Afrika hatuna viongozi bali watawala – prof. Chris maina peter.

Ngofilo

JF-Expert Member
Aug 29, 2010
221
66
Posted by M2S on September 7, 2012 Edit This
Posted in: SIASA NA SERA. Leave a Comment

[h=2] [/h] [h=2]Hakuna shaka yoyote kuwa Afrika ni bara tajiri sana katika suala la rasilimali, ila kinachokosekana ni Uzalendo na usimamizi wa rasilimali hii. Hayo yamebainishwa na profesa wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Prof. Chris Peter Maina.[/h] [h=2]Prof. Chris Peter Maina.[/h]

[h=2]N’guli huyo wa mambo ya sheria, aliyasema hayo alipokuwa anawasilisha mada katika mkutano unao endelea wa JUKWAA LA UCHIMBAJI MADINI, MAFUTA NA GESI Jijini Dar es salaam na kulinganisha utajiri wa lasilimali ya mafuta ya nchi ya Nigeria aliyogubikwa na umaskini wa kupindukia wa wananchi wake huku viongozi wake wakiishi maisha ya kifahari na anasa.[/h] [h=2]Jukwa hili lililo handaliwa na Haki Madini, Interfaith committee on Economic Justice and Intergrity pamoja na asasi ya Policy Forum inawajumuisha wachimbaji wadogo wadogo na wadau kutoka katika nchi za Tanzania, Kenya, Zimbabwe, Afrika ya Kusini, Ghana na Uganda.[/h]
[h=2]Alisema jambo la hatari zaidi ni namna ambayo mikataba ya wawekezaji inavyo fanyika kwa usiri mkubwa wakati kwa upande wa nchi walizotoka wawekezaji unaweza kupata mikataba hii kwa uraisi sana.[/h] [h=2]Profesa huyu alikwenda mbali zaidi na kufananisha mkataba Tata uliotiwa saini nchini Uingereza 2007 na kuufananisha na ule mkataba wa mwaka 1885 kati ya sultani Mangungu wa Tanga na Karl Peters ambao uliwapa uwezo wakoloni kumiliki sehemu kubwa ya Ardhi.[/h]
[h=2]Alisema viongozi wa sasa ambao wanahaminiwa kulinda rasilimali hizi katika bara hili la Afrika hawana upendo na uzalendo wa nchi zao katika nafsi zao bali usukumwa na tamaa za kujinufaisha wenyewe binafsi. Rasilimali inaonekana kama njia tu ya kujipatia nafasi na nguvu za kisiasa na kujitajirisha wenyewe binafsi.[/h] [h=2]Katika kizazi cha kwanza cha uongozi wa Afrika mtu alikuwa anaweza angalau kuona upendo usiyo fichika na uzalendo kwa bara hili la Afrika. Mtu hukuitaji kuwa na taharuma kuweza kujioneya matendo ya viongozi kama Kwame Nkuruma, Jomo Kenyata na Julius Nyerere kuona hisia na athari za upendo wa nchi zao na watu waliokuwa wanawaongoza.[/h]
[h=2]Licha ya makosa na mapungufu yao katika uongozi kwanamna yoyote hile hakuna njia wanaweza kulinganishwa na watawala wa sasa wa bara hili. Hatuna tena viongozi katika Afrika tuna wakwapuaji.[/h] [h=2]Profesa Maina alibainisha kuwa Katiba ya sasa haiweki wazi namna ya kulinda rasilimali za asili na inatoa fulsa kwa serikali kufanya chochote kwa rasilimali bila kuojiwa, akaongeza kuwa Katiba mpya lazima iwe na uwezo kwa wananchi kufanya maamuzi juu ya rasilimali zao za asili.[/h] Mkurugenzi wa Asasi ya Haki Madini Amani Mustafa (kulia) akizungumza jana na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema) Kabwe Zitto na Mratibu wa Asasi ya Policy Forum,Semkae Kilonzo (katikati) kwenye kongamano la siku tatu la wadau wa madini, mafuta na gesi linalofanyika jijini Dar es salaam na kuhusisha wadau mbalimbali.

[h=2]“Sisi ni wadhamini tu katika nchi hii, mali hii yote ni ya vizazi vya baadaye, kwa hiyo tunahitaji kuwa na Katiba ambayo itazuhia viongozi wenye tamaa kutaka kufuja madini.” alisema profesa.[/h]

source JAMII
 
Back
Top Bottom