Lyimo
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 3,826
- 2,017
Kula tano. Tuache ushabiki, mara ya mwisho kuona research ya wabongo kwenye Journal kama "Nature","Science" au nyingine yoyote ya caliber hiyo ilikuwa lini?
Wengine wanamaliza chuo bila hata kujua hizo journals ni nini ingawa zipo katika fields zao.
Na kama wasomi wetu ndio hao Dr. Kigwangwalla type (msomi Kigwangwalla) basi tushapigwa ngwala.
Naungana nanyi kwa kuelezea vigezo vinavyotumika katika ranking. Ila bado wasomi wetu ni bora, maana wanafit kwenye vyuo vilivyo bora dunianai na hata wapo wahadhiri kwenye hivyo vyuo ambao wamechimbuliwa na mifumo ya elimu ya Africa. Kuhusu machapisho, pia tuna watafiti wetu ambao wanachapisha kwenye majarida yenye high impact factor kama Nature, Science etc ila ni wachache. Pia nakubaliana tubadili mifumo ya PhD zetu zingine zipatikane kwa majarida (by papers) siyo kung'ang'ania za thesis/dessertation tu. Curriculum zetu pia ni bora kama za wenzetu na zinafanyiwa review mara kwa mara, labda changamoto iwepo kwenye ufundishaji, motivation na wanafunzi wenyewe kujishughulisha. Maana curriculum pekeyake si kigezo cha kutoa product nzuri. Nimefurahishwa na wana JF (na wadau wengine) kuwa sensitive kwenye hili.