Afungwa Jela miezi 3 kwa kukataa kuhesabiwa.

Mpigaji

JF-Expert Member
Feb 6, 2011
384
42
Mkazi mmoja wa mkoa uliopo katika kanda ya ziwa amehukumiwa kwenda jela miezi mitatu kwa kukataa kuhesabiwa katika zoezi la sensa linaloendelea nchini Tanzania.Mkazi huyo alikataa kujibu maswali ya dodoso la sensa ya watu na makazi kwa kuwa hakuna kipengele kinachouliza Dini!Mbele ya Hakimu wa mahakama,mkazi huyo alikiri kosa hilo,hakimu alimhukumu kifungo cha miezi 3!
SOURCE:Matukio Radio Free Africa-(29/08/12)
 
Hongera zake kwa kuonyesha msimamo hata mwisho. Hata kwenye Bible kina Shedrack walitupwa kwenye tanuru la moto kwa kukataa kuabudu Miungu feki, na Bwana wao aliwaokoa.
 
Hongera zake kwa kuonyesha msimamo hata mwisho. Hata kwenye Bible kina Shedrack walitupwa kwenye tanuru la moto kwa kukataa kuabudu Miungu feki, na Bwana wao aliwaokoa.

Wewe mbona hukufungwa kama yeye??
 
Hongera zake kwa kuonyesha msimamo hata mwisho. Hata kwenye Bible kina Shedrack walitupwa kwenye tanuru la moto kwa kukataa kuabudu Miungu feki, na Bwana wao aliwaokoa.
Waliomshamishi wanasemaje? Msimamo wa kijinga. Shedrack alikataa miungu feki, huyo aliyefungwa naye kakataa kitu gani feki? Mbona kakiri kosa?
 
mkazi mmoja wa mkoa uliopo katika kanda ya ziwa amehukumiwa kwenda jela miezi mitatu kwa kukataa kuhesabiwa katika zoezi la sensa linaloendelea nchini tanzania.mkazi huyo alikataa kujibu maswali ya dodoso la sensa ya watu na makazi kwa kuwa hakuna kipengele kinachouliza dini!mbele ya hakimu wa mahakama,mkazi huyo alikiri kosa hilo,hakimu alimhukumu kifungo cha miezi 3!
Source:matukio radio free africa-(29/08/12)

Kapelekwa lokapu lini, uchunguzi umefanyika lini, kesi imesikilizwa lini. Utetezi umefanyika lini. Mweee! Amakweli akili ni nywele. Nchi Hii kwa viumbe kama nyinyi kamwe haiwezi kuendelea. No wonder this country is poor but rich.

 
huu ni uonevu mtaani kwangu kuna watu wengi tu wamekataa kuhesabiwa wao na familia zao lakini hawajachukuliwa hatua..
 
huu ni uonevu mtaani kwangu kuna watu wengi tu wamekataa kuhesabiwa wao na familia zao lakini hawajachukuliwa hatua..

Kama Wameshawishiwa Karani anachokifanya ni kumpa taarifa Mwenyekiti wa Mtaa halafu baada ya Sensa Watakiona cha Moto
 
ivi hcho kipengele cha dni ndo kinakamilisha sensa? je uislam unapimwa na icho kipengele?
 
Mkazi mmoja wa mkoa uliopo katika kanda ya ziwa amehukumiwa kwenda jela miezi mitatu kwa kukataa kuhesabiwa katika zoezi la sensa linaloendelea nchini Tanzania.Mkazi huyo alikataa kujibu maswali ya dodoso la sensa ya watu na makazi kwa kuwa hakuna kipengele kinachouliza Dini!Mbele ya Hakimu wa mahakama,mkazi huyo alikiri kosa hilo,hakimu alimhukumu kifungo cha miezi 3! SOURCE:Matukio Radio Free Africa-(29/08/12)
vipi mkuu,kama ukisema kifungu gani cha sheria alichotumia jaj kutoa hukumu hiyo ili nikijue nkatoe elimu kwa maboya fulani hivi wanaobishi et hakunaga sheria ka hiyo!MSAADA PLEASE!
 
Sijajua kipengele cha Dini kwenye sensa kikiwekwa tukajua Waislamu wako kadhaa, Wakristo kadhaa, Wahindu kadhaa, nk ndio kinafuata nini? Ndio maendeleo (barabara, zahanati, hospitali, shule, nk) yatapangwa kulingana na dini hizo? Kama sivyo ya nini kugomea vitu vinavyoleta maendeleo?
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom