Afya ya Spika Makinda Utata, adaiwa kulazwa India

Mwana Mpotevu

Platinum Member
Sep 7, 2011
3,295
2,500
Ni habari katika Tanzania daima la leo

Afya ya Spika yazua utata


na Ratifa Baranyikwa


amka2.gif
KUNA taarifa za kutatanisha kuhusu afya ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, ambapo inadaiwa kuwa amelazwa katika Hospitali ya Apollo nchini India.

Habari za ambazo gazeti hili limezipata toka nchini India kwa watu wake wa karibu, zimeeleza kuwa Spika amelazwa tangu wiki iliyopita katika hospitali hiyo.

Vyanzo vyetu hivyo vilisema, Spika Makinda ameongozana na watu watano ambao wamekuwa wakionekana naye hospitalini hapo.

Hata hivyo, gazeti hili halikuweza kufahamu mara moja ugonjwa unaomsumbua kutokana na jambo hilo kuwa siri kati ya mgonjwa na madaktari wake.

Taarifa za ndani zinasema kuwa baadhi ya watu waliofika kumuona waliambiwa kwamba anasumbuliwa na macho.

Alipoulizwa kuhusu taarifa hizo, Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila, alikiri kuwa Spika alikwenda nchini humo kwa shughuli mbili ikiwamo ya kufanya uchunguzi wa afya wa kawaida.

Alisema Makinda alikwenda nchini humo mwanzoni mwa mwezi huu kwenye mkutano wa Maspika Wanawake (IPU) na baada ya kumaliza shughuli hiyo ndipo akaenda kufanya uangalizi wa afya yake.

Kashilila ambaye hata hivyo alikwepa kuzungumzia kama Spika amelazwa, aliishia kusema tu kwamba alipitia kufanya uangalizi wa kawaida wa afya yake na amekuwa akifanya hivyo kila mwaka.

Kwa mujibu wa Kashilila, Spika atarejea wiki ijayo baada ya kumaliza taratibu zote za kuangalia afya yake.

Wakati Dk. Kashilila akisema hivyo, mitandao mbalimbali ya intaneti, ilionyesha kuwa mkutano huo wa maspika wanawake ulifanyika kati ya Oktoba 3 hadi 4 mjini New Delhi, nchini humo.

Hivyo, endapo Spika alitoka kwenye mkutano na kupitia moja kwa moja kuangalia afya yake, atakuwa ametumia takriban siku 11 hadi kufikia leo.


TUMUOMBEE SPIKA WETU AREJEE SALAMA BUNGE LINAANZA HIVI KARIBUNI


 
Tunaendekeza sana ufisadi nchi hii, watu watano? Na kila siku wanakuja na misamiati mipya, eti "kuangaliwa" afya. Madokta wa hapa hawana macho?

wanajua fika kuwa serikali hainuni vifaa vya kutosha katika hospitali zetu ingawa sisi wanatudanganya kuwa serikali imeboresha huduma za afya. Mungu akiwaumbua na kuwauguza wao hapo ndipo ukweli unapojidhihirisha maana wanakimbilia kutibiwa nje kwa madai wamepewa rufaa baada ya hospitali zetu kushindwa. Au magonjwa yao ni tofauti ya kwetu?? Shame
 
wanajua fika kuwa serikali hainuni vifaa vya kutosha katika hospitali zetu ingawa sisi wanatudanganya kuwa serikali imeboresha huduma za afya. Mungu akiwaumbua na kuwauguza wao hapo ndipo ukweli unapojidhihirisha maana wanakimbilia kutibiwa nje kwa madai wamepewa rufaa baada ya hospitali zetu kushindwa. Au magonjwa yao ni tofauti ya kwetu?? Shame
Umepatia sawasawa.
 
Wakiumwa wao India,tukiumwa cc temeke,mwananyamala,ilala hospital n.k, kumbe huduma zetu haziwafai,hawa jamaa wanatufanya cc madaraja,kodi zetu lakini zinawanufaisha wao na jamaa zao, Mungu ibariki Bongo
 
Kizazi cha hawa viongozi wetu hakina aibu wala hakiwezi kututoa kwenye fikra potofu. Kinaabudu sana kila kitu nje! Hivi wanajisikiaje wakiwa wanaenda kutibiwa nje wakati kuna wataalamu kibao nchini? Na je watajisikiaje siku watakapokuwa kando ya uongozi harafu magonjwa yao yote waliyokuwa wanatibiwa nje yataakuwa yanatibiwa nchini pengine kwa gharama nafuu zaidi kuliko huko nje? Ndiyo maana wanaiba pesa, na badala ya kufungua miradi angalau iwaajiri watanzia wengine, wao wanapeleka uswisi pesa bila kujua wanadidmiza uchumi wa nchi yetu kwa kuzuia mzunguko wa pesa.
 
Hivi muhimbili ni gulio pale? Mbona wakuu hawatibiwi hospital za hapa? Maisha yao ya dhamani sana eeh?
 
Hivi wadau haya majimbo ambayo yapo wazi kwa sasa mbona sisikii tume ikitangaza chaguzi ndogo? Jingine 'Likitokea' Jeee!
 
Mwana Mpotevu ...ccm...ccm...yaani hata kupima afya kwa utaratibu wa kawaida ni zoezi la kufanywa ughaibuni?...sina ushaidi wa moja kwa moja...lkn nanusa mazingira ya rushwa hapa..! kwamba apollo hospital wametoa mlungula ili zoezi la kawaida la kupima afya za viongozi wetu kwa gharama za serikali..lifanyike hapo kwao...au kuna maafisa waliojaa ufisadi wamefanza dili tayari....wala huitaji phd kujua haya, na kufanya utafiti wa kisayansi kubaini ukweli wa hili ni kupoteza pesa zetu chache...na matumizi mabaya ya muda wetu mfupi tulionao...vinginevyo kama "wanafanyaga" hivyo kwa gharama zao..
 
Last edited by a moderator:
Medical check up mpaka India?
Medical check up gani hiyo mtu unalazwa hospitalini tena zaidi ya wiki nzima?
 
Tunaendekeza sana ufisadi nchi hii, watu watano? Na kila siku wanakuja na misamiati mipya, eti "kuangaliwa" afya. Madokta wa hapa hawana macho?

Madaktari wakidai hospitali zetu ziboreshwe..Ina-WALIMBOKA. Wabunge wakidai maelezo Spika huyo huyo anadai KESI Iko MAHAKAMANI!!!kwa sababu wana UFISADI wa kwenda INDIA. Watu watano wa nini? Wao ni WAUGUZI? kwani huko APPOLO hakuna wauguzi?
 
Hivi wadau haya majimbo ambayo yapo wazi kwa sasa mbona sisikii tume ikitangaza chaguzi ndogo? Jingine 'Likitokea' Jeee!

They have project more to vacant thus they are waiting so that by-election can be held on the same day
 
Get well soon Bi mkubwa,anaogopa sakata la wabunge kutuhumiwa kula rushwa,Ngwilizi kawageuzia kibao prof muhongo na maswi.
 
usihukumu, usije ukahukumiwa..mwachieni Mungu, ataitwa Mungu daima, na mkono wake , hakuna hata fisadi mmoja atakayepona
 
Back
Top Bottom