Afungwa siku 14 kwa kuvaa mlegezo mahakamani

Kwa hiyo kigezo ni kama zinaruhisiwa au hazuhusiwi kuuzwa? Kama ndio kigezo, basi kwa vile ni ruksa kuuza chupi basi watu wawe wanarhusiwa kuingia mahakama wakiwa wamevaa vyupi tuu?
nafikiri mfano wako ni mfu! haulengi maana. nguo kulegea si kuvunja sheria. hajatembea huchi huyu. zamani watu walivaa nguo pana (pekosi, bellbotom), wakavaa zinabana (chupa), madada wanavaa minskate na mapaja yako nje hawajakamatwa. si mlegezo zamani ziliitwa mtepesho!! the old is gold!! mahakama lazima ifuate sheria si tu hakimu anaamua tu.
mtu anaiba maelfu hafungwi mwizi wa kuku anakula miaka mingi tu haki ipo?
chenge anagonga nakuua analipa 7lki, daladala inagonga dreva miaka mingi jela haki wapi?
na mifano mingi inayoonyesha jinsi tanzania kusivyo na usawa hadi katika sheria.
oinabidi tuanze pia kuzipigia kelele hata mahakama.
 
Hii ni Jamaica... nimesoma hapa:

Ni sawa, na kama in Tanzania this applies too, basi hakim alifanya kazi yake.
BUT, naogopa kutakua na abuses. Imagine wanasema no earings. kwa nini? that is just because they don't like them? wengine tunavaa cultural earings, they are the symbol of us being daughers of such and such, sister of such and such, our position in the family, our status as mothers etc. Utamwambia mmasaai asivae hereni, it is part of his identity you are stripping just then. talkiing about masaai, would you tell them not to expose their tights in court if they come in their traditional outfit? they should exercise some judgement.

Mbaya zaidi WaTZ hatupo AWARE na hizo sheria...
Na utaratibu wa mawakili nao umetupita kushoto.
Sifagilii milegezo lakin naona huyo kaka wamemuonea tu.Huyo hakimu alipaswa kufikiria zaidi na sio kuweka misimamo yake binafsi
 
afi kabisa mana hii tabia imewaharibu vjana sana cjui lipi lipi linalowavutia
 
young.jpg


Katika hali iliyowashangaza wengi,msela mmoja aliyetambulika kwa jina la Rajabu Athumani, jana alihukumiwa kifungo cha siku 14 kwa kosa la kuonekana mahakamani akiwa amevalia kaptula chini ya makalio maarufu kama mlegezo au Kata K.


Athumani ambaye alifika katika Mahakama ya Wilaya Ilala kwa ajili ya kusikiliza kesi nyingine inayomkabili ambayo kwa mujibu wa karani wa Mahakama hiyo ni ya ubakaji, alionekana akiwa amevalia hivyo huku nguo za ndani zikionekana.


“Mtu kuvaa suruali chini ya makalio ikiwa sio maadili yetu na tamaduni zetu Waafrika hasa kwenye shughuli za Serikali na kuonesha nguo zake za ndani, anachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo,” alisema Hakimu.
 
Mbaya zaidi WaTZ hatupo AWARE na hizo sheria...
Na utaratibu wa mawakili nao umetupita kushoto.
Sifagilii milegezo lakin naona huyo kaka wamemuonea tu.Huyo hakimu alipaswa kufikiria zaidi na sio kuweka misimamo yake binafsi
I agree with you ZD. Ila hapo bold kuna msemo wa mahakama usemao: Ignorantia juris non excusat. (not being aware of a law is not an excuse [for violating it]) au tena:Nemo legem (jus) ignorare censetur (nobody is supposed to ignore the law)
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Achilia mbali maadili, wanadhalilisha viwanda vya nguo, wao wameweka saizi tofauti za ngua..20; 21;22........na kuendelea, sasa kama mwili wako ni mdogo nunua kulingana na ww, mwisho wa siku chupi tuta vaa juu ya suruali!
 
Achilia mbali maadili, wanadhalilisha viwanda vya nguo, wao wameweka saizi tofauti za ngua..20; 21;22........na kuendelea, sasa kama mwili wako ni mdogo nunua kulingana na ww, mwisho wa siku chupi tuta vaa juu ya suruali!

Ha ha haaa!! Hii kali mkuu.
 
hii ni kali kwa kweli.........
miaka minne???????
gharama za kumlisha miaka minne kwa kuvaa mlegezo?
kwa nini wasingemchapa bakora yakaisha?
au miezi sita?

Miaka 4 ipi tena mkuu. Ni siku 14, jamaa kapigwa ndani siku 14. Napenda kamata kamata ije mpaka mtaani, hasa vituo vya daladala makonda wote piga ndani.
 
MSHITAKIWA Rajabu Athumani (20) jana amehukumiwa kifungo cha siku 14 kwa kosa la kuonekana mahakamani akiwa amevalia kaptula chini ya makalio maarufu kama mlegezo.

Athumani ambaye alifika katika Mahakama ya Wilaya Ilala kwa ajili ya kusikiliza kesi nyingine inayomkabili ambayo kwa mujibu wa karani wa Mahakama hiyo ni ya ubakaji, alionekana akiwa amevalia hivyo huku nguo za ndani zikionekana.

“Mtu kuvaa suruali chini ya makalio ikiwa sio maadili yetu na tamaduni zetu Waafrika hasa kwenye shughuli za Serikali na kuonesha nguo zake za ndani, anachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo,” alisema Hakimu.

HabariLeo | Afungwa siku 14 kwa kuvaa mlegezo mahakamani

Wakuu hii nilishuhudia mwenyewe na siku kadhaa baadae mama mmoja alikoswakoswa kwa simu kuita akiwa mahakamani.
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Wadhamini wasweka rumande kwa kuvaa suruali mlegezo

25 Octoba 2010

MAHAKAMA ya Wilaya ya Ilala Ijumaa iliyopita iliwasweka mahabusu siku 14 wadhamini wawili wa mshtakiwa baada ya kuingia mahakamani wakiwa katika hali ambayo mahakama hiyo iliitafsiri kuwa ni nusu uchi.

Kabla ya mahakama hiyo kuamuru waswekwe rumande mwishoni ,wadhamini hao Ramadhani Bakire (19) na Mgeni Jetta (22) walifika mahakamani hapo kwa lengo la kumuwekea dhamana ndugu yao anayekabiliwa na kesi ya jinai. Wakati wakiingia mahakamani hapo walikuwa wamevalia suruali aina ya Jeans wakiwa wamezifunga kwa mikanda chini ya makalio katika mtindo uitwao “kata k” huku nguo za ndani zikionekana hadharani.

Hakimu Wilberforce Luhwago aliyekuwa akisikiliza kesi ya ndugu yao huyo alilazimika kuacha kusoma barua zao hizo za udhamini baada ya kuona nguo zao za ndani zikiwa nje hadharani ndani ya mahakama na kuwahoji sababu ya kuingia mahakamani wakiwa wamevaa namna ile.

“Ninyi kwa nini mnaingia mahakamani mkiwa mvaa nguo huku mmezishusha namna hiyo?” alihoji Hakimu Luhwago.

“Mheshimiwa Hakimu, kosa la kwanza si kosa tusamehe tu na siku nyingine hututakuja hivi,” alijibu mmoja wa wadhani hao, Ramadhani Bakire huku akipandisha suruali yake baada ya kubaini Hakimu kutopendezewa na hali.

Hata hivyo licha ya utetezi wao huo, Hakimu Luhwago aliyeonekana kukerwa na hali hiyo aliwaambia kuwa kamwe hawezi kuruhusu Mahakama kugeuka kuwa uwanja wa kufanyia maigizo na kwamba karipio la mdomo pekee halitoshi isipokuwa kuwapumzisha rumande

“Siwezi kuwapa karipio la mdomo kama njia ya kuwafundisha jinsi ya kuingia Mahakamani kwa adabu.Nafikiri aina ya uvaaji mliouvaa umeanza kukubalika kwa baadhi ya macho ya watu na katika baadhi ya maeneo fulani fulani;

Lakini kwa hakika siwezi nikaruhusu na Mahakama nayo kuwa sehemu inayoweza kuvaliwa uvaaji wa aina hii, huu ni uhuni. Kwa hiyo mtapumzika ndani (mahabusu ) hadi kesi hii itakapotajwa tena hapa mahakamani (Novemba 5 mwaka huu)” alisema Hakimu Luhwago.

Mwanamke mmoja aliyejiambulisha kwa Hakimu huyo ni dada wa vijana wadhamini hao alimuomba hakimu huyo awasamehe kwa kosa hilo, lakini bila mafanikio.

“Umeshindwa kuwalea na kuwafudisha kuwa aina ya uvaaji huo una mipaka, najua kazi ya malezi ni ngumu, na hata viongozi wa dini hawajafanikiwa sana katika hilo;

Kwa hiyo ndio maana sasa Mahakama inasaidia ulezi huo angalau kwa siku 14 tu hawatahitaji kufunzwa tena na hawatorudia tena kuingia kihuni mahakamani,” alisisitiza Hakmu Luhwago

Source: Wadhamini wasweka rumande kwa kuvaa suruali mlegezo

Same Hakimu. Very strict, yaani noma. Mahakama ya Ilala wanamhara kuanzia makarani, waendesha mashitaka na kila mtu. Kajamaa hakali rushwa hata kidogo.Atachukua pesa yako halafu siku ya hukumu unapata haki yako kama ni kifungo haya na pesa yako unarudishiwa.
 
Back
Top Bottom