Afya za wabunge wengi - viraka vitupu!!!???

Mgombezi

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
610
178
Leo nilipita sokoni Majengo hapa Dodoma katika kujipatia bidhaa, wakati nazunguka sokoni nikaona sehemu mama mmoja anauza Ubuyu (wenye rangi mbalimbali pamoja na unga wake). Nilivutiwa kwenda kuulizia mafuta ya mbegu za ubuyu kwani kuna ndugu aliniomba nimwangalizie huku Dodoma, ameelezwa yanasaidia kwa wale wenye vidonda vya tumba, naye ana tatizo hilo. Baada ya kuuliza haja yangu, huyu mama alinieleza kwamba yeye hana hayo mafuta bali huwa yanapatikana niendelee kutafuta tu hapa sokoni, lakini huyu mama hakutaka niondoke hivi hivi akanishawishi kwamba naweza kuchukua unga wa ubuyu kwa ajili ya juisi na kusisitiza kwamba una vitamin c. Mama huyu katika kuweka msisitizo hoja yake alisema kwa huzuni sana "UNAJUA TENA MWANANGU AFYA ZENYEWE SIKU HIZI NI ZA KUWEKA VIRAKA, HATA NAMI NATUMIA", hakuishia hapo katika kugongelea msumari wa mwisho katika msisitizo wa hoja yake akasema, "SI UNAJUA TENA BUNGE LIMEANZA WIKI HII, KUMEKUWA NA MSURURU WA WABUNGE HAPA KUNUNUA UNGA HUU WA UBUYU" akamalizia kusema "TUNAFANYA KAZI SANA WIKI HII"

Nilimshukuru yule mama kwa maelezo yake na kuendelea na shughuli zangu pale sokoni, lakini ilinipa kutafakari maneno ya huyu mama juu ya neno VIRAKA, kwanza nilipata picha ya nguo iliyowekwa viraka; kwa wale tulioishi vijijini tunaelewa maana ya nguo yenye viraka, siku hizi walau nguo za mitumba zimepunguza wingi wa viraka katika nguoa. Kwani ukiona nguo imechakaa sana waweza kununua mpya. Sasa mtazamo wa mama huyu anaona AFYA ZA WABUNGE WETU ZIMEJAA VIRAKA VITUPU?.
 
mmh, kidole kimoja chasonta wabunge, vitatu vinakusonta wewe.

Mi kujustify kwamba ubunge,ama wabunge ni kielelezo cha uzinzi huwa sikioni.. Sijui wenzangu wanatumia macho gani..

Yaani uwaangalie watu walionyanyua mizigo,ujipe tu jibu kuwa hawa watakuwa wameshuka kwenye mabasi ya mikoani...au watakuwa wanaenda stendi..
 
Back
Top Bottom