawajaenda kwake lakini hakuna alieongea nae wala kumjibu hadi akaona aibu akajiondokea...mie mwenyewe nilishuhudia akisalimia wanakijiji wakanyamaza nikauliza kulikoni wakasema ni kutokana natabia yake chafu....

Makubwa haya tena.!

Sasa naoana ndiye anayetumia kichwa kuotesha nywele
 
werema ameshindwa kutofautisha kazi na siasa, kitu ambacho kinamghalimu sana
 
Inaweza kuwa tunamlaumu na kumshambulia bure, kwani hayo ayafanyayo ndiyo job discription yake.
 
Back
Top Bottom