AG awaunga mkono CHADEMA

Any way, kuna mambo mengine ni ya kisheria kuliko siasa,
Na mengine pia ni practical reality.

Bahati mbaya, katika sheria kuna tofauti kati ya NCHI na DOLA (Country and State)

Ni vizuri kabla ya kutoa hoja, ukajua yafuatayo

DOLA na NCHI katika Sheria ni vitu sawa?
DOLA ni nini Katika Sheria za Kimataifa?
Ili kuwe na DOLA, vitu gani vinahitajika?
Je, Kati ya Tanzania na Zanzibar, Ipi ni DOLA?
Kwa nini Zanzibar sio Member wa UNO?


Wakati unafikiria maswali hayo, jiulize!

1. Kwa nini Abkazia na Usetia, baada ya kujitangazia Uhuru kutoka kwa Georgia, mpaka leo hazijawa DOLA?
2. Kwa nini Western Polisario ina mipaka na watu, lakini sio DOLA?
3. Kwa nini ISRAEL ni DOLA lakini mipaka yake bado iko disputed, but hali ni tofauti kwa wenzao wa PALESTINE?

UTAPATA JIBU KWAMBA, yanahitajika mambo zaidi ili NCHI iwe DOLA, na sio HIZI SIASA ZETU ZU ZA KILA SIKU.
 
Kwa kauli hii ya Werema, JK hana nchi anayoongoza. Si raisi wa Tanganyika, si raisi wa Zanzibar. Ukiangalia kwa makini hizi nchi mbili bado zipo, hii inayoitwa 'TANZANIA' ni kiini macho.
 
hivi ule mkataba wa muungano ulipatikana?
nadhani kama tunajivunia muungano, ni vema tuuweke wazi na tujivunie hio mkataba.
Au kama haukuandikwa tujivunie kuwa na viongozi wenye kuweza kuaminiana kwa maneno kiasi hicho.
Ni jambo la kujivunia pia.
 
sasa mtaalam wa chemistry, je muungano wa Tanzania ni mixture au compound ?? in my opinion ni compound kwa sababu pamoja na kuungana kila mtu amebakia na asili yake.( refer to the properties of compund)[/QUOT

We umesoma Chemistry shule za kata au chini ya muti??????? Our Union is neither a compound nor a mixiture. A compond is where a newly formed chemical substance possesses new property while in a mixture each component retain its property. In our Union Tanganyika lost its properties while zanzibar retained its properties.
 
sasa mtaalam wa chemistry, je muungano wa Tanzania ni mixture au compound ?? in my opinion ni compound kwa sababu pamoja na kuungana kila mtu amebakia na asili yake.( refer to the properties of compund)
Kaka hii ni mixture, kwasababu bado mmoja amebaki na Identity yake,unless tuwe na serikali moja.
 
Wabunge wa ccm na AG walijibu hoja za Lissu kisiasa na kishabiki wakati zile ni hoja za kisheria na zilihitaji tafsiri ya kisheria na sio sera za ccm au ushabiki! Mfano nilitarajia AG aeleze nini maana ya idara maalum inayoundwa zanzibar na kazi zake zipi??na kwa nn wafanyakazi wa idara hizi maalumu hawaruhusiwi kushiriki kwenye siasa?

Na kwa nn rais wa Zanzibar amejichukulia madaraka ya kuigawa zanzibar mamlaka ambayo imekasimiwa kwa rais wa JMT? pia kwa nn mahakama ya rufaa haikubaliki zanzibar wakati ni ya muungano??Katiba ya SMZ inataja zanzibar ni nchi na mipaka yake na rais wake ni rais wa zanzibar wakati katiba ya JMT inataja zanzibar kama sehemu ya JMT?

Sasa utata huu na mwingine mwingi kati ya hizi katiba mbili ndio unatakiwa ufafanuzi sio kuanza kumshambulia Lissu na professor Shivji!!

Tujikite kwenye hoja za Lissu na zijibiwe moja baada ya nyingine kuliko kuzijibu kwa ujumla na kwa kukashifiana na kushambuliana na wasiojua katiba wazisome walinganishe na anachodai Lissu kuliko kuchangia kitu amabacho hata hukijui!! Muungano uwepo kwa hoja na matakwa ya wananchi sio kwa nguvu na propaganda za viongozi wa CCM!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom