Afungwa siku 14 kwa kuvaa mlegezo mahakamani

EJM_

JF-Expert Member
Jul 8, 2011
3,836
2,091
MSHITAKIWA Rajabu Athumani (20) jana amehukumiwa kifungo cha siku 14 kwa kosa la kuonekana mahakamani akiwa amevalia kaptula chini ya makalio maarufu kama mlegezo.

Athumani ambaye alifika katika Mahakama ya Wilaya Ilala kwa ajili ya kusikiliza kesi nyingine inayomkabili ambayo kwa mujibu wa karani wa Mahakama hiyo ni ya ubakaji, alionekana akiwa amevalia hivyo huku nguo za ndani zikionekana.

“Mtu kuvaa suruali chini ya makalio ikiwa sio maadili yetu na tamaduni zetu Waafrika hasa kwenye shughuli za Serikali na kuonesha nguo zake za ndani, anachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo,” alisema Hakimu.

Katika hatua nyingine, Mawazo Nelson Kigalu (34) amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala akikabiliwa na shitaka la kuiba tairi za behewa zenye thamani ya Sh milioni 1.5.

Mbele ya Hakimu Jannet Kinyage , Mwendesha Mashitaka Denis Muyumba alidai Desemba 13 mwaka jana muda usiojulikana usiku katika yadi ya reli katika Wilaya ya Ilala, Nelson aliiba tairi mbili za behewa zenye thamani ya Sh milion 1.5 mali ya kampuni ya reli.

Mshitakiwa alikana shitaka na kurudishwa rumande hadi Aprili 3 mwaka huu shauri hilo litakapotajwa tena.

Kaaazi kweli kweli!
 
hao wavaao mlegezo wakamatwe.pia waoneshao matiti nje wakamatwe pia.
Umenikumbusha kuna wakati fulani kulikuwa na fashion ya wasichana ya kuvaa suruali zimeachia juu sasa walikuwa wakikaa kwenye daladala kwenye vile viti vya nyongeza kila kitu njeeee
 
Umenikumbusha kuna wakati fulani kulikuwa na fashion ya wasichana ya kuvaa suruali zimeachia juu sasa walikuwa wakikaa kwenye daladala kwenye vile viti vya nyongeza kila kitu njeeee

Suruali za kuachia juu ndiyo zipi?

Au kutofunga kifungo na zipu?

Alaah.. Unasema kwa nyuma,mgongoni... Ilikuwa balaa kweli..
 
Suruali za kuachia juu ndiyo zipi?

Au kutofunga kifungo na zipu?

Alaah.. Unasema kwa nyuma,mgongoni... Ilikuwa balaa kweli..
Yaani zilikuwa hazina mikanda halafu nyingi zilikuwa za jeans halafu kama hazijapindwa hivi kwa juu so u can imagine balaa lake
 
hakimu bana eti mtu kuvaa kinyume na tamaduni na maadili yetu waafrika 'hasa kwenye shughuli za serikali'....anachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo...
 
hakimu bana eti mtu kuvaa kinyume na tamaduni na maadili yetu waafrika 'hasa kwenye shughuli za serikali'....anachukuliwa hatua haraka iwezekanavyo...
Mi haya maadili ya mavazi bhana utasikia ooh maadili ya kiafrika, hivi wamesahau kama kimsingi maadili ya kiafrika ni kutembea uchi au kujifunika hapa mbele tu!
 
ni kujaza magereza hovyo na kutumia kodi za watanzania kijinga jinga, kwa nini asipewe adhabu za kuhudumia jamii kama kuzibua mitaro huko barabarani?
 
ni kujaza magereza hovyo na kutumia kodi za watanzania kijinga jinga, kwa nini asipewe adhabu za kuhudumia jamii kama kuzibua mitaro huko barabarani?

Umeongea la maana sana, tatizo la sie waTz hatuna ubongo shirikishi, ebu imagine productivity ingekuwaje once the countless people waliofungwa kwa petty crimes wangepewa adhabu za kuhudumia jamii.
 
Umeongea la maana sana, tatizo la sie waTz hatuna ubongo shirikishi, ebu imagine productivity ingekuwaje once the countless people waliofungwa kwa petty crimes wangepewa adhabu za kuhudumia jamii.
Tabu ni kwamba wanaostahili kwenda jela hawaendi na wale wasiostahili ndio wamejazana huko
 
tairi za mabehewa? mabehewa yana tairi? Hii itakuwa kesi ya kupakaziwa.
 
Kama hujajiandikisha kupiga kura tafadhali do zoezi likianza, hiyo ni hatua ya kwanza 2015 sio mbali.
But what difference doest make? Coz mahakama inafuata sheria ambazo whoever is in charge anafuata sema ni upuuzi wa watu wenyewe tu
 
Back
Top Bottom