AG: Ufafanuzi juu ya uteuzi wa wabunge na kupewa uwaziri

Kama mnaenda mahakamani basi jiandaeni kabisa maana gazeti huru la serikali linariport
nanukuu:

"WAKATI mawaziri wapya na waliobadilishwa wizara wakitarajiwa kuapishwa leo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amesema uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete wa wabunge watatu kuwa mawaziri kabla ya kula kiapo bungeni, ni sahihi wala hajavunja Katiba ya nchi.

Jaji Werema ametoa ufafanuzi huo siku moja baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe kudai kwamba Rais amevunja Katiba
kwa kuwateua wabunge hao kuwa mawaziri kabla ya kuapishwa bungeni."

Mwisho wa kunukuu

sosi:HabariLeo | Mawaziri mguu sawa

Tatizo wakubwa walishazoea kuendesha nchi kama 'absolute monarchy'
 
Mkuu nimeangalia hii post nimeona Tanzania inaendeshwa kama mkokoteni yaani breki ni kubuluza mkokoteni chini. Kitu ambacho kimenifanya sasa nione kuwa tupotupo tu ni huu upuuzi wa kumwachia mtu kama mwanasheria mkuu kujifanya anatafsiri sheria na katika wakati hii ni kazi ya mahakama.

Ni hawahawa CCM na mwanasheria huyuhuyu walizuia swali la mbunge wa CDM ambaye alipeleka swali lake kabla ya kuapishwa na kulipiga chini kuwa hakuwa na uhalali wa kulituma wakati hajala kiapo. Leo hii wanakuja na huu ufafanuzi wa kindumilakuwili kuwa walioteuliwa wana uhalali wa kuanza kazi mara moja. Maana yake nini?, ni kwamba maswali ya wabunge yaliyopelekwa in advance watayatafutia majibu wao katika bunge lijalo kabla hawajaapishwa. Wataandaa budget itakayokuwa sehemu ya bunge lijalo kabla hawajaapishwa na spika.

Nadhani katiba mpya inatakiwa kuweka wazi kuwa Tanzania tunahitaji supreme court itakayokuwa na kazi kuu mbili

1. Kutafsiri katiba pale inapotokea mkanyiko kama huu na si mtu mwenye kuwajibika moja kwa moja kwa aliyevunja katiba ndiyo atolee ufafanuzi kuwa imevunjwa au la

2. Kushughulikia rufaa zote.

Ufafanuzi huu wa Werema maana yake ni kwamba kuna mmoja kati Spika na Rais kavunja katiba na anatakiwa kuwajibika. Kama JK hakuvunja basi Spika alivunja kwa kukataa swali la mbunge aliyetangazwa na mamalaka halali (NEC) kama ambavyo yalivyo mamlaka ya rais kuteua wabunge 10.

Mkuu Hofstede,
Kupeleka swali bungeni hilo ni moja kwa moja kushiriki shughuli za bunge lazima uape kwanza.

Lakini pia yule dada mbunge wa CHADEMA Arusha mbona aliruhusiwa na mwanasheria huyo huyo kwenye uchaguzi wa Meya Arusha? CCM walimgomea kwamba hajaapishwa lakini Mwanasheria akasema huyo ni mbunge halali na ana sifa za kushiriki uchaguzi wa Meya. Kitu ambacho hawezi kushiriki ni shughuli za bunge (national assembly).

Tanzania ina wanasheria wengi tu mahiri, kwanini tusiwatafute na kuwauliza hili? Kwanini mnafikiri mpaka sasa hawajasema lolote?
 
Kuwa waziri si "shughuli ya mbunge" kwa sababu uwaziri si shughuli, ni cheo.Mbunge ambaye hajaapishwa na Spika anaweza kuwa waziri kwa sababu kuwa waziri si "shughuli" achilia mbali "shughuli ya mbunge".

Kuuliza maswali bungeni ni shughuli ya mbunge, kwa hiyo mbunge ambaye hajaapishwa na Spika, kwa mujibu wa katiba, hawezi kufanya shughuli yoyote ya mbunge zaidi ya kumchagua Spika.

Tofautisha shughuli na cheo.
 
=Mtanzania;3861904]Pasco,

Wewe hapa ndiye umechemsha na waulize walimu wako wa mlimani wakusaidie.

Unafikiri kwanini akina Shivji wamekaa kimya toka juzi kama katiba ingelikuwa imevunjwa?

Vifungu hivyo vya sheria viko wazi sana hasa ukisoma katiba ya TZ kwa kiingereza. Pia katika katiba ya TZ hakuna kitu kama mbunge mteule; mbunge akichaguliwa au kuteuliwa huyo ni mbunge.

Ili ashiriki shughuli za bunge (national assembly) inatakiwa aape kwanza kwa spika. Wala hili hata hawajaweka muda wa kuapa. Hivi yule mbunge marehemu wa Arumeru aliapa lini? Je alipoteza haki ya kuwa mbunge kwasababu hakuapa kwa spika?
Mkuu wangu Jeremia Sumari alikuwa naibu waziri na alitangazwa baada ya kuwa mbunge usitake kunambia hakuapishwa... acha hizi mkuu wangu mtu kafariki mwaka huu unataka kusema hakuwahi kuapishwa kweli? na akawa naibu waziri kwa muda wote watu wasihoji?
 
Kama mnaenda mahakamani basi jiandaeni kabisa maana gazeti huru la serikali linariport
nanukuu:

"WAKATI mawaziri wapya na waliobadilishwa wizara wakitarajiwa kuapishwa leo, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema amesema uteuzi wa Rais Jakaya Kikwete wa wabunge watatu kuwa mawaziri kabla ya kula kiapo bungeni, ni sahihi wala hajavunja Katiba ya nchi.

Jaji Werema ametoa ufafanuzi huo siku moja baada ya Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
, Freeman Mbowe kudai kwamba Rais amevunja Katiba
kwa kuwateua wabunge hao kuwa mawaziri kabla ya kuapishwa bungeni."

Mwisho wa kunukuu

sosi:HabariLeo | Mawaziri mguu sawa

Mkuu ina maana kuwa haya ni maelekezo ya CCM kwa majaji kama kawida yao au?
 
Unarudia makosa yale yale ya AG. Waziri au naibu Wazira lazima awe mbunge. Katiba haitoi exemption. Ni mbunge, basi. Kwa tafsiri rahisi sana ni kwamba waziri au naibu waziri anafanya kazi za kibunge. Waziri au naibu waziri anahuduria vikao vya kamati za bunge, anaanda bajeti, anaanda majibu ya wawakilishi wa wananchi (wabunge wenzake). Sasa watafanya hizi kazi kama nani? wabunge wateule? Kama kiapo sio tatizo kwa nini kiwepo?

Kuhusu Marehemu Summari. Strictly speaking, marehemu Summari bado alikuwa mbunge mteule maana hakuwa amekula kiapo.

Ngoja nikueleweshe! katiba ya JMT ni kweli inataka ili uwe waziri lazima uwe mbunge lakini ujue kwamba BUNGE(mbunge) na SERIKALI(waziri) ni mihimili tofauti! zipo nchi ambazo katiba zao zinasema si lazima waziri awe mbunge na nchi nyingine katiba zao haziruhusu kabisa kwa mawaziri kutokana na wabunge lakini mawaziri hawa wanakuwa ni sehemu ya bunge! na kwa Tanzania rais na AG ni sehemu ya bunge pia, sasa kazi za bunge kwa mujibu wa katiba yetu ni kuisimamia na kuishauri serikali. Mbunge ambaye ni waziri ana majukumu yake ya uwaziri ambayo ni tofauti na majukumu yake ya ubunge na sikubali kwamba shughuli za kila siku za waziri ni za kibunge, la hasha! hata kuandaa bajeti, majibu ya masuala mbalimbali n.k ni shughuli zake za kiserikali ambazo itabidi awakilishe bungeni kwa majadiliano, hii sifa ya waziri lazima awe mbunge si kwamba imeshushwa toka mbinguni bali ni utaratibu tuliojiwekea na ndo maana kuna watu wanapendekeza katika katiba mpya sifa hii iondolewe na hata kama ikiondolewa yaani waziri asitokane na wabunge bado mawaziri watakuwa sehemu ya bunge!
Bado nasisitiza kwamba shughuli za kila siku za waziri ni za kiserikali na ufanisi wake utahojiwa na bunge lakini shughuli zake za kibunge zitapimwa na wananchi anaowakilisha! kwa hiyo mawaziri wana mizigo miwili kwanza kutekeleza shughuli za kiserikali na pili kutekeleza majukumu kwenye jimbo lake ila wale wabunge wasio mawaziri wana majukumu ya kibunge tu! Unaposema waziri au naibu waziri anafanya kazi za kibunge unataka kuniambia hujui kuwa waziri ni sehemu ya serikali! na anayo majukumu yake ndani ya mhimili huo ambayo ni tofauti na majukumu ya kibunge!
Halafu marehemu sumaye hakuwa mbunge mteule kwa kuwa alikuwa AMECHAGULIWA kwa kura na si KUTEULIWA na sijawahi kusikia wala kuona ndani ya katiba ya JMT mtu mwenye sifa ya MBUNGE MTEULE.
Ni sawa na kusema shehe fulani ili mwanamke awe mkewe lazima awe na wowowo kubwa na vile vile awe ana uwezo wa kuzaa yaani sio tasa halafu mtu aseme wake wa shehe wanazaa kwa sababu wana mawowowo makubwa wakati ukweli sifa ya kuwa na wowowo haihusiani na uwezo wa kuzaa!
 
Kwani ni lazima Shivji atie neno katika kila linalojiri?
La hasha, tatizo si Shivji kutia neno kwenye kila linalojiri, bali wewe kujipendekeza na kudandia treni kwa mbele kwa ishu usisozijua mapana na marefu yake kwa hoja mbuzi huku ukijifanya interested na mjuaji.
 
La hasha, tatizo si Shivji kutia neno kwenye kila linalojiri, bali wewe kujipendekeza na kudandia treni mkwa mbele kwa ishu usisozijua mpana na marefu yake kwa hoja mbuzi huku ukijifanya interested au mjuaji.

Kubwa jinga una matatizo ya akili wewe.

From now on you are ignored.
 
Mkuu Hofstede,
Kupeleka swali bungeni hilo ni moja kwa moja kushiriki shughuli za bunge lazima uape kwanza.

Lakini pia yule dada mbunge wa CHADEMA Arusha mbona aliruhusiwa na mwanasheria huyo huyo kwenye uchaguzi wa Meya Arusha? CCM walimgomea kwamba hajaapishwa lakini Mwanasheria akasema huyo ni mbunge halali na ana sifa za kushiriki uchaguzi wa Meya. Kitu ambacho hawezi kushiriki ni shughuli za bunge (national assembly).

Tanzania ina wanasheria wengi tu mahiri, kwanini tusiwatafute na kuwauliza hili? Kwanini mnafikiri mpaka sasa hawajasema lolote?
@Mtanzania, Mkuu wangu swala hapa ni kiapo gani kinatangulia kingine sio lini mbunge anaweza kuwa mbunge kabla ya kuapishwa ila swala ni waziri kuwa waziri kabla hajaapishwa na sheria ipo wazi kabisa ikidai lazima aapishwe kwanza. Hatubishani lolote kuhusu Mbunge iwe kashiriki uchaguzi wa Meya au waziri kashiriki uteuzi wa Katibu mkuu au Kenda Ikulu na kuzungumza na rais.

Nimekuuliza swali moja tu. Ibara ya 56, inasema waziri na manaibu hawawezi kushika mamlaka yao bila kuapishwa na rais pamoja na KIAPO Kinginecho.. hivi kiapo kinginecho ni kipi?. maana haiwezekani sheria iandikwe ikiwa hakuna kiapo kinginecho isipokuwa hiki cha bungeni.
 
Asante AG,

Tumetambua nani anajua sheria na nani mbumbumbu wa sheria!

Lakini pia tumetambua hitajio la katiba mpya kuondoa mikanganyiko hii

By Tume ya katiba

Hii imeandikwa na mtu mpana katika mambo ya sheria, na hapa Mwanasheria Mkuu wa serikali ameaibika sana, vinginevyo back to school.
 
werema reasoning capacity yake n ndogo sna nakumbika kwenye maadhimmisho ya miaka50 ya udsm kitivo cha sheria aliandamwa na PRO kanywanyi, PROF shivj na baadh ya wanasheria alipozidiwa akasema walimu wachuo kikuu udsm n wahun na wanafundisha watoto uhuni kwanye maswla ya sheria kwahiyo atarurisha chet chake cha udsm nikacheka sana na alimtukana shivji lakin ukwel baada hap nkamfata PROF Kabud alezee msimamo wake kwenye hili la werema la kurudisha chet akajibu akasema huyu n mkurupukaj hata asiwaumize kichwa na kwali huyu bwana anakurupuka n kwamba unajua simple mathematics huze hesbu hadi 5 ikaruka 3 hapo unakusea wabunge wanateuliwa na rais then wanaapishwa ndan ya bunge anather step wanapata mamlaka nyingine za kuatumikia wa tz kama uwaziri ili waweze fanya kazi na wabunge wengine watawajibikaje kwa bunge wakati hawajawa sehamu ya bunge? na ili uwe sehemu ya bunge lazima uapishwe na bunge.go to hell stupid lawyer and judge
 
Ninachosikitika ni kwamba wengi mnasema kuwa JK/AG wamekiuka katiba bila wale wanaokosoa kunukuu ni ibara au kipengere gani kimekiukwa! sivyo mtu yeyote anavyodhani kuwa ni sawa au si sawa basi ndio iwe haki bali tuangalie katiba inasemaje kuhusu suala hili na si kutoa hoja zetu kutoka kwenye kila kichwa cha mtu!
 
Mkuu Hofstede,
Kupeleka swali bungeni hilo ni moja kwa moja kushiriki shughuli za bunge lazima uape kwanza.

Vipi na kuandaa majibu ya maswali ya wabunge in advance? ili uje uyajibu ukiwa umeapishwa?. Hebu tuache kudanganyana kwenye hili CCM hawana pa kutokea ni ama Rais kavunja katiba ama Spika alivunja katiba.

Hii ni mara ya kwanza nchi kuingizwa kwenye mkenge kama huu na taasisi ya rais. Sasa ndiyo ninajua kuwa kwa nini Tanzania ni masikini. Kwa miaka hamsini plus tumekuwa na katiba ya hovyohovyo.

Lakini pia yule dada mbunge wa CHADEMA Arusha mbona aliruhusiwa na mwanasheria huyo huyo kwenye uchaguzi wa Meya Arusha? CCM walimgomea kwamba hajaapishwa lakini Mwanasheria akasema huyo ni mbunge halali na ana sifa za kushiriki uchaguzi wa Meya. Kitu ambacho hawezi kushiriki ni shughuli za bunge (national assembly).
Mkuu naomba uniwie radhi sijakuelewa kabisa yaani kwenye paragraph hii. Mbunge huyo ni yule aliyerithi kiti cha Regia Mtema(RIP) ambaye aliapishwa pamoja na Nassari last month. Kama sijakosea nadhani wewe unamuongelea Marry Chatanda katibu wa CCM Arusha ambaye ni mbunge wa viti maalum CCM kupitia mkoa wa Tanga. Halafu aliyemruhusu huyu si Werema ni mkurugenzi wa halmashuri ambaye alikuwa msimamizi wa uchaguzi wa meya wa Arusha

Kitu ambacho hawezi kushiriki ni shughuli za bunge (national assembly).
Hii kauli pia katika cerebrum yangu ambayo ina Giga Gigabites with free space 30% reserved for learning from people like you ( I mean used 70%)naona imegoma ku-upload pia naomba ufafanuzi mkuu. Napata Error 52.
 
Mbona Jeremia Sumari alipofariki ilikuwa inatangazwa kuwa mbunge wa Arumaru mashariki kafariki, huku hakuwahi apa hata siku moja bungeni na hakukuwa na mjadara kama huu?. Ikumbukwe kuwa Jeremia Sumari hakuwawahi apa hata siku moja na alizikwa kwa heshima zote za kibunge. Mimi nafikiri tulishaharibu muda mrefu, what we need now is explicit laws to guide us on these issues
 
68. Every member of Parliament shall be required to
take and subscribe before the National Assembly the
oath of allegiance before commencing to take part in
the business of the National Assembly save that he may
take part in the election of Speaker before taking that
oath.

Tafsiri katika Kiswahili!

68.
Kila Mbunge atatakiwa kuapishwa katika Bunge kiapo cha
uaminifu kabla hajaanza kushiriki katika shughuli za Bunge; lakini
Mbunge aweza kushiriki katika uchaguzi wa Spika hata kabla
hajaapishwa.

Nafikiri pia kinachogomba zaidi hapa ni lugha, je hizi tafsiri mbili ni sahihi?...binafsi naamini hizi tafsiri mbili hazifanani wala hazipatani, kwa mfano mdogo tu;

  1. Allegiance - Uaminifu?
  2. Parliament - Bunge? National Assembly?
Na hapo bado kupitia vipengele vyenyewe, yaani mkanganyiko mtupu, nachoka! Yaani tafsiri ya Kiswahili inasikitisha na inaonesha mapungufu makubwa katika umakini unaotakiwa kwenye jambo zito kama Katiba.
 
Back
Top Bottom