Afrika Kusini kujiondoa mahakama ya ICC

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,397
Afrika Kusini imeanzisha mchakato wa kujiondoa kutoka uanachama wa mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita.

Wanadiplomasia wa Afrika kusini wamearifu umoja wa mataifa juu ya uamuzi huo na kuilaumu ICC kwa kuzilenga zaidi nchi za Afrika.

Uamuzi wa Afrika kusini kujiondoa ulitokana na shinikizo ilikumbana nazo mwaka uliopita za kuitaka imkamate rais wa Sudan Omar al Bashir wakati wa mkutano wa muungano wa nchi za Afrika mjini Johannesburg.

Septemba mwaka jana, mahakama nchini nchini Afrika Kusini iliinyima serikali ya nchi hiyo ruhusa ya kukata rufaa uamuzi ulioishutumu kwa kukosa kumkamata Bw Bashir alipohudhuria kongamano hilo mwezi Juni mwaka 2015.

Serikali ilitaka kukata rufaa uamuzi wa Mahakama Kuu ikisema Bashir alikuwa na kinga ya urais kwa sababu yeye ni kiongozi wa taifa.

Lakini Jaji Hans Fabricius alisema rufaa hiyo haiwezi kufanikisha chochote.

Aliongeza kuwa Afrika Kusini ni mwanachama wa Mkataba wa Roma uliounda mahakama hiyo, na kwamba mkataba huo unabatilisha sheria zozote ambazo huenda zingempa kinga Bashir asikamatwe na kushtakiwa.

Kiongozi huyo wa Sudan amekuwa akisakwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kwa tuhuma za kutekeleza mauaji ya halaiki na makosa ya uhalifu wa kivita Darfur.

Kiongozi huyo aliyechukua mamlaka kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 amekanusha madai hayo.

Chanzo: BBC
 
Muda wa Afrika kuanza kujitambua umewadia, sasa nchi ya AK imeanza rasmi mchakato wa kusitisha Uanachama wake na ICC namuomba Raisi Magufuli pia aiondoe nchi yetu kwa pia kusitisha Uanachama wetu na ICC!

Raisi Zuma ukimaliza ICC hamia commonwealth pia Waafrika wote tujitoe kwenye huu upuuzi!

Hongera AK!

Respect!
 
Maana yake wakubwa / watawala hawatakuwa na uoga wa kuwauwa raia wa nchi zao kwakuwa hakutawa na chombo cha kuwashitaki na hata katiba za nchi zao mara nyingi utakuta wakuu wa nchi au watawala hawashitakiwi.

Jambo hili si la kufurahia hasa sisi makapuchi/maskini/ tusiokuwa na kinga za kutokushitakiwa/walalahoi na watu wengine wote wanaoangukia katika makundi haya.Inashangaza kidogo kama si kusikitisha wananchi wa kawaida ambao kimbilio lao pekee wanapoteswa na kuuwawa na watawala lilikuwa ICC pekee mahakama zetu zimefungwa na sheria zinazowakinga wakubwa dhidi ya kushtakiwa.
 
Sawa nimekuelewa,

Ila japo kwa kutafakari kwako wewe kuhusu hiyo Mahakama ya ICC unamtizamo gani Mkuu......??
Ni ukweli usiofichika kuwa zina egemea upande mmoja hasa ukiangalia washitakiwa mbalimbali wengi ni waafrika tu!
Sasa je kujitoa ni suluhisho la tatizo?

Kuna mambo mengi ambayo mataifa yaliyoendelea yanavifanya ili kukidhi matakwa yao na usipotekeleza unawekewa vikwazo vya uchumi kama zimbabwe na kuishia kuteseka!Ni vema tunapotaka kujitoa kuangalia je tunaweza kuhimili mikiki baada ya hivyo vikwazo?

Nafikiri unaelewa hatua zinazoendelea kuchukuliwa dhidi ya burundi

Kwa tanzania bado hatujafikia hatua ya kuleta jeuri ukilinganisha na south africa

This is my opinion....
 
Ahsante sana Mkuu nimekuelewa vizuri,
Japo kama sisi Waafrika tutategemea misaada yao mpaka lini ikiwa tunarasilimali nyingi ambazo huwa tunanyonywa na hawa Wazungu....???

Na kama Nchi zote za Africa Kwa sauti ya pamoja kujiondoa na hiyo ICC, Hao Europe na paka Wao Marekani hawatoweza kutuletea wimbo Wao wa vikwazo au kutunyima misaada yao zaidi ya kutubembeleza tuu tusijiondoe kwenye hicho kichaka Chao cha ICC.
Sababu wanajua wapo ambao tutakao shirikiana nao kwenye biashara, na vile vile wanajua Kuwa sie waafrika ni watu muhimu sana kwenye mambo ya Kibiashara kutokana na Rasilimali tulizo Jaaliwa
 
2+2=4 full stop. tukisema 5 ni kosa hatuwez kung'ang'ania jibu liwe 5 kisa jirani yako kasema 5 alaf kapewa marks. Ni kwel trend inaonyesha wanaopelekwa huko wengi ni viongoz wa afrika na ni kweli waliofikishwa huko wametutendea isivyo mema, kwan wametuua, wametutesa, wametuachia ulemav na umasikini wakutupa na wala hawajaonewa na wameyatenda haya wakijua ni wanachama wa ICC, je nje ya icc si watatufanya kitu mbaya zaid?
mimi nadhan tuendelee kuwa wanachama wa icc lkn tukiendelea kuwakaba koo na wengine nao washtakiwe. huo ndo utaratibu
 
Na unapo sema wengine washtakiwe kama kina nani.....???
 
Ahsante sana Mkuu nimekuelewa vizuri,
Japo kama sisi Waafrika tutategemea misaada yao mpaka lini ikiwa tunarasilimali nyingi ambazo huwa tunanyonywa na hawa Wazungu....???

Na kama Nchi zote za Africa Kwa sauti ya pamoja kujiondoa na hiyo ICC, Hao Europe na paka Wao Marekani hawatoweza kutuletea wimbo Wao wa vikwazo au kutunyima misaada yao zaidi ya kutubembeleza tuu tusijiondoe kwenye hicho kichaka Chao cha ICC.
Sababu wanajua wapo ambao tutakao shirikiana nao kwenye biashara, na vile vile wanajua Kuwa sie waafrika ni watu muhimu sana kwenye mambo ya Kibiashara kutokana na Rasilimali tulizo Jaaliwa
Ingekuwa hilo la kukubaliana kwa kauli moja litawezekana mambo yangekuwa mazuri!
Kama hata EPA tu inataka kuleta mgigoro sababu wengine walikwisha saini sembuse bara zima! nafikiri ni ngumu sana......

Nafikiri utakuwa mwanzo wa kugombana wenyewe mwisho wa siku wote tutajikuta tumedondokea mikononi mwao! Tuna rasilimali ya kutosha lakini hilo halitoshi kuleta jeuri kutokana na technologia yetu ya chini

Kusalitiana wenyewe+ teknolojia ndogo ndio vitaendelea kutufanya tunakuwa watumwa kwa wazungu
 
waziri anapeleka mswada bungeni,bunge likilidhia watajitoa na Zuma ameulizwa kwa nini hii hoja umeileta baada ya kutoka kenya..wakati Kenyata haitaki hata kusikia kwa sababu ya kesi yake je Zuma umeshawishiwa au unajitoa kwa maslahi ya wa Afrika kusini? tusubiri bunge litaamua nini..
 
Baada ya Burundi kuweka wazi nina ya kujiondoa katika mahakama ya makosa ya kiarifu yaani ICC wiki hii Afrika Kusini kama taifa lenye nguvu kiuchumi hayo imetangaza kujitoa katika mahakama hiyo, na mataifa mengine ya Kiafrika kama Kenya na Namibia yako mbioni kuweka wazi kujiondoa. Je ni suala jema ama nchi za Kiafrika zinajiharibia? Vipi kama Tanzania iwapo nayo ikatangaza kujiondoa je tupo tayari?
 
Viongozi wa Afrika wanajitoa ICC ili wawe huru kutenda maovu dhidi ya raia wake. Nyambafu zao. Raia wa Afrika tusikubali huu ujinga wa viongozi wetu.
 
Baada ya Burundi kuweka wazi nina ya kujiondoa katika mahakama ya makosa ya kiarifu yaani ICC wiki hii Afrika Kusini kama taifa lenye nguvu kiuchumi hayo imetangaza kujitoa katika mahakama hiyo, na mataifa mengine ya Kiafrika kama Kenya na Namibia yako mbioni kuweka wazi kujiondoa. Je ni suala jema ama nchi za Kiafrika zinajiharibia? Vipi kama Tanzania iwapo nayo ikatangaza kujiondoa je tupo tayari?
Hakuna tunachojiharibia Mkuu,

Tena viongozi wote wa Africa wakijitoa lazima lazima heshima irudi hapa Africa,

Tutaheshimiana tuu
 
Back
Top Bottom