Afya ya Spika Makinda Utata, adaiwa kulazwa India

Tunaendekeza sana ufisadi nchi hii, watu watano? Na kila siku wanakuja na misamiati mipya, eti "kuangaliwa" afya. Madokta wa hapa hawana macho?
aLLOWANCE ZA WATU WATANO KUMSINDIKIZA SPIKA iNDIA zinatosha kujenga maktaba ya shule ya secondari ya mapambano pale Sinza! Hawa watu alioandika kuwa Tanzania ni moja ya nchi kumi za africa zenye Good governance wanayajua haya?Mambo mengine jamani siyo tuu yanatia uchungu bali yanazaa uchungu!!
 
madhala ya kutawaliwa na siasa ya ujamaa na kujitegemea ni mabaya kupita hata utumwa wa mkoloni. Ona sasa kiongozi akatibiwe india wakati tuna hospitali bora hapa nchini kama tano! Jamani tupiganie katiba mpya kabla ya uchaguzi ujao.
 
Acheni uzushi bibi wa watu yuko fiti kama kijiti cha mpingo,kwa jinsi ya ufahamu wangu kama angekuwa ni mgonjwa kwa sheria sisi kama raia tuna haki ya kujulishwa hali ya viongozi wetu,labda watufiche maradhi yake.
 
Hii sikuipenda. JF itaonekana ni jukwaa la vichaa kwa sababu ya fundamentalists!

Mimi siwalaumu hata kidogo kwani viongozi wetu hawajali kabisa maisha ya watu maskini.Maskini wa nchi hii wanakufa kwa kukosa huduma za afya alafu ukitokea mgomo wa madaktari huyo huyo spika anakuwa upande wa serikali sasa kwani akifa yeye sisi tusikitike.kumbuka jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kuzima hoja zozote kuhusu kujadili mgomo wa madaktari bungeni.Jiulize kama yeye alikuwa hajui kuwa kuna watu wanakufa kutokana na mgomo ule.Jiulize alizima zile hoja kwa manufaa ya nani kama sio chama chake.Tafakari kiongozi wa aina hiyo kwake muhimu ni chama chake au mwananchi.

Angalia hata raisi wa nchi kila siku safari.Jiulize hizo hela za kugharamia safari zake zinatoka wapi wakati watumishi wa umma hawalipiwi haki zao kwa madai kuwa serikali haina hela lakini hela za kugharamia safari za raisi kila siku zipo.

Nchi hii ni ya ovyo sana.Maskini wa nchi hii umuhimu wake ni wakati wa uchaguzi tu na uchaguzi ukipita na utu wake ndio umepita.
 
Ndugu yangu huyu ni binadamu.....ana ndugu jamaa na marafiki....unadhani wanajihisi vipi wakisoma andishi lako??? Kura ngapi utapoteza kwa kujenga chuki isiyo na maana?? .....TAfakari.....

Kuna watu wana roho mbaya hujawahi ona.
 
Mimi siwalaumu hata kidogo kwani viongozi wetu hawajali kabisa maisha ya watu maskini.Maskini wa nchi hii wanakufa kwa kukosa huduma za afya alafu ukitokea mgomo wa madaktari huyo huyo spika anakuwa upande wa serikali sasa kwani akifa yeye sisi tusikitike.kumbuka jinsi alivyokuwa mstari wa mbele kuzima hoja zozote kuhusu kujadili mgomo wa madaktari bungeni.Jiulize kama yeye alikuwa hajui kuwa kuna watu wanakufa kutokana na mgomo ule.Jiulize alizima zile hoja kwa manufaa ya nani kama sio chama chake.Tafakari kiongozi wa aina hiyo kwake muhimu ni chama chake au mwananchi.

Angalia hata raisi wa nchi kila siku safari.Jiulize hizo hela za kugharamia safari zake zinatoka wapi wakati watumishi wa umma hawalipiwi haki zao kwa madai kuwa serikali haina hela lakini hela za kugharamia safari za raisi kila siku zipo.

Nchi hii ni ya ovyo sana.Maskini wa nchi hii umuhimu wake ni wakati wa uchaguzi tu na uchaguzi ukipita na utu wake ndio umepita.

Nakuunga mkono, lakini hata hivyo, sikubali kuwa Spika Makinda akifa ndipo tutapata suluhisho la matatizo yetu. Lugha ya kumuombea mwenzako kifo inakera. Upinzani sio uadui.
 
Kuna watu wana roho mbaya hujawahi ona.

Hapa. Si suala la Rohombaya.....ni suala la ufinyu wa kufikiri....kutojiamini.....kwamba mnaweza kuwepo pale tu wasipokuwepo...mmekata tamaa...nani atawaamini sasa??
 
ukitaka kujua hospital zenu hakuna kitu aumwe mtu mkubwa hata ni homa ataenda nje ya nchi kwa kifupi sisi mafukala ndio tuna tibiwa kwenye hizi hospital amabazo hazina dawa, vifaa, hata machine za kuona ugonjwa gani unamsumbua mgonjwa
 
wanajua fika kuwa serikali hainuni vifaa vya kutosha katika hospitali zetu ingawa sisi wanatudanganya kuwa serikali imeboresha huduma za afya. Mungu akiwaumbua na kuwauguza wao hapo ndipo ukweli unapojidhihirisha maana wanakimbilia kutibiwa nje kwa madai wamepewa rufaa baada ya hospitali zetu kushindwa. Au magonjwa yao ni tofauti ya kwetu?? Shame

ANATAKIWA AUGUE MIEZI KAMA KUMI HIVI, AJUEALICHOKUWA ANATETEA ULIMBOKA. Simtakii nafuu kwa sasa mpaka ajifunze utu!!
 
Jamani ! yawezekana ni kuangalia afya tu, wakashanga anaweza kutembea na magonjwa aliyonayo!
 
ANATAKIWA AUGUE MIEZI KAMA KUMI HIVI, AJUEALICHOKUWA ANATETEA ULIMBOKA. Simtakii nafuu kwa sasa mpaka ajifunze utu!!

Duh hapa ndio nimejua sasa kuwa watu wamechoka unafiki maana wengi sana wamemuombea mabaya huyu mama
 
mungu wa majeshi

Viongozi walio wagumu na watendayo kinyume na matakwa yako washindwe kwa jina la yesu.

Angalia bwana, wanashindwa na hawataki kufanya mazuri hapa, wakitegemea kuyapata nje kwa kutumia ukiburi walionao.

Ikiwezekana bwana fanya kama upendavyo kutuepusha nao kwa njia upendayo bwana.

Amen

Walahi! Hili ombi hili? Bhaasi
 
Back
Top Bottom